Jirani mkorofi, anafugia ng'ombe kwenye ukuta wangu

Tafuta chatu mkubwa, anayeweza kummeza mbuzi,akila mbuzi wake wawili tu,atapata akili ya kuishi na jirani zake🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Ishu ni kufuga ng'ombe au kuweka Banda Kwa kutumia ukuta wako?
Kama ishu ni ufugaji nenda Kwa afisa mifugo kama ni mjini kuna sehemu hawaruhusu kufuga mijini.
Huo ukuta wako umejenga mpakani kabisa au uliacha sehemu yako kidogo?
Tatizo limeanzia kwenye ujenzi wa ukita inaonekana jamaa kajenga mpakani kabisa
 
Hahaha!! Hii Kali mnoo.ilikuaje
Alikuwa anamwaga kinyesi cha ngombe kwenye ukuta,ukimwambia anasema kwamba hicho kinyesi ukutani kwangu kinasogea chenyewe ila yeye huwa anamwaga kwenye shamba lake.

Nilichukua vijana wawili na mimi tukawa mtu tatu nikakikusanya chote nikaenda kumwekea mlangoni kwake kabisa,aliponiuliza sikumjibu chochote. Akajaribu kuwatisha wale vijana nikawaambia wale vijana wamsikilize aliyewapa kazi😅😅 mpaka leo akaamua kujenga ukuta kati yake na mimi ili aendelee kumwaga mauchafu yake.
 
Ukisikia roho mbaya ndio hiyo.
Ulikuwa unapungukiwa Nini wakichunga kwenye eneo lako?
 
Nilichojifunza kwa jirani akikuletea mpelekee na yeye mtaheshimiana tu. Ila ukiwa mnyonge imekula kwako.



Utakuja kila siku kulia lia huku. Me wangu alikuja siku moja kunipandishia kwangu. Kaelewa kwamba me sio anaogopa hata kupita kwenye uwanja wangu.
 
Hakuna shida cha kufanya mwite mwambie akikataa usigombane weka ukuta urefu wa mnara wa musu wa umeme harufu itakosa kwa kwenda itajazana kwake .imeisha
 
Kaa na jirani yako muone mnatatua vipi suala Hilo... Ikishindikana nenda Kwa mamlaka husika. Ila usifanye Hila kupoteza uhai wa ng'0mbe wao hawana makosa.
Mwisho wa siku wote mtaacha ng'ombe na ukuta Hapa duniani.
 
Kanuni ni ile ile bro, dawa ya mshenzi ni kuwa mshenzi zaidi yake.. at the end hata Mungu kaahidi kudeal na washenzi wote effectively.. fata sheria una haki
 
Kaa na jirani yako muone mnatatua vipi suala Hilo... Ikishindikana nenda Kwa mamlaka husika. Ila usifanye Hila kupoteza uhai wa ng'0mbe wao hawana makosa.
Mwisho wa siku wote mtaacha ng'ombe na ukuta Hapa duniani.
Ukiendekeza hii misemo utakuja kuchapiwa mke wako kwako. Mwanaume unapambana kitu chochote kisiingie kwenye himaya yako. Inatakiwa ajue anachofanya sio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…