Habari za Mida? Wajasiriamali poleni na wale tulio binasifisha muda wetu baada ya sisi kuto kuwa na kazi nao pia poleni.
Jioni hii niko naongea na Dada anaye uza uji baada ya kupita kupata kikombe cha uji. Huyu Dada kasoma Chuo cha Uhasibu Arusha ina baada ya kuhitimu kaamua ajiajiri kwa kupija uji na kuuza.
Anasema kwa siku hipika Themos 15 zile kubwa kabisa za mahotelini. Na kwa sababu ana tumia vikonbe vikubwa basi kila themos hutoa vikombe 8 tu.
Themos 15 x 8 ni vikombe 120.
Vikonbe 120 x 500= 60,000/
Akitoa gharama zote kama Sukari, mkaaa, Siagi, unga, Maji na maziwa basi anaweza tunza faida ya 30,000/
Siku mbaya huwa ni elfu 20 na siku zingine 25.
30,000/ x siku 30= 900,000/
kwa mwezi anaweza pata hiyo pesa.
Mshahara wake kwamwezi anao jilipa ni mkubwa kuliko sisi wavaa tai asubuhi.
NB: Dada kasomea Procurement.
AIBU NA UOGA NDO MUHIMILI WA UMASIKINI WAKO.
Endelea kumuonea aibu Demu wako/Mchumba/mke/Rafiki/jirani yako/wafanyakazi wenzako na kadhalika.
Sent using
Jamii Forums mobile app