sio kweli, fuatilia wakati jews wanakataliwa ulaya US ndie aliyewapokea na hapo ni kabla hata hajawa superpower kipindi hicho super power ni ujerumani, US aliwapokea wayahudi wengi ambao walikua ni wanasayansi kutoka ujerumani na sehem zingine za ulaya mfano einsten aliyeleta mapinduzi kwenye nuclear project na kumfanya muamerica kugundua nuclear weapon, wayahudi hao kwa kiasi walichangia marekani kua super power, hayo mambo sijui ya suel canal na porojo tupu mana kipindi hicho US hakua superpower bado, hadi kipindi US anaibuka superpower tayari wayahudi walikua wameshajenga uhusiano mzuri sana US, ndio mana Uingerrza na Marekani waliamua kuwalipa fadhila kwa kuidhinisha wao kupata inchi, unafikiri walipewa bure bure tu? kasome mchango wa einsten kwa sayansi ya marekani na pia mchango wake kuanzishwa taifa la Israel ndo Utajua Israel na Us wana bond kali kiasi gani?
USA haikupokea wayahudi pekee, ndio maana nakuambia ni maslahi zaidi, scientists wengi tu toka ulaya walipokelewa na US mfano Gugliemo Marconi, huyo ndiye mwanasayansi aligundua kusafirisha taarifa pasipo wire, yani wireless technology , radio, television , wifi, bluetooth n.k huyo ndiye mgunduzi, alitoka Italy na alikuwa muitaliano akiwa anaonekana wa kawaida nchini kwao, alipokelewa US kama raisi, akawezeshwa na akafanya maajabu. 1909 akapewa tuzo ya Nobel.
Ni utaratibu wa marekani wa muda mrefu kupokea wageni, ndio maana leo hii Indians, Chinese, Africans na koo na kabila zote zipo pale, isingeleta maana kuwapokea wengine na kuwakataa Jews, Jews walipokeewa kama watu wengine ikizingatiwa walikuwa adui machoni pa Hitler.
Hakuna u special wowote US aliuona kwa Jews bali ni kuwasaidia na suala zima la kisiasa kama kuonyesha ukarimu wake na kuonyesha ukatili wa Hitler katika mauaji juu ya Jews.
Habari za kunambia myahudi alichangia US kuwa super power hizo ni story za kwenye kahawa wale wazee hata shule hawakwenda miaka nenda rudi wanaamini ujinga waliolishwa.
Utumwa wa watu weusi(black labor) ndio umeinyanyua marekani hapo ilipofikia kiuchumi, walitengeneza miundombinu na kufanya kazi katika mashamba ya pamba, tumbaku n.k...
Marekani inakuwa super power Hitler ana miaka 9, mwaka 1898 US ndio inakuwa giant na kuogopwa duniani, mwaka 1889 Hitler anazaliwa, Jews wanafanyiwa Holocaust na Hitler na kukimbia akiwemo Einsten tayari US ni giant na inaogopeka, sasa hao jews walikuja lini kuitengeneza US kuwa super power? wakati Hitler mwenyewe aliye watesa Jews anakua US ni super power.
Ndio maana wataalamu, wachambuzi wa vita miaka hio walitabiri kama mwisho wa Germany baada ya US kusema wanaingia vitani, kwa maana nguvu ya US ilifahamika tayari.
Mzee napngea kwa fact na historia imelala, mimi sio wa story za kwenye kahawa, nasoma vitabu. Watu weusi ndio wenye mchango mkubwa leo hii US kuwa pale ilipo kuliko hao Jews waliokudanganya.