Jitibu U.T.I kwa mmea huu kwa matokeo yenye ufanisi zaidi

Jitibu U.T.I kwa mmea huu kwa matokeo yenye ufanisi zaidi

Vipi na huu? Nasikia pia ni dawa nzuri sana [emoji116] View attachment 1726002
Huku uchagani wazee wanachemshiaga majani yake kwenye nyama wakati wakichemsha nyama
Pia huu mmea unatumiwa sana kutibu kifua, na tumbo na hivi karibuni ulisemekana pia unauwezo wakutibu corona ukisaidiwa na mimea kama limao, parachichi, opera na mwembe
 
Mkuu tafadhari elezea hapa nikachukue point za ziada. Nimeshampatia dawa moja ila ni ya dharula, nimemtafutia nyingine ya kudumu jana nimeipokea ila sijampatia, sasa ongeza na hii ili tatizo nilikomeshe kabisa. Mara ya mwisho alienda hospitali kwa maumivu

Mkuu tupo mrejesho wa hizo dawa zote
 
mimea huitwa majina tofauti kulingana na sehemu hivyo ndio maana tunatumia sana majina ya kisayansi "common name" hivyo yawezekana mtu akaujua kwa jina tofauti.
 
Wakuu habari za leo ! Poleni na mihangaiko ya hapa na pale katika kutafuta riziki.

Nimekaa na kufikiri ni jinsi gani wazee wetu walikuwa wataalamu Wa tiba asilia lakini walikuwa wagumu sana kufundisha watu wakaribu yao, matokeo yake walikufa na maarifa yao, kwa Leo Mimi sitaki kufanana na hao wahenga.

Tangu nitambue kuwa huu mmea unatibu U.T.I, sasa Nina miaka miwili sijawahi tumia dawa za hospital, ninachokifanya Mimi ni kwenda kupima ili nijue nasumbuliwa na ugonjwa gani, baada ya hapo huwa narudi nyumbani na kuchuma majani haya , nayachemsha na kunywa. Hakika hii ni tiba nzuri sana wapendwa, kamwe hutakaa utake kutumia vidonge vya hospital kwa kutibu U.T.I., ufanisi wake ni zaidi ya % 80.

Matumizi yake ni kama ifuatavyo:

Chuma majani kati ya kumi hadi kumi na tano,baada ya hapo yasafishe kwa maji na kuyaweka katika chombo(sufuria) tia vikombe vya chai vitatu,na injika jikoni hadi yachemke(yatokote), hakikisha maji hayo baada ya kuchemka yanabaki vikombe vitatu, yakishachemka yaepue na toa majani yakae pembeni ili kubaki na kimiminika halisi,kunywa kikombe kimoja kutwa Mara tatu, hakikisha mchemsho unaoutengeneza ni Wa siku moja pekee, tumia dawa hii kwa muda Wa siku tatu hadi tano kwa matokeo yenye ufanisi.

NB. Jina la Mmea huu halijulikani,maana kwa utafiti wangu nimeuliza watu wengi lakini wanaishia kuniambia maua,lakini watu wengi hupenda kuutumia kama fensi/uzio.

View attachment 1725807View attachment 1725809
Ahsante sana aisee
 
Back
Top Bottom