ngoja nikuulize swali rahisi sana, unasema wayahudi watumie akili, utajiri wao na uwezo kijeshi tuwaone duniani, hivi unafikiri inch ya israel pale middle east inasurvive vipi kwenye ardhi ambayo imezungukwa na inchi maadui pande zote? we unafikiri ni neema za mungu au akili? mfano ingekua sisi tanzania ndo tumezungukwa na waarabu pande zote alaf waarabu ni maadui zetu hivi tungemaliza hata mwezi kweli? we si unaona waarabu walivo na roho ngumu??
Waonyeshe ubabe wao sasa, watu wenye akili nyingi duniani kote, matajiri na wenye ushawishi mkubwa sana katika serikali ya USA, wenye nguvu za kijeshi na hawawezi kupigwa na taifa lolote....🤣🤣🤣🤣
Sasa watumie uwezo wao kijeshi, watumie akili zao ku neutralize hao arabs wasiendelee kuwapiga sio lazima watumie nguvu, maana ya kuwa na akili nyingi ni unakuwa flexible unatumia akili ulizonazo kutatua chagamoto katika mazingira yanayo kuzunguka.
Israel hawana maajabu mzee.
Ngoja nikupe za chini kabisa ambazo niliingia mwenyewe kutafuta info. na huzipati kokote, nachokuambia ni email zilizovuja usiniulize nimetoa wapi..
Kuna kampuni ya Mexico ilikuwa inaitwa HYDRA, hawa jamaa walikuwa wanatengeneza drones, katika kipindi cha mapigano kati ya Georgia na Russia, Georgia walikuwa wananunua drones kutoka Israel.
Hio ni miaka ya 2006-2008 hapo.
Serikali ya Mexico waliweka pesa katika kampuni hio, Zile drones za Israel zilikuwa zinakuwa hacked na Russians na kutua juu ya ardhi, Russians walikuwa wanaingilia signal.
Baada ya Georgia kufanya majaribio katika drones za HYDRA waligundua kwamba zina uwezo mkubwa kiusalama na kiulinzi kuliko drones za Israel, ulipotaka kuzi hack zilikuwa zinarudi base zenyewe zinajiongoza, yaani zikihisi threat au kuwa hacked zinarudi zilipotoka hata kama signal zimekuwa jammed, can you imagine?
Georgia wakaomba wauziwe drones na Mexico, Mexico waka kataa kwa sababu wangeingia kwenye migogoro ya kisiasa na Israel. Kumbe Israel kuna wapiga deal baadhi waliuza codes za zile drones kwa Russians kwa makubaliono Russian atawapa codes za s300 zilizoko kule Syria, na ikawa hivyo, lakini zile drones za Hydra ni noma na nusu, hata kama angetokea mpiga deal ana codes, zilikuwa haziwezi kuwa hacked.
Hivyo Israel na Russia walikuwa wanapiga deal, Israel anamuuza Georgia na Russia anamuuza Syria, ndio lile shambulizi Israel walikwenda kupiga Syria wakasema wame jam s300 kumbe Russia kawapa codes, Iran ikatuma engineers kwenda kufanya maintenance baada ya hapo Israel hawakuweza ku hack.
Mexico ni top exporter wa high tech products katika nchi za Latin America, ndio maana kuna kipondi US walianza kufikiri kutoa viwanda China na kuviweka Mexico.
Nakuambia hivyo kwa sababu, kuna nchi zina tech za juu na wapo kimya, na wanafanya maajabu, yani kuna majitu yana akili duniani, mpaka uwe una chimba vitu, lakini wafuatiliaji wachache ndio wanajua hizi taarifa, wachache ambao ni werevu katika majority ndio wanajua ukweli. Ndio wana monitor hii dunia wakiwacheka wajinga wengi waliodanganywa na medias.
Mi nachimba vitu hadi kwenye vyanzo huvipati google.