Jioni ya leo nina furaja kukutana na Dada mpika Uji

We jamaa ulivyoleta thread ya mchoma mahindi watu tulikuchukulia upo serious na unachoongea. Lakin kumbe umeamua kuzingua watu, no body will take you serious from now on. Ukimaliza thread ya muuza uji, uje tena na thread ya graduate muuza maji ya kandoro.
 
naona kaka umeamua kuwaamsha vijana kwa nguvu zote..

mimi siku hizi graduate akiniambia hana kazi na hana nauli au hela ya soda huwa namtukana moyoni na huwa namuona chizi tu
Usifanye hivyo mkuu waelimishe tu elimu ya chuo imewaathiri...mie wananishangaa ninavyouza mashuka na juice mtaani

love thé love or hâte thé love.....
 
chasha nimekuelewa sana..endelea kutumotivate vijana..
huyo dada akikazana anaweza fungua mgahawa mbeleni.
mafanikio sio lazima uanzie na mtaji wa million..
na uoga ndo unatufanya tushindwe kusonga..mimi kweli sitoona aibu..na watashuhudia mafanikio yangu
 
Tatizo lako wajifanya mjuaji, kisa umekutana na hao wachache wanaofanya tofauti na walichosomea usidhani wengi wanafanya kile ambacho hawakusomea
Unatafuta nini kwenye post za mjuaji? anzisha zako basi unashinda kwenye post za mjuaji unatafuta nini?

Kila nikianzisha Post lazima uwe wa kwanza kuchungulia. achana nazo kama hazikufai dili na zinazo kufaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kudanganya watu ww, hizo ni ndoto za mchana hakuna aliyetoboa kwa kazi hizo
Hahah unatoboa kwa kua na yad ya kuuza magari au kua na hardware ndo utatoboa?
Basi kwanini akina bakhresa na akina Mengi kwanini wasingeanza na kujenga maviwanda makubwa ndo watoboe au Mengi wakat ana hustle kwanini asingeanzisha itv
 
Comrade uko vizur kwenye tafit zako nimependa
 
Nikipata muda ntakuletea ya muuza kahawa mmoja,mafanikio ni kujitoa na kua na juhudi

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Huyo inamaana afanye kazi kila siku no likizo wala kuumwa.
Je akiba ya uzeeni anajiwekea na vp kuhusu bima ya afya? Bora niendelee kuvaa tai tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna muuza uji mmoja hapa Mbeya wallahi akikuuzia uji lazima uombe namba
 
Masanja aliwahi kudanganya watu hivi hivi kuwa ukiwa na laki 5 tu ukakodi shamba na kulima matikiti maji baadaya ya miezi 3 ukiuza unapata faidi ya milioni 6.....hapo umetoa gharama zote...kuna vijana walikopa wengine wakaacha kazi za laki 3 hizi wakajichimbia morogoro..hahahahaa.....waulize saivi wako wapi walipigwa joto la jua balaaaaaa hwana hata senti 5 maisha yamewachapa hatari
 


Ndo hizi mnatumiaga kama Ngao.

Waziri akiwaambia jiajiri mnaanza oo mbona yeye kaajiriwa? Mbona yeye hajaanzisha biashara?

Fuata ujumbe achana na mtu.

Ukiambiwa na Waziri jijiri usianze kwamba yeye mbona kaajiriwa?

HIZI HUWA SABABU ZA WENGI KUHALALISHA AIBU NA UOGA WAO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza tambua dhima kuu ya Elimu duniani pote haijawah kua Ajira kumfanya mtu aajiriwe dhima ya Elimu ni kumpa mtu maarifa swala la ajira ni dhumuni binafsi
 
Kuna mwingine nimemsikia asubuhi kwenye radio yuko mwanza yeye kamaliza chuo education yeye anafanya kazi ya kuosha magari...
 
Vijana wengi wanawaza kuajiriwa na kufikiria whitecolar jobs ila wakifika uzeeni wanajigundua ni masikini wa kutupa walishinda wakiuza muda wao.
Huyu dada anafanya kazi kwa masaa machache tu kwa siku tena ni boss wa kazi yake mwenyewe ila anaetumikishwa na kufokea na kuamka asbh asbh kukimbizana anakejeli.

Mungu wabariki Vijana na waepushe na Utumwa wa Fikra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…