Jirani yangu ni mganga, anatufanya tusilale usiku

Jirani yangu ni mganga, anatufanya tusilale usiku

Ni mwaka na miez 2 tokea nimeanza kuishi maeneo haya mwazoni tulikuwa tunaishi vizuri, sababu Mimi napenda maeneo yanayotulia makelele sipendagi kabisa.

Miezi 2 nyuma Jirani yangu aliuza nyumba, yake mtu alionunua Ile nyumba hatumfahamu shida imeanza wiki ya pili sasa usiku hatulali, ni makelele tu Mara ngoma zinapiga usiku majira ya saa 7 au 8 na nyimbo zinaimbwa muda huo, usiku unasikia vishindo vya mtu anakimbia anazunguka nyumba eti anakimbizana na wachawi, Usiku umelala ghafla unasikia vilio Kama watu wanalia hivi sijui ndo wateja wake ni shida.

Baada ya kuulizia Ile nyumba anaishi nani tunasikia ni Mganga wa kienyeji shughuli zake anafanyia pale kwa sasa

Tumeongea na balozi akaongee naye kuhusu tabia yake ya kutupigia makelele usiku tunaona kimya balozi sijui anamuogopa mpaka watoto usiku wanaogopa.

Kama mganga kweli si akaishi milimani uko?

Naomba kuwasilishaa
Bila shaka huyo ni mrokole mtafutie ushahidi mpeleke kwa serikali ya mtaa akishindikana kwa mtendaji kisha kusanya ushahidi huo mpeleke mahakamani kamdai fidia
 
Hakuna Mganga hapo mkuu waganga wanakaa mjini na bando za voda anaweka na kuliwa zile za 75% na analalamika...
 
Bila shaka huyo ni mrokole mtafutie ushahidi mpeleke kwa serikali ya mtaa akishindikana kwa mtendaji kisha kusanya ushahidi huo mpeleke mahakamani kamdai fidia
Jumatatu tunampeleka serikali za mitaa
 
Ni mwaka na miezi 2 tokea nimeanza kuishi maeneo haya mwazoni tulikuwa tunaishi vizuri, sababu Mimi napenda maeneo yanayotulia makelele sipendagi kabisa.

Miezi 2 nyuma Jirani yangu aliuza nyumba, yake mtu alionunua Ile nyumba hatumfahamu shida imeanza wiki ya pili sasa usiku hatulali, ni makelele tu Mara ngoma zinapiga usiku majira ya saa 7 au 8 na nyimbo zinaimbwa muda huo, usiku unasikia vishindo vya mtu anakimbia anazunguka nyumba eti anakimbizana na wachawi. Usiku umelala ghafla unasikia vilio Kama watu wanalia hivi sijui ndo wateja wake ni shida.

Baada ya kuulizia Ile nyumba anaishi nani tunasikia ni Mganga wa kienyeji shughuli zake anafanyia pale kwa sasa.

Tumeongea na balozi akaongee naye kuhusu tabia yake ya kutupigia makelele usiku tunaona kimya balozi sijui anamuogopa mpaka watoto usiku wanaogopa.

Kama mganga kweli si akaishi milimani uko?

Naomba kuwasilishaa
Sasa ukae vizuri asije akakuhamisha hapo mtaani. Na sumu kubwa ya waganga pawe na watu wanaosali kwa Mungu wa Kweli na kutaja taja lile Jina Lipitalo Majina Yote, YESU KRISTO. Hatachukua raundi, atasepa.
 
Back
Top Bottom