Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Big anakungoja korongoni anataka muyajenge saa sita hii usikuTukutane asubuhi, wapendwa. Usiku mwema.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Big anakungoja korongoni anataka muyajenge saa sita hii usikuTukutane asubuhi, wapendwa. Usiku mwema.
poa mwambaTukutane asubuhi, wapendwa. Usiku mwema.
Jomba ile hamsini bora ungeachana nayo tu.[emoji38][emoji38][emoji38]Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida – 07
Nilitazama ndani ya kiroba kile pasipo kujali harufu yake kali iliyonifanya nizibe pua, ndani yake nikakuta nywele nyingi, sikujua ni nywele za nini na za wapi ila zilikuwa nywele ndefundefu za usinga, nguo zilizojifinyangafinyanga na nyama zilizokuwa zinatoa harufu … nyama ya nini hii? Nilijiuliza nikipekua, kidogo nikakutana na kichwa cha mbuzi, kichwa hicho kilikuwa na pembe fupi ambazo zimengushiwa uzi mwekundu, kukibinua kichwa hicho kukikagua na kukitazama vema mara nikasikia kitu kimedondoka mguuni pangu, nikapatwa na hofu kubwa, niliangaza upesi kwa tochi ya simu nikaona sarafu ya hamsini iko chini, sarafu hiyo ni mpya kama imetoka benki muda huu.
Niliichukua sarafu hiyo nikaiweka mfukoni kisha nikaendelea kupekuapekua kiroba kile kwa kijiti, nywele nyingi nisizozeielewa pamoja na manyoyamanyoya ambayo niliamini ni ya mbuzi yule yalijaa humo, kabla sijamaliza zoezi hilo nikasikia sauti za wanaume wakiwa wanateta, wanaume hao walikuwa wanakuja kutokea upande ule wa bar nilikotokea.
Nilitazama upande huo nikaona mwanga wa tochi ukimulikamulika, na pia nikasikia vishindo vya miguu vikisogea kwa upesi, basi haraka nikaona ni vema nikajificha kwani nikionekana hapo hakuna mtu atakayenielewa kuwa mimi ni mshuhudiaji tu, niliona hilo ni wazo bora kwasababu kama ningejaribu kukimbia ama kurejea katika njia yangu basi wangenikuta kabla sijafanikisha hilo na basi wangehisi kuna kitu kinaendelea na mimi humo korongoni.
Nikajibana nyuma ya mti nikatulia tuli niwezavyo, nikawasikia watu wale wakijongea na kujongea karibu huku wanaongeaongea, tochi yao kali inamulika hapa na pale, mwendo wao wa upesi sana.
Majamaa wale walipofika mahali fulani katikati ya korongo lile, katika kumulikamulika kwao huku na kule, wakamulika kile kiroba nilichokuwa nakipekua, nikamsikia mmoja akisema;
“Oya, nini kile?”
Nilitazama nikiwa hapo nyuma ya mti, nikaona kile kichwa cha mbuzi. Sijui akili yangu ilikuwa wapi, kumbe kile kichwa nilikitupia chini nikakiacha papo hapo, sasa kichwa hicho kilikuwa kimesimama chini kikitazamia kule njiani! Nikahamaki na moyo wangu. Niliogopa watu wale wasije kwa karibu kukitazama kwani wakifanya hivyo tu basi ningekuwa nimekwisha. Japo sikuwa kwa ukaribu mkubwa lakini uwezekano wa kuniona nilipojibana ulikuwa ni mkubwa pia.
Mwingine akamjibu mwenziwe: “Mbona kama kichwa cha mbuzi?” Walimulikamulika maeneo hayo ya karibu huku wakiwa wanaongeaongea kuhusu korongo lile, mimi akili yangu ikiwa inaomba tu wasije wakasogea upande wangu, muda si mrefu wakakata shauri wakaondoka kuendelea na safari yao, hiyo ndo’ ikawa ahueni yangu.
Mabwana wale wakawa wameenda wakiwa wemeniachia funzo kubwa kwani nilihisi nimevuka sana mipaka na sikutakiwa kabisa kufanya yale niliyoyafanya. Vipi kama ningeonekana hapo na watu wakanishuku na kunidhuru kwa ulozi?
Nilitoka nikaenda nyumbani moja kwa moja, hakukuwa na kingine siku hiyo, nilijilaza na kwa msaada wa pombe nilizokunywa siku hiyo nikapitiwa na usingizi mapema ya saa saba, hiyo kwangu ilikuwa ni mapema maana si kawaida yangu. Kesho yake nikaendelea na mambo yangu mengine huku nikiwa najaribu kuona ratiba yangu itakuaje hapo karibuni ili nikapate kumtembelea bwana Tarimo kule Muhimbili.
Ikapita siku na masiku, bado sikwenda kumtazama mgonjwa, kila nilipojifaragua na ratiba ya kazi sikufanikiwa kabisa kupata upenyo hata weekend nilihisi uchovu, kiasi kwamba yule jirani niliyeagana naye kwenda pamoja hospitali akajiendea mwenyewe. Bwana huyo aliendea siku tatu tu baada ya siku ile ya Mwananyamala, mimi nikaapa mwisho wa wiki ijayo, yaani weekend nyingine inayofuata, haswa Jumapili, lazima nitaenda kumwona bwana yule kumjulia hali, kwahiyo kwa wakati wote huo nilikuwa naulizia tu na kupewa habari za mgonjwa toka kwenye vinywa vya watu wengine.
Nakumbuka vema, ilipofika siku ya Jumamosi, yani bado siku moja kwenda kumtembelea mgonjwa kama nilivyopanga, nikiwa nipo nyumbani pamoja na familia majira ya asubuhi, tulisikia tangazo la kipaza sauti likikatiza katika mitaa yetu, kwa mara ya kwanza nikadhani ni watu wa kuuza sumu za panya, mende, kunguni na viroboto maana nao siku hizi wamerahisisha kazi zao kwa vipaza sauti lakini kitambo kidogo tangazo hilo lilifika karibu nikalisikia vema, lilikuwa ni tangazo la kukumbusha kikao cha mtaa wa Mashuka, wito ukitolewa na mwenyekiti.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, kikao kilikuwa kinafanyika kuanzia saa kumi jioni kwenye kiuwanja fulani kidogo ambacho kilikuwepo upande wa kushoto mita chache tu tangu ukiacha njia pana iliyosakafiwa kama unatokea kituo cha Kontena kushuka zaidi kule Mashuka. Kiwanja hiko hakikuwa rasmi, kilikuwa kipo tu katika ‘saiti’ ambayo haikumaliziwa, nyumba fulani hivi ambayo ni kama ilitelekezwa kwa muda kidogo.
Agenda kuu ya kikao hiko ilikuwa ni kujadili kuhusu kumaliziwa kwa barabara ile ya sakafu tokea pale ilipokuwa imeishia, mbele kidogo ya geti la lile ghorofa la bweni la Saint Joseph, iende mpaka mwisho kabisa wa Mashuka, yani njia zima kusiwe na vumbi.
Tangazo hilo kwangu likawa ndo’ mara ya kwanza kulisikia lakini nilipouliza, ‘wife’ akaniambia ni siku ya tatu sasa linapita lakini kwasababu majira yake yalikuwa ni mchana, muda ambao mimi sipo home, ndo’ maana sikupata kulisikia.
Basi baada ya hilo tangazo, nilikaa hapo nyumbani mpaka majira ya mchana nikatoka kwenda Goba centre kwenye mnada. Siku ya Jumamosi kulikuwa na mnada hapo na mimi nilikuwa napendelea kwenda kwasababu ya kuchukua vitu vingi vya ndani kwa bei nzuri kuliko kuchuuza kidogokidogo.
Nilienda huko nikafanya kila kilichonipeleka, wakati wa kurudi, kama kawaida, nilipofika kituo cha Kontena nilishuka na barabara ile iliyosakafiwa kuelekea nyumbani kule Mashuka. Nilipomaliza barabara hiyo nikashika njia ya vumbi, kidogo mbele, pale kwenye kile kiwanja nikakuta tayari watu wameanza kusogeasogea, hapo pamewekwa viti kadhaa vya plastiki tayari kwaajili ya kikao.
Mimi nikanyookea nyumbani kwanza kutua mizigo na kuoga kabisa, kisha nikarejea kujumuika na wale watu wa kwenye kikao. Nilikuta tayari wameshaanza.
Kuhusu ile barabara, nilichosikia kwa maneno ya mwenyekiti, ilikuwa ipo katika mpango wa kuendelea kujengwa kumaliziwa lakini changamoto iliyoibuka ni kwamba kuna baadhi ya makazi ya watu na hata pia magenge yamebana hifadhi hiyo ya barabara, haswa huko Mashuka kwa chini, na watu hao si kwamba wamevamia ama wametenda kosa, la hasha, yale ni maeneo yao kabisa kwa haki hivyo kikao kiliitwa ili pajadiliwe na ikiwezekana watu hao waombwe kutoa sehemu ndogo za maeneo yao kwaajili ya kukamilisha mradi wa barabara ile ilosakafiwa.
Kitendo cha serikali ya mtaa kukaa kimya muda mrefu bila kuiendeleza ile barabara, kuliibua minong’ono kwamba pesa iliyotengwa huenda ilishapigwa, kwasababu hiyo kikao cha kuweka mambo wazi kilikuwa ni muhimu.
Watu wakajadiliana na wakakubaliana, wengine waliokuwa wamiliki wa maeneo husika wakiwa pale, mwisho wa siku ikaadhimiwa mwenyekiti atatengeneza pendekezo rasmi na litafikishwa kwa walengwa, lakini wachache waliokuwepo pale wao waliridhia kabisa kugawa maeneo yao alimradi maendeleo yapite.
Baada ya swala hilo kumalizika mwenyekiti alitoa fursa kwa watu kuuliza ajenda zingine muhimu mbali na ile iliyojadiliwa, katika uwanja huo ndipo mjumbe akaibuka na yale ya kule korongoni juu ya namna gani watu wameligeuza kuwa dampo lisilokuwa rasmi. Mjumbe huyo alieleza kuwa korongo hilo limegeuka kuwa kero kubwa ya harufu kwenye baadhi ya maeneo kitendo ambacho ni hatarishi kwa milipuko ya magonjwa haswa kipindi cha mvua.
Swala hilo likaibua mengine, kuna wajumbe wakasimama na kuituhumu pia shule ya St. Joseph wakisema shule hiyo imekuwa ikielekezea uchafu wake wa machemba kule kwenye lile korongo. Punde chemba zao zinapojaa basi wanazifungulia kumwagia korongoni na ndo’ maana halijawahi kuonekana gari lolote la kunyonya maji machafu hapo shuleni tangu kuanza kwake kwa shughuli.
Basi swala hilo mwenyekiti akaahidi kulifanyia kazi lakini pia akapiga marufuku kwa mtu yeyote kutupa taka kule korongoni na endapo yeyote akikamatwa basi atawajibishwa. Katika kutimiza hilo, tena likijumuishwa na swala la wezi majira ya usiku wa manane ambalo kumbe lilishawahi kuongelewa kwenye vikao vya nyuma, mwenyekiti pamoja na wajumbe wakaazimia kuwe na ulinzi shirikishi katika maeneo yale japokuwa mimi mpaka naondoka kikaoni haikuelezwa wazi oparesheni hiyo itaanza rasmi lini.
Nilishika njia ya kurejea nyumbani, nikajikuta napatana na majirani wenzangu wawili wa kuongozana nao, majirani hao nao walikuwa katika kile kikao hivyo tuliongozana kwa pamoja tukiyajadili yale yaliyozungumzwa kikaoni, mwelekeo wetu ukiwa mmoja, hapo majira sasa yakiwa yanaelekea kuwa giza la saa moja.
Kufika getini tulipokelewa na sauti ya kilio cha mtoto, mtoto ambaye mimi sikumfahamu ni nani kwa sauti yake hiyo. Tuliingia ndani tukakuta wanawake wawili wakiwa wanahangaika na mtoto mmoja wa kike anayeishi humu ndani, mtoto wa kama miaka kumi hivi kwa makadirio, ambaye alikuwa analia kwa machozi mengi huku amejishika kichwa.
Mtoto huyo nilipomtazama vema, kwa upande wake ule wa pili, alikuwa anavuja damu kichwani, juu kidogo ya sikio lake la kushoto. Mkono wake ulioshika hilo jeraha ulikuwa umelowa damu vidoleni.
Kabla sijafanya jambo, nikamwona ‘wife’ anakuja kwa kasi akitokea nyumba kubwa, amevalia khanga kiunoni na kifuani, akasema: “Hamna mtu ndani, yupo yule mtoto peke yake. Nimegonga na kuita lakini kimya, mlango ameufunga kwa ndani.”
Katika maongezi yalojiri hapo nikabaini kuwa yule mtoto wa BIGI ndiye aliyemjeruhi mtoto huyo kisha akakimbilia ndani na kujifungia, lakini zaidi katika maongezi hayo nikabaini kuwa mtoto yule wa BIGI kumbe hakuwa mtoto mzima kama wengine bali ana matatizo makubwa ya akili. Hata muda huo tukiwa tunazungumza na kumpatia huduma mtoto yule aliyejeruhiwa, yeye alikuwa dirishani akitutazama. Mimi nilimwona.
Lakini zaidi ya yote, nilijikuta napoteza yale yote niliyokuwa nayajenga kwaajili ya usalama wa familia yangu … si jingine bali jambo la kutokutaka kuwahusisha kwenye lolote lile kuhusu mwenendo wa yule jirani.
***
Ile bike yetu pale nje inahitaj ulinz pia kuchelewa kulala ni jadi yetu.So vitu vinavyopitapita nje lazima tutie jicho kdg.[emoji16][emoji16][emoji16]Huyu msimuliaji ana vitu vifuatavyo:-
1. Ana kiasi kikubwa sana cha umbea, kuacha uaingizi saa tisa usiku kukaa dirishani kuangalia nani ataingia.
2. Ulinzi ungemfaa zaidi kuliko kazi anayofanya kwa sasa, haiwezekani ukeshe usiku kucha kulinda nyumba kwa niaba ya wapangaji wote ambao hawajakuomba.
Msalimie BIGI mdogo hapo ndani 🤣Ngoja nifunge dirisha kwanza namuogopa BIGI
Mwamba anajua kusimulia.Naweka kambi!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Msalimie BIGI mdogo hapo ndani [emoji1787]
😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁🤔🤔🤔🤔🤔😤😤😤😤Ukianza kusoma stori unaweza kudhani jamaa alikua na jirani mchawi kumbe alikua na jirani anaeacha mlango wazi na kumfanya jaamaa aogope pikipiki yake kuibiwa
Summarise then uendelee na shughuli zako, mkuu. Kuna watu wanapenda ikiwa hivi, wataendelea kufuatilia. Quite simple mwanangu, kwanini ujitese.Sawa bhn mkuu ila mkuu hi story ungefanya summary tu kwa kifupi Sana
Story za umughaaka Ni riwaya kbsa usiige
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wanakosoa ila hawaachi kusoma...na hawaachi kutazama kama mwendelezo umetumwa au lah.Nashangaa watu mnapenda story alf kutwa kukosoa kama hupend story usisome tengeneza yako ilio kamili story ikiisha ndo toa comment watu mnasoma story kutafta weakness while hamjawah andika hata story moja
Daaaah nimecheka sana 😂😂😂😂 jf kuna wajuaji, mwanangu uenivunja mbavu sana daaaah aiseeNotorious B. I. G wa Goba
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣