Jirani mkorofi, anafugia ng'ombe kwenye ukuta wangu

Jirani mkorofi, anafugia ng'ombe kwenye ukuta wangu

Habari za leo?

Kuna jirani yangu hapa mtaani anafuga ng'ombe. Kawajengea banda kwenye ukuta wa fensi niliojenga mimi na anajaza kifusi cha mavi ya ng'ombe kwenye ukuta huo na kupelekea harufu kali kwa upande wangu hasa kwenye madirisha ya nyumbani.

Naomba mbinu nzuri ya kumtia adabu iwe ya kisheria au ya kibabe. Maana haya maeneo yamepimwa kwa ajili ya makazi na sio ufugaji wa ng'ombe.

Tulishamwambia awe mstaarabu kwa kutokurundika mavi mengi ya ng'ombe na kuleta kero kwetu, tunaona analeta dharau, sasa nimeamua ubaya ubaya liwalo na liwe.

Asanteni.
Tafuta chatu mkubwa, anayeweza kummeza mbuzi,akila mbuzi wake wawili tu,atapata akili ya kuishi na jirani zake🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Ishu ni kufuga ng'ombe au kuweka Banda Kwa kutumia ukuta wako?
Kama ishu ni ufugaji nenda Kwa afisa mifugo kama ni mjini kuna sehemu hawaruhusu kufuga mijini.
Huo ukuta wako umejenga mpakani kabisa au uliacha sehemu yako kidogo?
Tatizo limeanzia kwenye ujenzi wa ukita inaonekana jamaa kajenga mpakani kabisa
 
Hahaha!! Hii Kali mnoo.ilikuaje
Alikuwa anamwaga kinyesi cha ngombe kwenye ukuta,ukimwambia anasema kwamba hicho kinyesi ukutani kwangu kinasogea chenyewe ila yeye huwa anamwaga kwenye shamba lake.

Nilichukua vijana wawili na mimi tukawa mtu tatu nikakikusanya chote nikaenda kumwekea mlangoni kwake kabisa,aliponiuliza sikumjibu chochote. Akajaribu kuwatisha wale vijana nikawaambia wale vijana wamsikilize aliyewapa kazi😅😅 mpaka leo akaamua kujenga ukuta kati yake na mimi ili aendelee kumwaga mauchafu yake.
 
Mi nina jirani kama wako yeye kaamua kufuga nguruwe bado namfikiria kumtia hasara, kuna mwingine alikuwa anakuja kuchungia mbuzi wake kwenye kiwanja changu nikamwambia hakusikia, nlinunua debe la mahindi nikaliweka maeneo mbuzi wakaja kula mahindi yote, kiwanja changu kipp mtoni wakaenda kunywa maji, jioni akaja kuwachukua wameshiba balaa, usiku alikuta maiti ya mbuzi zaidi ya 10
Ukisikia roho mbaya ndio hiyo.
Ulikuwa unapungukiwa Nini wakichunga kwenye eneo lako?
 
Habari za leo?

Kuna jirani yangu hapa mtaani anafuga ng'ombe. Kawajengea banda kwenye ukuta wa fensi niliojenga mimi na anajaza kifusi cha mavi ya ng'ombe kwenye ukuta huo na kupelekea harufu kali kwa upande wangu hasa kwenye madirisha ya nyumbani.

Naomba mbinu nzuri ya kumtia adabu iwe ya kisheria au ya kibabe. Maana haya maeneo yamepimwa kwa ajili ya makazi na sio ufugaji wa ng'ombe.

Tulishamwambia awe mstaarabu kwa kutokurundika mavi mengi ya ng'ombe na kuleta kero kwetu, tunaona analeta dharau, sasa nimeamua ubaya ubaya liwalo na liwe.

Asanteni.
Nilichojifunza kwa jirani akikuletea mpelekee na yeye mtaheshimiana tu. Ila ukiwa mnyonge imekula kwako.

Utakuja kila siku kulia lia huku. Me wangu alikuja siku moja kunipandishia kwangu. Kaelewa kwamba me sio anaogopa hata kupita kwenye uwanja wangu.
 
Hakuna shida cha kufanya mwite mwambie akikataa usigombane weka ukuta urefu wa mnara wa musu wa umeme harufu itakosa kwa kwenda itajazana kwake .imeisha
 
Kaa na jirani yako muone mnatatua vipi suala Hilo... Ikishindikana nenda Kwa mamlaka husika. Ila usifanye Hila kupoteza uhai wa ng'0mbe wao hawana makosa.
Mwisho wa siku wote mtaacha ng'ombe na ukuta Hapa duniani.
 
Ukiendekeza hii misemo utakuja kuchapiwa mke wako kwako. Mwanaume unapambana kitu chochote kisiingie kwenye himaya yako. Inatakiwa ajue anachofanya sio.
 
Back
Top Bottom