Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.
Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.
Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.
Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.
Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.
Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Pia soma; Sasa maji ya Ziwa Tanganyika kutumika kwa wananchi wa Jimbo la Kavu Wilaya ya Mpibwe Mkoani Katavi