Jirani: Kabla ya tukio la mauaji ya wanandoa, kulitokea mauzauza nyumbani kwao

Unapopata Mali, hasa Mali za biashara za madini na majini, watu wake wengi vifo vyao huwa vinaacha maswali mengi, kwa maana Mali nyingi hupatikana kwa maagano, kwa hiyo Mara nyingi sababu ya kifo huwa Ni kisababishi tu,, Ila msingi wa kifo marehemu anakuwa ameshajua siku nyingi atakufaje,,, maana maagano Yana Siri kubwa, kupata Mali,, sio kazi rahisi, na Mali ya namna hiyo huwezi kuzeeka ukiwa tajiri,, lazima pesa itaisha,,, ikudharirishe, au utakuwa maskini ndio baadae ufe
 
Hii ni "version" ya ngapi ya tukio hilo!!???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu mashuhuda waseme dereva wa lori ajali ya wanakwaya njombe alisinzia,wakaabishwa na video. Nawatilia shaka sana
 
Lazima kulikuwa na nguvu za kishetani kwa jinsi tukio lilivyokuwa.

Hakikisha Yesu Kristo yu ndani yako nawe utakuwa salama.
Amen,

Nje ya Kristo ni hatari tupu. Fikiria mtu ameijiwa na shetani, kisha anaenda kutafuta msaada kwa watumishi wa shetani (waganga wa kienyeji). Just imagine!


YESU KRISTO ni BWANA na MWOKOZI
 
Waganga wa Kichawi huenda wamechangia kwa kiasi kikubwa kuleta hilo balaa.

Watu ambao Mungu kawafanikisha badala ya kumtegemea YEYE mnawategemea Mawaliki wa Shetani.

Unatoka nyumbani kwenda kumwita mganga mchawi aje akusaidie. Hakuna msaada hapo bali unaalika nguvu za Giza zikushambulie.

Lengo la Shetani ni Kuuwa, Kuiba na Kuharibu tu basi.

Shetani hana na hatokuwa msaada kwa Wanadamu hata sekunde moja.

Ushirikina unaweza kabisa kuwa chanzo cha hilo tukio.

Tumepewa Jina lipitalo Majini Yote, Simba wa Yuda, Mfalme wa Amani, Ngome imara. Yeye ndiye Kinga yetu sisi Wanadamu.

Isaya 5:13
Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

(Mwenye Maskio)
 
Ikabidi marehemu Swalha ambaye ni mke wa marehemu kwenda kumtafuta mganga na kumtibu mumewe. Baada ya hapo mauzauza yakaanza mpaka wawili hao walipokuja kufariki.

KOSA KUBWA SANA HILI
 
Na CID atageuka FIB kwa msaada wa tunguli.
 
Ikabidi marehemu Swalha ambaye ni mke wa marehemu kwenda kumtafuta mganga na kumtibu mumewe. Baada ya hapo mauzauza yakaanza mpaka wawili hao walipokuja kufariki.

KOSA KUBWA SANA HILI
Tunakusubiri kutoa ufafanuzi wako, Mtaalam Mbobevu wa taaluma ya Science Beyond Material.

Hapa kosa lilikujaje?
 
Tunakusubiri kutoa ufafanuzi wako, Mtaalam Mbobevu wa taaluma ya Science Beyond Material.

Hapa kosa lilikujaje?
Tuanzie hapa

Njiwa aliyefungwa sanda alidondoka getini katika nyumba ya wanandoa hao na kumfanya marehemu Saidi azimie.

Ikabidi marehemu Swalha ambaye ni mke wa marehemu kwenda kumtafuta mganga na kumtibu mumewe.

*Njiwa aliyefungwa sanda alikuwa na tafsiri nyingi.. Inaweezekana nyumba ilikuwa konki hivyo njiwa akakutana na phantom
*Kilichomzimisha Said ni mshuko wa njiwa mwenye sanda ama ni kingine cha sirini? Ambacho ni ngumu kukiweka wazi?

Kuna kukosea masharti na ukikosea unaambiwa kabisa dalili itakuwa ipi. Je njiwa alikuwa dalili?

*Kukimbilia kwa mganga lilikuwa kosa kubwa bila kutafakari kwanza na pengine bila kushirikishana...Hawa ni waumini wa nguvu za giza hivyo njiwa alitumika kama bomu la kutegwa.. Kukimbilia kwa mganga ilikuwa ni kuuza ramani. .. Unampa njia adui ya kumfahamu mganga wako na uwezo wake kifuatacho hapo ni kubutuliwa tuu

*Mnapokuwa wanandoa mmepata mali hasa kama mna background ya mahusiano mengine rasmi yaliyovunjika vita huwa mara 3
1. Vita kwa wenza wenu mlioachana
2. Vita ya kupata mali (washindani na washindwaji)
3. Wivu, husuda, vijicho, vinyongo na rohombaya toka kwa majirani marafiki wanafiki, ndugu na hata jamaa wa karibu
Hapa ni lazima sana kuplay low, kumshika sana Mungu, kuishi bila maringo na show off za mitandaoni na mitaani.. Nknk

Kwenye kubarikiwa kama huko mali, mke mzuri, mume mzuri, maisha mazuri huku nyota zenu wote zinawaka.. Mlinzi pekee ni Mungu mkuu na si waganga wa kienyejj..kuwategemea hao ni kukaribisha vita ambayo hutashinda.. Kwakuwa wewe si mkamilifu una makandokando yako na bado unatafuta mwingjne ambaye naye si mkamilifu akulinde

CC: Mtu chake
 
Case Closed
 
Kila mtu na story yake kwenye tukio hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…