Jirani mkorofi, anafugia ng'ombe kwenye ukuta wangu


Huu ni zaidi ya uchawi
 
Kwenye kujenga nunua eneo kubwa ili ukijenga fensi Bado kuwepo na eneo la shamba linalobaki nje ya nyumba Yako kuwaepuka majirani wenye visirani kama hawo,niliwai kujenga mahali majirani wote walikuwa wenyeji,wakaanza kuwa wanakuja kutupa utumbo nje kwangu Kila mara.niliuza Ile nyumba nikaapa sitajenga mahali Kuna wenyeji au waswahili. nitanunua eneo kubwa mbali na mji na hakika nitapata Kwa sababu napenda amani na utulivu.
 
Ila kuna watanzania wanapenda shari, wanapenda kupelekana kwa balozi, wanapenda kupelekana kwa Mwenyekiti, wanapenda kupelekana polisi

Angalia tu asije akasema ukuta na nyumba yote ni yake, waswahili wengine bwana! Ni heri ukawa na jirani mwarabu au mzungu hawatakudisturb
 
Mimi ndio nimejenga kwa gharama zangu 100%
Kama walivyosema wakuu humu, huo ukuta ni wa kwenu wote, kila mmoja ana haki nao. Kwenye jamii ya wastaarabu, kabla ya kujenga mngepiga hesabu na kujua unagharimu shilingi ngapi na mnge-share hizo gharama.

Wastaarabu wengine, hata kama ulijenga wewe wanaweza kuja kukulipa kwa kuwa wanaona ukuta unawafaidisha na wao.

Kama mngetumia option ya kuandikishana kwanza kabla ya kujenga ukuta, mngeweka na masharti ya matumizi ya huo ukuta.
 
Kama ukuta utaanguka ama kuharibika sehemu aliyojenga banda basi gharama za matengenezo ziatoka kwake.
Zitatoka kwake kwa sheria au muktadha upi wakati hakuujenga yeye, na wala hajauharibu?? Yaani akisema kuwa yeye upande wake hauna ukuta, hivyo anachokiweka, anakiweka mahali wazi..huo ukuta wa jirani, umejengwa pasipo yeye kushirikishwa, mtambana wapi? Yaani mtamlazimishaje kulipa ukuta usio wake??
 
Kosa nila mbuzi au mfuga mbuzi?
 
Na kama ukuta nimejenga upande wangu kutoka mpaka ulipo kama cm 40 bado atadai ni wake? (mm bado sijajenga uzio nataka nijue ili nisije kujichanganya huko baadae)

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama jirani anakwambia sina pesa wala sina mpango wa kujenga ukuta na mm ningeacha kujenga ukuta?
Mkuu umeshawahi kujenga nyumba yenye fensi?
Yaani kujenga ukuta hadi kuandikishana na jirani sijawahi kuona tangu kuzaliwa kwangu..
 
Ukuta kama upo mpakani ni wa kwenu wote, ila kama umejenga mita 1 kutoka mpakani haruhusiwi kutumia ukuta wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…