Jirani mkorofi, anafugia ng'ombe kwenye ukuta wangu

Jirani mkorofi, anafugia ng'ombe kwenye ukuta wangu

Habari za leo?

Kuna jirani yangu hapa mtaani anafuga ng'ombe. Kawajengea banda kwenye ukuta wa fensi niliojenga mimi na anajaza kifusi cha mavi ya ng'ombe kwenye ukuta huo na kupelekea harufu kali kwa upande wangu hasa kwenye madirisha ya nyumbani.

Naomba mbinu nzuri ya kumtia adabu iwe ya kisheria au ya kibabe. Maana haya maeneo yamepimwa kwa ajili ya makazi na sio ufugaji wa ng'ombe.

Tulishamwambia awe mstaarabu kwa kutokurundika mavi mengi ya ng'ombe na kuleta kero kwetu, tunaona analeta dharau, sasa nimeamua ubaya ubaya liwalo na liwe.

Asanteni.
Afisa mifugo Kata amefahamishwa kero yako? Jaribu kutoa taarifa kwenye mamlaka kama hakuna hatua inayochukuliwa basi tumia akili
 
Huo ukuta utengenezee namna siku udodonke usiku uuwe hao ng'ombe wake
Alafu asubuhi anza kumlaumu kwanini anafugia ng'ombe kwenye ukuta wako alafu mwambie ona sasa mifugo yako imedondosha ukuta na imekufa .

Mwisho mpe pole kwa yaliyotokea atakuwa kajifunza

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Ushauri huu ndo wa kiCCM haswaa
 
Watu wana stress za maisha ni balaa.. mtu yuko town kiwanja kidogo lakini atalazimisha kufuga kuku, bata, ng'ombe na mifugo mingine. Watu kama siwezi kabisa kuwatembelea kwasababu ya hali ya uchafu kwenye mazingira yao. Lazima pawe pananuka balaa... miji isimamie sheria zake za kutofuga mijini.
 
Ishu ni kufuga ng'ombe au kuweka Banda Kwa kutumia ukuta wako?
Kama ishu ni ufugaji nenda Kwa afisa mifugo kama ni mjini kuna sehemu hawaruhusu kufuga mijini.
Huo ukuta wako umejenga mpakani kabisa au uliacha sehemu yako kidogo?
Tupo ndani ya jiji.
Issue ni harufu kali ya mavi ya ng'ombe pili ana haribu ukuta wangu wa fensi kwa mavi yake ya ng'ombe.
 
Jana kuna sehemu nimepita nikakuta kuna jamaa anafuga ng'ombe kaacha kinyesi mpaka kimefika usawa wa magoti asee nilichukizwa. Nikaamua kugonga hodi walau tuzungumze kwa bahati mbaya hakuwepo. Nikawa najiuliza au pengine hiyo hali ni afya kwa mifugo!!
 
Huo ukuta utengenezee namna siku udodonke usiku uuwe hao ng'ombe wake
Alafu asubuhi anza kumlaumu kwanini anafugia ng'ombe kwenye ukuta wako alafu mwambie ona sasa mifugo yako imedondosha ukuta na imekufa .

Mwisho mpe pole kwa yaliyotokea atakuwa kajifunza

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Dah!! CCM wakuchukue unaziweza fitna kaka mkubwa 😂😂😂
 
Dawa ni kutafuta nyasi kilo moja na sumu ya panya, lowesha hizo nyasi kwa sumu ya panya kwa muda wa saa 2½ kisha vizia usiku tupia vifurushi vya nyasi kwa upande wake.

Asubuhi utapata mrejesho.

Baada ya wiki hiyo kero itakuwa imeisha na utabaki na Amani tele.
 
Sasa ng'ombe wamekosea nini? Aside kuna watu mna roho mbaya.
Wanyama hawana kosa. Mwenyekiti ng'ombe ndio washughulikiwe.
 
Back
Top Bottom