Jitibu U.T.I kwa mmea huu kwa matokeo yenye ufanisi zaidi

Jitibu U.T.I kwa mmea huu kwa matokeo yenye ufanisi zaidi

Hii ni dawa safi sana,kwetu tunauita mkingili(ikingili) ukiacha magonjwa madogomadogo mengi ambayo mmea huu huweza kutibu kwa mafanikio makubwa nilipata jingine kwa rafiki yangu muhindi,yeye kwake ameyapanda kila sehemu kuzunguka ua wake,nikamuuliza kwa nini ameyaweka mengi kuliko maua mengine mazuri?...
Ubarikiwe sana mkuu
 
Hii ni dawa sana Kwa wadada wanapata maumivu Kipindi Cha hedhi
Mkuu tafadhari elezea hapa nikachukue point za ziada. Nimeshampatia dawa moja ila ni ya dharula, nimemtafutia nyingine ya kudumu jana nimeipokea ila sijampatia, sasa ongeza na hii ili tatizo nilikomeshe kabisa. Mara ya mwisho alienda hospitali kwa maumivu
 
mpatakufa..
ni bonge moja ya dawa km unasumbuliwa na mafua chuma jani litafune kisha weka puan km unanusa katika tundu zote..
ni chungu kiasi ila kwa mafua na kuumwa tumbo hii dawa ndio kiboko yake.
Mkuu huu mmea ndo unaitwa mpatakufa?
 
Huo mmea unaitwa "Umulavumba" kwa Kiha .... Tangu utoto nilikuwa nausikia kwa waliotutangulia, siku za hivi karibuni niliamua kuupanda na kujaribu uwezo wake katika tiba, ukisha yatafuna hayo majani ni machungu kuliko kawaida, ndani ya dakika moja utalazimika kuyatema kwani yanawasha na kuunguza kuliko hata pili pili.... Kinachofuata hapo ni kamasi na udenda ukitoka wangu wangu.

Huo mmea kwa vitu kama mafua, kikohozi, vidonda mdomoni ni kanchinya.... breki za nyuma!😎 Nina mpango wa kuupeleka kwa mkemia mkuu ili waufanyie mchakato ili kujua umejengwa na nini.... Inawezekana kabisa hata jamaa yetu UVICO anaweza kudhibitiwa na mmea huu.
 
Ukitafuna unakuwa kama na harufu flani hivi? Na je ni jani linalotambaa kwa muoto wake au linaluwa kama na vimiti
 
Vipi na huu? Nasikia pia ni dawa nzuri sana [emoji116]
Screenshot_20210315-005309.jpg
 
Wakuu habari za leo ! Poleni na mihangaiko ya hapa na pale katika kutafuta riziki.

Nimekaa na kufikiri ni jinsi gani wazee wetu walikuwa wataalamu Wa tiba asilia lakini walikuwa wagumu sana kufundisha watu wakaribu yao ,matokeo yake walikufa na maarifa yao,kwa Leo Mimi sitaki kufanana na hao wahenga...
Huu unaitwa MZUGHWA kule Ushoto.

Msambaa Kama hajapanda huo mmea nje ya nyumba yake Basi sio msambaa halisi
 
Ukitafuna unakuwa kama na harufu flani hivi? Na je ni jani linalotambaa kwa muoto wake au linaluwa kama na vimiti
Siyo jani, ni mmea mti. Ukiuchomeka chini ni lazima utaota tu, unatengeneza majani mapana ambayo ukiyafikicha yanatoa ute unaonata wenye harufu fulani mahususi. Nitaweka picha hapa karibuni.
IMG_20210315_074349_645.jpg
 
Wakuu habari za leo ! Poleni na mihangaiko ya hapa na pale katika kutafuta riziki.

Nimekaa na kufikiri ni jinsi gani wazee wetu walikuwa wataalamu Wa tiba asilia lakini walikuwa wagumu sana kufundisha watu wakaribu yao ,matokeo yake walikufa na maarifa yao,kwa Leo Mimi sitaki kufanana na hao wahenga..
Huu sisi tunaita MPATAKUVA muulize mzanzibar hasa Mpemba atakwambia mbali na hilo lakutibia u.t.i pia ni dawa ya tumbo mzuri sana kabisa ukihisi unatafunwa ni tumbo ikiwa lá kuhara au lolote unalojuwa wewe isipokuwa lá njaa basi chuma na kuchemsha majani yake epua badaaye kunywa au baada ya kuchuma osha majani na uyatwange chukua weka kikombeni na maji kisha unywe maji yake.. Mimi ninao na umekuwa vizuri kabisa.
 
Pia ni dawa nzuri sana ya kutibu tumbo kwa watoto.
Unachuma majani mawili au matatu,unapikicha mkononi kisha unakamulia katika kijiko ili kupata maji yake na unamnywesha mtoto.
Muda si mrefu anapata nafuu kama alikuwa analalamika tumbo linamuuma.
Si kwa watoto pekee inatibu umri wa rika zote.
 
Back
Top Bottom