zerominus10
JF-Expert Member
- Aug 25, 2022
- 8,142
- 13,721
Mpige kabari akupe Pesa zote basiEti profeshono. Nna njaa halafu unaniita ujinga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpige kabari akupe Pesa zote basiEti profeshono. Nna njaa halafu unaniita ujinga
Za kwake au za kwangu?Mpige kabari akupe Pesa zote basi
Maana yao ya kujaza tena taarifa za elimu ni nn wakati ulishajaza?Siku ulipojaza taarifa kwa mara ya kwanza ku-join NSSF taarifa zako ziliingizwa kwenye system yao,so kama ulijaza una Degree basi System inasoma hivyo kwamba wewe Professional,leo huwezi kwenda kudai ukisema ni Fomu 4,shida ndio hiyo,Fomu 4 kushuka chini ndio unachukuliwa kama Kibarua(Non Professional)
Zozote Jamaa hapo anataka aelekezwa wanapokodi Gobole akajitose maana haiwezekani kazi afanye yeye Pesa wakae nazo watu wengine na kumpatia hawataki wanamwekea masharti ya kiduanzi na Pesa ni za kwakeZa kwake au za kwangu?
Wanataka wapunguze mpungaMaana yao ya kujaza tena taarifa za elimu ni nn wakati ulishajaza?
Ha ha haaa. Ila sio fair. Mazingira ya kutoa hela ni magumu mno warahisishe mchakatoZozote Jamaa hapo anataka aelekezwa wanapokodi Gobole akajitose maana haiwezekani kazi afanye yeye Pesa wakae nazo watu wengine na kumpatia hawataki wanamwekea masharti ya kiduanzi na Pesa ni za kwake
Jamani kaka naomba ni connect nipate msaada na Mimi. Mimi ndo nataka kuiombaUlifanya makosa kukubali hiyo laki mbili kwa miezi SITA, kwasabb sasaiv umeshaingizwa kwenye mfumo huo. Isingekua hvo ningekuconnect kwa maneja mmoja wa hapo nssf akusaidie
nlikua na changamoto kubwa zaidi ya huyo mleta maada lkn I managed to solve itJamani kaka naomba ni connect nipate msaada na Mimi. Mimi ndo nataka kuiomba
Huwezi kupata fedha kabla ya kustaafu kwa sababu zile fedha ni kwa wastaafu. Ni duniani kote na siyo Tanzania tu. Halafu huu mtindo wa kulipa kwa mkupuo mtu anapostaafu nao ulikuwa wa kizamani. Kwa uzoefu wangu nchi nyingine mtu akibadilisha sehemu ya kazi basi anahama na mchango wake na atalipwa siku akistaafu tu.Mimi Nilikuwa private sector…
Nilipopata ajira serikalini nikaambiwa mfuko wAngu kwa sasa ni Pssf…
Nikaamua kuwafuata NSSF wa nipe mwongozo wa pesa zangu nilizochamgia kwao….
Wakaniambia kwamba nisubiriiiii hadiiiii ninapostaafuu….….😂😂😂😂😂…
Boss samahani nimekuandikia PMMwaka jana
nlikua na changamoto kubwa zaidi ya huyo mleta maada lkn I managed to solve it
Manager to be heheeeeeeeeeeeeEti profeshono. Nna njaa halafu unaniita ujinga
Na Mimi Nilitaka kuhama na Mafao yanguHuwezi kupata fedha kabla ya kustaafu kwa sababu zile fedha ni kwa wastaafu. Ni duniani kote na siyo Tanzania tu. Halafu huu mtindo wa kulipa kwa mkupuo mtu anapostaafu nao ulikuwa wa kizamani. Kwa uzoefu wangu nchi nyingine mtu akibadilisha sehemu ya kazi basi anahama na mchango wake na atalipwa siku akistaafu tu.
Kuna jamaa aliwahi niambia kwamba kuna sheria ilipitishwa kwamba watu wapate asilimia 33.3 haijalishi ni professional au non-professional.Siku ulipojaza taarifa kwa mara ya kwanza ku-join NSSF taarifa zako ziliingizwa kwenye system yao,so kama ulijaza una Degree basi System inasoma hivyo kwamba wewe Professional,leo huwezi kwenda kudai ukisema ni Fomu 4,shida ndio hiyo,Fomu 4 kushuka chini ndio unachukuliwa kama Kibarua(Non Professional)
Yaah walinilipa kwa kila mwezi yani mwisho wa mwezi kwa Mimi nilikua nachukua laki 2 kwa miezi 6 alafu baada ya hapo kama hujapata kazi basi unasubirbmiezi 18 kama Bado hujapat kazi unaenda kuwaomba uwe unajichangia paka ufikishe umri wanaoutaka waoSijajua ni tsh ngapi kwa haraka haraka , ila alipewa miezi 6 ,baada ya hapo wakakata
Mkuu haya yameandikwa tu ila uhalisia tunajua wenyeweKuna jamaa aliwahi niambia kwamba kuna sheria ilipitishwa kwamba watu wapate asilimia 33.3 haijalishi ni professional au non-professional.
Bob wakati wa kuajiriwa Kuna mambo mengi ajira hakuna kwaio watu wanafanya kazi za ajabu Ili maisha yaende kwaio huwezi kusema Mimi nna degree alafu uajiriwe kama kibarua kwenye kampuni za ujenziSiku ulipojaza taarifa kwa mara ya kwanza ku-join NSSF taarifa zako ziliingizwa kwenye system yao,so kama ulijaza una Degree basi System inasoma hivyo kwamba wewe Professional,leo huwezi kwenda kudai ukisema ni Fomu 4,shida ndio hiyo,Fomu 4 kushuka chini ndio unachukuliwa kama Kibarua(Non Professional)
Wakuu habari zenu. Poleni na majukumu ndugu zangu
Mimi nilikuwa nafanya kazi katika kampuni ya ujenzi ya Waturuki inaitwa Yapi Merkezi inayojenga reli ya SGR ambayo kwa sasa iko lot 3. Kwa sasa kazi imesimama na hakuna kinachoendelea.
Sasa sisi tulipumzishwa kuanzia mwezi wa kwanza kutokana na kampuni kupunguza matumizi na sababu nyingine. Mimi niliajiriwa kama kibaria tu upande wa survey baada ya kupambana kutumia elimu niliyonayo kupata kazi basi niliamua kujichanganya Ili nifanye kazi yoyote nipate mtaji.
Sasa baada ya kufika pale NSSF nikapewa form nikajaza; sasa nikajaza na elimu niliyokuwa nayo yani degree Baada ya mda kufika nikapewa laki 2 wakati nilikuwa nategemea zaidi ya milioni 4. Kuwafata wakasema mimi ni professional kwahiyo nalipwa kwa kikokotoo yaani kwa jinsi walipiga hesabu zao basi nalipwa laki 2 kwa mwezi paka iiishe miezi 6 baada ya hapo kama hujapata kazi tena unasubiri miezi 18 na kama bado haujapata tena kazi unaenda kuwaomba uwe unajichangia paka ufikishe miaka yao wanayotaka.
Sasa wakuu mimi nimeshakaa miezi 6 imeisha na kazi sijapata na njaa inazidi kila nikicheki maisha yamekuwa magumu sana na nilitaka nipate mafao Ili nianzishe biashara vidogo vidogo. Sasa ombi langu kwa wale wazee wa michongo mimi nataka kuzitoa zile pesa kwa njia yoyote mana haiwezekani wakae na pesa yangu halafu mimi sina mtaji wala pakushika sina.
Kama unajua njia ya kuzichomoa huko basi njoo PM aisee tuone tunafanyaje. Nitafurahi kama nitapata msaada wakuu kwa wale watu wa madili aisee nisaidieni wakuu mana hii serikali ya Maza siielewi.
Mimi nimefanya kama kibarua Ili nipate mtaji nianzishe maisha mengine halafu wanazishikilia pesa zangu kisa nimesoma yani sielewi aliyeleta kikokotoo alikuwa na maana gani.
Kama unaweza michongo njoo PM tuyajenge waungwana.
Shukrani