Jinsi ya kuweka akiba kwa wale tunaoanza maisha

Naomba usikilizwe sana Beberu
 
Haitekelezeki hiyo Mkuu!!

Labda kama huna ndugu wala wazazi wanaokutegemea!!

Mi nashauri ISHI kutokana na nature ya jamii na familia uliyotoka!!

Familia hazifanani halafu wasomi wenye ajira kwenye baadhi ya koo au familia hao ni miungu watu!

Asikudanganye mtu!!!

Haitekelezeki hiyo kanuni kibongo bongo!
 
Kutembea kuanzia kimara hadi ubungo,
Ulikuwa ni mfano tu, lengo lilikuwa kuonesha panga karibu na unapofanyia kazi ambapo hutatumia nauli kubwa au utatumia nauli kidogo sana
 

Ni kweli tuna majukumu mengi, mm hapa naonyesha jinsi gani unaweza punguza hayo matumizi mengi na kubaki nayo machache through vitu kama, kukwepa madem wa mizinga, kupunguza kodi ya nyumba, kupunguza nauli na vitu ka hivyo
 
kumekucha 😅😅😅
 
Sikubaliani na wewe kwa mambo machache. Ila mengi nakubaliana nawe na ahsante kwa ku-share.

Sikubaliani nawe ktk mambo yafutayo;

i) Kuhusu kodi ya nyumba. Sijui utafiti wa 10% umefanyikia wapi, ila naona hili jambo si halisi sana. Hata kama unataka kujibana, ila ni muhimu sana kuwa na sehemu nzuri (si ya anasa) ya kukuwezesha kuishi vizuri. Unaweza kuwa na uhaba wa chakula, ila ukiwa na sehemu nzuri ya kuishi itakufanya usijutie sana.

ii) Suala la pesa kwa ajili ya mwanamke. Mtu ambaye hujaoa, kwa nini uendekeze masuala ya kuhonga? Usipendelee kumfanya mwanamke kuwa tegemezi kwako. Mfanye ajitegemee kiuchumi. Najua ki-Africa ni ngumu ila huu ndo ukweli utakaokuweka huru. Labda uwe unamsaidia mpenzi wako kwenye uhitaji ule wa lazima. Kiasi cha msaada inategemea sasa na hali halisi ya jambo husika.

iii) Napendekeza kuachana kabisa na mambo ya michango ya harusi hasa kwa mtu mtafutaji. Ni jambo ambalo halina tija kabisa. Kama unataka ku-socialize na jamii yako tafuta namna nyingine ila siyo mambo ya kuchangiana pesa za harusi. Unaweza kuchangia kidogo kwa watu wachache sana ambao unadhani usipochangia itasababisha moyo wako usiwe na amani kabisa. By the way, usipendelee sana kuwekeza kiwango chako kikubwa cha furaha kutokana na watu. Watu wengi si waungwana. watakuliza tu.

iv) Ukiondoa masuala ya michango ya harusi, badala yake ongezea kipengere cha kuwasaidia wahitaji wagonjwa utakaoweza kuwasaidia kadri utakavyojaaliwa.
 
Shukran kwa mchango wako uliojaa hoja nzito,

Kuhusu swala la chumba nimesisitiza kiwe livable na pia kisiwe cha bei kubwa na ndo mana nikasema 10% ya kipato,
Kuhusu wanawake licha ya kuwa upo sahihi kwa mtazamo wako ila jamii yetu bado haijafika hio level, kwa hio tuanze kwa kuwapunguzia kwanza kuhonga mpaka hapo wataposhtuka hatuhongi tena

Kuhusu michango ya harusi naungana na wewe, ila kwenye kukwepa lawama ndo mana nimesema toa tu 10k usepe zako usibebe kadi unless ni mtu wa karibu

Yote kwa yote mchango wako ni mkubwa, na wenye madini ya kutosha ambayo mtu akiyafuata atakuwa bora zaidi na zaidi
 
Yote Kwa yote saving 1.8 M per year won't take you anywhere..take it or leave it

Saving ya 2M kwa mwaka,
Unaenda Njombe unapanda miti eka 10, baada ya miaka 10 unauza kwa si chini ya 50M, imagine now una 30, at 40 una 50M, sasa kama kila mwaka ulikuwa unawekeza kwenye kitu kikubwa, utapofika miaka 50 una zaidi ya 500M, utajiri unajirundika sio wa kuja mara moja
 
Kuhusu swala la imani nazungumzia Sadaka ,zaka au fungu la kumi. 10% ya pato lako iende kwa Mungubaba..! Japo kuna miezi inakua migumu sanaa.. But Muhimu
 
Asante
 
kilimo cha pdf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…