Jinsi ya kuzitoa pesa NSSF

Maana yao ya kujaza tena taarifa za elimu ni nn wakati ulishajaza?
 
Zozote Jamaa hapo anataka aelekezwa wanapokodi Gobole akajitose maana haiwezekani kazi afanye yeye Pesa wakae nazo watu wengine na kumpatia hawataki wanamwekea masharti ya kiduanzi na Pesa ni za kwake
Ha ha haaa. Ila sio fair. Mazingira ya kutoa hela ni magumu mno warahisishe mchakato
 
Ulifanya makosa kukubali hiyo laki mbili kwa miezi SITA, kwasabb sasaiv umeshaingizwa kwenye mfumo huo. Isingekua hvo ningekuconnect kwa maneja mmoja wa hapo nssf akusaidie
Jamani kaka naomba ni connect nipate msaada na Mimi. Mimi ndo nataka kuiomba
 
Huwezi kupata fedha kabla ya kustaafu kwa sababu zile fedha ni kwa wastaafu. Ni duniani kote na siyo Tanzania tu. Halafu huu mtindo wa kulipa kwa mkupuo mtu anapostaafu nao ulikuwa wa kizamani. Kwa uzoefu wangu nchi nyingine mtu akibadilisha sehemu ya kazi basi anahama na mchango wake na atalipwa siku akistaafu tu.
 
Vibarua huwa wanalipwa kwa mkupuo labda ni ile kutofahamu kwako, ungejaza tu kama umeishia form 4 au form 6.

Kaongee na muhudumu vizuri na umhakikishie kumkatia pande upate mpunga wako.
 
wastaafu wakizeeka wanatusumbua mno

Ndiyo maana tunawatunzia
mtakuwa mnachukuwa kidogo kidogo
 
Na Mimi Nilitaka kuhama na Mafao yangu
 
Kuna jamaa aliwahi niambia kwamba kuna sheria ilipitishwa kwamba watu wapate asilimia 33.3 haijalishi ni professional au non-professional.
 
Sijajua ni tsh ngapi kwa haraka haraka , ila alipewa miezi 6 ,baada ya hapo wakakata
Yaah walinilipa kwa kila mwezi yani mwisho wa mwezi kwa Mimi nilikua nachukua laki 2 kwa miezi 6 alafu baada ya hapo kama hujapata kazi basi unasubirbmiezi 18 kama Bado hujapat kazi unaenda kuwaomba uwe unajichangia paka ufikishe umri wanaoutaka wao
Sasa laki mbili kwa mwezi unaishije? Alafu kule NSSF una Hela nyingi yani ukiangalia mfano ukazipata na ukaingia shamba unatoka unakua na mtaji wa waana hii serikali aisee yakinyonyaji
 
Bob wakati wa kuajiriwa Kuna mambo mengi ajira hakuna kwaio watu wanafanya kazi za ajabu Ili maisha yaende kwaio huwezi kusema Mimi nna degree alafu uajiriwe kama kibarua kwenye kampuni za ujenzi
Kwaio unaenda kama darasa la Saba au form 4
Ukianza kufatilia mafao ndio wankupa form za kukaza Tena elimu yako
Sasa kwa wazoefu hili wanlijua Ile form wanajaza form 4 alafu anachonga na HR nae wanamaluza jambo
Sasa sisi tuliokua tumeingia kichwakivhwa mana ajira hizi hatujaziea basi tukajaza tu degree ndio hayo yametokea pesa wamekaza nazo
Mtu unajua kabisa nna milioni 5 kule alafu hauwezi kuzichukua yani unitunzie milioni 5 wakati Mimi nna njaa paka nizeeke ndio unipe kwa nini usinpe saiz nikapambane nikiwa kijana?
 
Wewe ulijichanganya mwenyewe ulitakiwa uandike darasa la saba coz Ile kazi ulivyokuwa unafanya ulikuwa ni kibarua hapo utulie kabisa au Kuna barua unaandika kujicommit kuwa utaajiliwa sehemu yoyote ndani ya miaka mitano na inasainiwa na mwanasheria ndo utapewa Hela hiyo. Pole sana . Welcome to private practice my friend
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…