Urban Edmund
JF-Expert Member
- Mar 20, 2018
- 2,250
- 3,607
kuweka akiba bila mipango endelevu ni sawa na mwanafunzi anaejituma kusoma na kujua vitu vingi lakini siku ya mtihani kushindwa kupambana kufanya mtihani vizuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Saving ya 2M kwa mwaka,
Unaenda Njombe unapanda miti eka 10, baada ya miaka 10 unauza kwa si chini ya 50M, imagine now una 30, at 40 una 50M, sasa kama kila mwaka ulikuwa unawekeza kwenye kitu kikubwa, utapofika miaka 50 una zaidi ya 500M, utajiri unajirundika sio wa kuja mara moja
Umenena vema sana mkuuUkifanya hivyo utaishi limited life na kipato chako hakitakuwa. Ili uchumi wako ukuo pamoja na maendeleo yako binafsi unahitaji challenges.
Nachoweza kuwashauri:
Moja focus kwenye kukuza kipato kila siku badala ya kufocus kubana matumizi.
Pili, Weka matumizi mdabala wa matumizi yasiyo ya muhimu, hapa nazungumzia kuwekeza katika assets.
Tatu, tumia utashi wa kupembua kabla haujafanya maamuzi ya kulipia kitu chochote. Jiulize maswali kama kitu hicho unachotaka kulipia unahitaji au unakitaka tu?
Kuwa na roho ngumu na isiyo mbaya, kuna mambo mengine bila kuwa na roho ngumu hutoki.
Ukifanya hivyo utasave huku ukifurahia maisha na ustawi wako ukiendelea vizuri.
Huu siyo utaratibu wa HUSTLER mpenda maendeleo. Hustler anakula mara mbili tu, asubuhi na jioni. mchana ni muda wa kazi, utakula saa ngapi?Naungana na ww kwa baadhi ya vitu vingine siafiki;
Msosi kupika labda jioni na chai ya asubuhi mchana unakula huko huko kazini!
Umesema usigongee demu lodge 🤔🤔aisee siwezi peleka demu geto hawa wa kwa chalamila wanatabia za kuzoea au kung'ang'ania, Kuja mara Kwa mara napenda kuyamaliza lodge
Pombe kama unapenda tumia ila kwa umakini
Harusi na misiba hapa inategemea, usipawekee sheria kiasi hicho ni sehemu ya kudeal nayo kimkakati
Lazima. Mbinu zisipobadilika, Waafaa na hiyo familia.Mkuu hizo ni mbinu kwa wanaoanza maisha, ukiwa na familia mbinu hubadilika aiseee
Tule mbususu kwa kuzikopa mpaka zikome.Ndio mkuuu
Huu siyo utaratibu wa HUSTLER mpenda maendeleo. Hustler anakula mara mbili tu, asubuhi na jioni. mchana ni muda wa kazi, utakula saa ngapi?
Asubuhi pika msosi wako fresh na kula ushibe. Nenda kwenye kazi za watu. Jioni pika na ule ushibe. Mchana ni mwendo wa maji tuuu😡😡 mambo ya kuwaiga wazungu wanaokula kila baada ya masaa mawili sisi Waafrika yanatumaliza kiuchumi. Fikiria babu wa babako alikunywa chai wapi? Alikula chakula cha mchana wapi na jioni alikula nini?
Mambo ya mademu kila mmoja abebe mzigo wake.
Unachemsha usiku asubuhi yamepoa unabeba kwenye recycled bottle 1.5 litres. Yatosha kwa siku.hayo maji ya mchana unanunua au unakunywa ya bombanii?
HIYO CONSISTENCY SINA AISEEEE,,,ILA NIMEJIWEKEA BUDGET YA KUNUNUA MAJI KWENYE KILA KIPATO NINACHOPATAUnachemsha usiku asubuhi yamepoa unabeba kwenye recycled bottle 1.5 litres. Yatosha kwa siku.
Ya bombani ndiyo safiiiihayo maji ya mchana unanunua au unakunywa ya bombanii?
Hapano kwenye fridge Cha hifadhi mboga umedanganya maana unaweza Kuta ukahifadhi kibakuli Cha hero kwa umeme wa elfu2Habari zenu wakuu, ni jioni sasa, akili yangu inaniambia wacha nishee nanyi Watanzania wenzangu kitu kimoja kuhusu kusave pesa ili kuweza kufikia uhuru wa kiuchumi na kutimiza ndoto zetu iwe kujenga, kununua gari au kuanzisha kampuni.
NB: This is not financial or life advice, za kuambiwa changanya na zako
#1 Kodi ya nyumba
Ukitaka kusave pesa hapa ndio pa kuanzia, angalia unakaa nyumba ya kodi kiasi gani. Sheria zote za uchumi zinasema kuwa hakikisha kodi ya nyumba yako haizidi 10% ya kipato chako cha mwezi, kwa maana kwamba, kama unalipwa laki tano basi hakikisha kodi ya chumba chako kwa mwezi haivuki Tsh. 50,000/-, Kwa sababu pesa hii haizalishi chochote kile, na uzuri kwa Tanzania yetu maeneo mengi tu vyumba utapata hadi vya 20k, kikubwa ishi kwenye kipato chako.
Ubaya wa kukaa nyumba ya gharama kubwa itakuacha na % chache za kutumia kwenye vitu vingine vya lazima, chumba unachoishi kikubwa kiwe livable tu, (nazungumzia bachelors).
#2 Nauli ya kwenda kazini kwako
Hapa sasa tazama vema, unafanya kazi point A ila unakaa point C inabidi uanze kupanda magari mawili kila siku kwa nauli ya zaidi ya Tsh. 2,500/- sawa na Tsh. 75,000/- kwa mwezi, na wengi wetu tunatumia nauli kubwa ili kukwepa kodi ya chumba ambayo utakuta ni Tsh. 20,000 au Tsh. 30,000.
Chukulia mfano, mtu anaefanya kazi Ubungo kisha akaamua kukaa Kiluvya ambako unapata Master nzuri ya Tsh. 70,000 ukakwepa kupanga maeneo ya Kimara ambako ungetembea kwenda kazini kwenye kodi ya Tsh. 100,000/ kwa chumba chenye hadhi hio hio.
Mtu huyu kwa mwezi anatumia nauli ya Tsh. 75,000 + Tsh. 70,000 ya kodi jumla ni Tsh. 145,000, wakati angepanga Kimara gharama ingekuwa Tsh. 100,000 kodi + 0 nauli jumla ni Tsh. 100,00 tofauti Tsh. 45,000 ambayo kwa mwaka ni Tsh. 540,000/- (hii pesa unanunua shamba heka 5 Njombe huko upande miti ya mbao). Panga karibu na kazini, utasave nauli.
#3 Chakula
Kula wakuu ni muhimu tule sana, ila kwenye kusave sasa kuna vitu nakushauri uvifanye ili uweze save pesa ya chakula;
~ Pika chakula chako mwenyewe kwa ladha na usafi wa hali ya juu.
~ Nunua chakula kwa bei ya jumla, mfano mchele kg 10, Unga kg 5 na kama unaweza.
~ Kama unaweza nunua fridge, litakusave sana kwenye mboga. Mjini hapa mboga majani ni jero ila ukinunua huwezi imaliza mara moja au 2, cha kufanya nunua fridge, nunua nyanya kwa bei ya jumla sokoni eg kisado, nunua karoti kwa bei ya jumla, hoho vile vile kisha ziweke kwa fridge, ukinunua nyama 1/2 kilo utaweza kula hadi mara 6 achana na matajiri wa JFwanaokula kg nzima mara moja), chemsha maharage yako hata kilo nzima (hapa utasave pia cost ya gas kama kwenye nyama pia) kisha yajaze kwa fridge utakula mwezi mzima, (usiyaunge, utayaunga unapotaka kula).
Hapo kwenye chakula tunategemea usave mpaka 80,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na 960,000 kwa mwaka, na ile 540,000 hapa tunakuwa tumesave Milioni 1.5 kwa mwaka.
#3 Mavazi
Hapa ndugu zangu, nunua nguo kali za kudumu, kwa wanaume, nunua shati zako za dukani japo 5 nunua suruali zako kali japo 5, kisha nunua kiatu cha ngozi kikali, utakuwa smart muda wote na pia itakuepusha na gharama za kununua nguo kila mwezi. Hapa utasave walau Tsh. 300,000/ kwa mwaka, na ile ya juu basi jumla utakuwa na Milioni 1.8.
#4 Kuendekeza wanawake
Hapa kukwepa vizinga simply unashauriwa ufanye yafuatayo;
~ Kuwa na mwanamke mmoja anaetoa mzigo bila kubania, usiwe na michepuko sabisa, pakuvuja pakiwa pengi itakuwa balaa.
~ Kuwa na mwanamke mpambanaji, usichukue beki tatu aisee, usibebe mwanamke wa kumlipia kodi aisee, mwanamke awe anajimudu, wew uwe unaweka chachandu na mahitaji madogo dogo. Bora kuwa single ila sio na beki tatu (Ukweli unauma najua).
~ Tenga bajeti ya mpenzi wako, eg ukisema kwa mwezi umpe mpenzi wako Tsh. 50,000 ya mahitaji, ikizidi hapo tangaza huna hela hadi mwezi ujao, kama ni muelewa wewe mwambie mapema kabisa, mimi kwa mwezi nakupa Tsh. 20,000 ya kusuka, Tsh. 10,000 ya vocha na Tsh. 20,000 ya extra then kila mwezi wewe mpe hiyo pesa halafu usisumbuane nae.
Mwambie kwa level yangu mama mi nakupa Tsh. 50,000 kila mwezi basi, ila kama uwezo wako wa Tsh. 10,000 mwambie kabisa (Hapa sheria ni isizidi 9.8% ya kipato chako, kama mnakumbuka Mungu tunampa 10% kwa hiyo hatuwezi mpa mwanamke kiwango kinachozidi hapo.
~ Usigongee mwanamke lodge (haitaki maelezo hii) mlete geto.
~ Mwana akija apike mwenyewe asinunue chakula, hataki afie mbele.
~Usiwe na mwanamke wa mbali mfano mkoa mwingine, hata kama upo naye mji mmoja hakikisha nauli kumleta geto haizidi Tsh. 2,000 kwa bodaboda na Tsh. 1,000 kwa daladala. Hili halina maelezo wote tunajua kauli ya sina nauli.
~ The best of all kama ukiweza kuwa single tu, kikubwa usiwe Punga au Chaputa
#5 Pombe
Simply acha pombe utasave at least Tsh. 200,000 kila mwezi na kwa mwaka Tsh. milioni 2.4, hivyo na ile Tsh. milioni 1.8 tunafika Tsh. Milioni 4.2 ambayo unaweza fanyia kitu kikubwa sana, hapo bado sijasemea kwa pesa utakayosave kwa mwanamke.
#6 Michango ya harusi na Misiba
Ndugu yangu michango ya sherehe ni muhimu kwa umoja wa taifa, lakin hakikisha unapunguza sana idadi ya michango. Epuka kwenda kwenye sherehe zisizo na umuhimu, mtu akikuletea kadi ukaona huyu humtaki, usipokee kadi, mpe kiasi fulani cha kuzugia kisha ondoka.
Mfano kama kadi ni Tsh. 50,000 wew mpe Ths. 20,000 kisha mwambie akatafute mbele (make sure unasave ya kutosha kwa ajiili ya harusi yako au usifunge kabisa maana watarudisha tena 😂). Same kwenye misiba, usiwe pedeshee ndama mtoto ya ng'ombe (hapa sheria ni michango ya kadi haitakiwi kuzidi 3% ya kipato chako cha mwezi)
Ukifanya hivo utasave kiasi cha kutosha, kuweza kufanya maendeleo.
Mpaka wakati mwingine tena, ulikuwa nami Beberu J,
Bye bye 👏
Lakini Kuna watu wanatafuta 500k wafanye mtajiYote Kwa yote saving 1.8 M per year won't take you anywhere..take it or leave it