Baada ya kusogea na kuhamia nje ya mji kidogo nimeishi kwa amani na furaha sana , eneo langu ni almost kama heka moja hivi ,eneo nililojenga nyumba pako jirani na mtu mwingine, ujirani huo ndio source ya shida yangu kwa sasa.
Jirani yangu kahamia almost mwaka sasa, aisee huyu mbena ni shida , eneo lake dogo kwenye Hilo hilo eneo anafuga nguruwe , ngombe kuku na anaishi na mbwa jitaftie , harufu inayotoka hapo kwake inakera sana, nimejaribu kumuomba nimpe pesa ahame anatangaaza kwa majirani Nina dhalau, nimepandisha ukuta ka nyumba za wauza madawa ya kulevya aisee bado halafu naisikia , mfano nikiwa nje kwangu nateseka sana,sifurahi tena mazingira yangu.
Nipo njiapanda sana je nihame , nikitazama pesa niliyoweka hapo kwenye ujenzi inanipa wakati mgumu, nikijaribu kumvua hataki, nawaz ukija lipuka ugonjwa wa nguruwe nitafte vipande vya nyama za nguruwe niweke hapo bandani kwake TU huu mradi ufe kabisa