Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

P
pole ndio maisha.
 
Usiombe ukae jirani na shule ya nursery vile vitoto🤣vikianza kupiga kelele na hapo unakuta labda siku hiyo umepumzika hutaki kelele utaisoma namba
Licha ya kupiga kelele , mpira wao ukiangukia kwenye fence yako wanategemea uwarushie, na ukiwarushia baada ya dakika tano wamerusha tena.
 
Hii ni kero kubwa kwenye mitaa mingi Dar es Salaam.. Bar,pub,vibanda vya chips,vijiwe vya bodaboda,ufugaji holela, fremu kila kona makanisa na misikiti.
Juzi kati nilipita mitaa ya Leaders,ni eneo zuri nyumba nzuri lakini kuna harufu ya samadi mtaa mzima sababu wa ufugaji wa ng'ombe.
 
Hao wachafu Kuna jamaa Yuko maeneo tena ushuani ana nguruwe 20 hamna hata harufu nguruwe wasaf sana
Kuna sehemu moja mtaa wa pili jamaa mmoja anafuga nguruwe harufu iliyopo pale hata ukiwa nyumba ya 5 kutoka kwake harufu inafika sasa sijui yule jirani wa karibu anaishije harufu mbaya kinoma mimi mpita njia tu sikuhizi nimebadili njia
 
Mimi dirisha langu lilikuwa limepakana na jirani ambaye ni Mkatoliki.

Huyu dingi alikuwa anacheo kuanzia Kanisani hadi kwenye redio Maria.

Basi ilikuwa kila ifikapo night yule mzee anafungulia gospel za Kikatoliki tena kwa sauti ya juu.

Mzee alikuwa ni mtani wangu sa kila nilipojaribu kumuambia kuhusu swala la kelele za redio alijua malalamiko yangu ni sehemu ya utani wetu pia.

Hiyo hali ilienda mpaka ikafika time kutokana na hizo nyimbo kupigwa kila saa namimi nikajikuta nimezikariri nyimbo zake zote.
 
Jifunzeini kununua maeneo makubea nje ya mji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…