DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Pengine wenzetu was CCM wanamaanisha yale maji yetu yale....otherwise hawatutendei haki. Malagarasi kachimba 70m tu anapata maji safi, ila kuna vijiji kibao havina maji.

IMG_20211120_142854_201.jpg
 
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazi 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.

Labda upungufu wa uwezo wa kufikiri, vipaumbele, mikakati sahihi, utekelezaji madhubuti.

Mvua tu inaweza ikavunwa na kuhifadhiwa, ukichimba chini kuna maji ya kutosha. Bahari kubwa ya kutosha.

We are just not resourcel enough with our resources.
 
Kabisa, badala ya kufunga kumuomba Mungu mvua, tufunge tumuombe akili ya kuweza kutumia rasilimali tulizonazo.
Nabii Sulemani alimwomba Mungu hekima na maarifa ya kuwaongoza watu wake!

Sisi badala ya kuomba kizazi chenye akili ya kutawala mazingira yetu, kinyume chake kila mara tumekuwa tukiomba mkate ambao umekuwa ukiisha na kujikuta tuna uhitaji tena na tena.

In short hata tuombe nini hatujui!
 
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Hebu ita Uber nakupm location yangu uje nikupe dada yangu m'moja uwe shemeji yangu usijali ndoa nitagharamia. Lakini pia agiza mdudu na beer ule kabisa na kunywa muamala nakutumia.
 
kwa kuwakumbusha tu pia TANGANYIKA ndio ziwa pekee samaki wanakufa kwa uzee na kuna samaki humo tangu kuumbwa dunia wanaishi humo
na kuna kina maeno tangu kuumbwa kwa dunia mpk leo hakuna mashua iliwahi fikia ikarudi salama
ni ziwa la pili kwa kina kitefu duniani

hvyo inahitajika MAARIFA ya ziada kuyatoa maji humo
hilo ZIWA lina mambo makubwa si mchezo ni moja ya milango ya kufikia HIDDEN WORD(kuzimu) ndio mana likawa afrca mashariki
na ndio mana NCHI yetu inaitwa NCHI ya MAZIWA MAKUU
hiyo TENDA ya kuyatoa maji humo labda apewe MCHINA
 
Kama Ziwa lingekuwa letu pekeyetu ingekuwa poa lakini Burundi,Drc,Zambia nao wamo.
Ziwa lina kilomita za ujazo 18900, na tunamiliki 46% kwa kila mtanzania kutumia lita 100 kwa siku tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 tu kwa mwaka. Pamoja na hayo, kuna mikataba juu ya matumizi ya maji yanayomilikiwa na nchi zaidi ya moja.
 
Hebu ita Uber nakupm location yangu uje nikupe dada yangu m'moja uwe shemeji yangu usijali ndoa nitagharamia. Lakini pia agiza mdudu na beer ule kabisa na kunywa muamala nakutumia.
Hahaaaa😀😀😀
 
kwa kuwakumbusha tu pia TANGANYIKA ndio ziwa pekee samaki wanakufa kwa uzee na kuna samaki humo tangu kuumbwa dunia wanaishi humo
na inahitajika MAARIFA ya ziada kuyatoa maji humo
hilo ZIWA lina mambo makubwa si mchezo
na tenda hiyo labda apewe MCHINA
Maji yatolewe??,Ili yapelekwe wapi sasa??
 
Back
Top Bottom