Jirani anazalisha K Vant feki na kuziingiza sokoni, nimripoti wapi?

Status
Not open for further replies.
Ni rahisi sana. Usiende polisi kwani anaweza kuhonga na kurudi kuendelea na pengine watamwambia mbaya wako ni huyu. Nenda moja kwa moja kwenye ofisi au kiwanda cha hiyo bidhaa, omba kuonana na meneja masoko umueleze. Si ajabu utapewa na zawadi. Au piga simu waeleze, wakupe utaratibu wa kuonana nao. Hakikisha unawasiliana na uongozi wa juu au mwenye kiwanda kabisa kwa sababu hii hujuma inaweza ikawa inafanywa kwa ksuhirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kwenye kiwanda.
 
Kaushaa
 
Nawashukuru kwa mawazo wandugu hata kwa wale mlionishambulia. Mnaosema nimripoti kwa KVant wenyewe nimeshindwa maana hawana active Website hivyo sijapata namba ya simu wala Email. Pia mimi nipo Kigamboni na Kiwanda kipo Arusha hivyo siwezi kwenda Arusha. Nadhani niache tu kikubwa mnaokunywa KVant mjue mnalishwa madubwasha ambayo hayajathibitishwa na TBS.
 
Kunammmoja alikuwa kmr sijui.kama yupo bado alikuwa na stika za tra ana watu anawalipa kukusanya vidubwasha used vya smart gin aisee ameviuza kmr yaan ubungo mpaka mbezi kama unaonja hii kitu smart g acha namini na ilemambo atakuwa anaonja pia
 
Mkuu usiteseke. Nenda kwa wauzaji wa pombe za jumla omba wakupe namba za watu wa mauzo au supervisor wa K-vant eneo hilo. Kama wakikuuliza shida nini waambie unaulizia taarifa za kutaka kufungua biashara ya jumla kwa bidhaa yao (k-vant). Watakucheki chap kwa haraka.
 
Acha unoko ndugu..

Nchi yenyewe ina ufeki kila mahali, siasa feki, maisha feki, serikali yenyewe ina viongozi wenye ufeki mwingi..

Acha mwamba alishe familia yake..
Siku ndugu yako wa karibu atavyolazwa muhimbili kwa tatizo la figo mkaanza kuchangishwa ndio utakumbuka hii kauli yako,inaweza kuwa wewe binafsi hutumii lakini watu wako muhimu likawapata jambo
 
Acha ukuda kwani walevi wakifa wanafaida gani?
 
Siku ndugu yako wa karibu atavyolazwa muhimbili kwa tatizo la figo mkaanza kuchangishwa ndio utakumbuka hii kauli yako,inaweza kuwa wewe binafsi hutumii lakini watu wako muhimu likawapata jambo
Ukienda hiyo Muhimbili kwa siku wanapokea wagonjwa wapya wa stroke wasiopungua 3.... Wagonjwa figo wa kutosha, wagonjwa wa ini, plus magonjwa mengine yasiyoambukiza ya kutosha..

Moral of the story ni kwamba siku hizi fakes are everywhere....

Mwamba aachwe asongeshe maisha..

Serikali si inasisitiza watu wajiajiri? Let them be.
 
Kwanini naweww usianzishe PEPSI fekibupige pesa????
 
Acha unoko ndugu..

Nchi yenyewe ina ufeki kila mahali, siasa feki, maisha feki, serikali yenyewe ina viongozi wenye ufeki mwingi..

Acha mwamba alishe familia yake..
Yaani aendelee kuumiza watu?
 
akikujua umekwisha
 
ukerewe kwetu Njoo PM please serious
 
Hizo K Vant original zenyewe una uhakika na ubora wake? Usikute hizo feki ni bora na salama kuliko original.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…