Jitihada za Vyama vya Siasa wanazozifanya kwa wanaume, juu ya uongozi kwa mwanamke

Jitihada za Vyama vya Siasa wanazozifanya kwa wanaume, juu ya uongozi kwa mwanamke

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Suala la uongozi ni hakiya raia wote na sio kwa wanaumme pekeo .
Kwani Haki ya uongozi imetajwa katika Kifungu cha 21 (3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinasema kila Mzanzibari anayohaki ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyoko chini ya Mamlaka ya Zanzibar.
IMG-20250203-WA0022.jpg
Sera na Sheria mbalimbali za Zanzibar zimeelekeza kutambua haki ya mwanamke kushiriki katika demokrasia na uongozi.

Historia inatuonesha kwamba uislamu unaruhusu mwanamke kuwa kiongozi, kwani wapo wanawake kadhaa ambao walishiriki nafasi za mamuzi wakati wa Mtume Muhammad (S.A. W).

Ambapo miongoni mwa wanawake walioshika uongozi ni Bi Khadija mke wa Mtume (S.A.W), mtu wa mwanzo kuupokea Uislamu kutoka kwa Mtume Muhammad.
Pia Bi Asma binti Abu Bakar ndie alieongoza kitengo cha utoaji wa tarifa na habari kwa Mtume ( S .A. W) wakati wa kuhamia Madina.

Hivyo ni wazi kwamba mwanamke anaruhusiwa kushika nyadhifa kwenye uongozi, ingawa hadi leo tumekua tukishuhudia wanawake kadhaa ambao hupewa talaka na waume zao, kwa sababu wameingia kwenye siasa.

Makala hii imewatafuta viongozi wa vyama vya siasa na kutaka kufahamu wanachukua jitihada gani kuwaeilimisha wafuasi wa vyama vyao pamoja na wananchi, kuona wanawashajiisha na kuwapafursa wanawake, waweze kujiingiza majimboni kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mwaka huu 2025.
IMG-20250203-WA0023.jpg

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA
Katibu wa Chama cha ACT -WAZALENDO Mmkoa wa Micheweni kichama Khatib Hamad Shehe anasema wanachokifanya ni kuwapa elimu jamii, ili wawape nafasi wanawake waweze kushiriki kwenye kwenye masuala ya uongozi.

‘’Tunachokifanya kwa sasa tunawahamasisha wanajamii, wawaruhusu wanawake, waweze kuingia kwa wingi majimboni katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 ili kuepuka talaka hizo za ovyo ovyo,’

Maryam Saleh Juma ni Mwenyekiti wa Mkoa Chakechake Chama cha Ukombozi Chauma anasema katika Chama chao wamekua wakiwaelimisha wanawake wanaotaka kugombea kwanza kujielewa, kulinda utu wao na pia kuheshimu maadili ya dini yao, ili waweze kujijengea uwaminifu kwa waume zao, katika kipindi chote cha uchaguzi.

‘’Tumekua tukitoa elimu siku zote kwa wagombea wanawake na waume zao, waweze kuaminiana na kuheshiniana, ili kubakia katika ndoa zao mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ,’’anaeleza.

Habib Ali Khamis katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pemba anasema wanachokifanya wao ni kuwapa mafunzo wanawake wanaotaka kugombea waweze kujitambua, na kufahamu wana nafasi gani katika dini yao, ndoa zao na pia kwenye chama chao.

‘’Tunawaelimisha wanawake kwanza waweze kujitambua na vipi anapata ruhusa kwa mume wake ya kujiingiza kwenye harakati za uongozi,’’anaeleza.
Anasema ikitokea kuna mwanamke wamempa elimu na mume wake hakumpa ruhusa, wanawaita wote wawili na kuwaelimisha, na kuona wanabakia kwenye ndoa yao endapo mwanamke atagombea.

‘’Endapo kama itatokea kunamwanamke anataka kugombea mume wake hampi ruhusa, hatumuachi tu akapoteza ndoto yake, bali tunahakikisha tunamuelimisha mwanamme kufahamu umuhimu na faida za wa uongozi kwa mwanamke,’’anafahamisha.

Anasema watahakikisha wanatumia njia za busara kuwaelimisha wanaume wa Chama chao kuwaruhusu wanawake waweze kujitokeza kwa wingi majimboni katika Uchaguzi wa mwaka huu, ili kuona hakutokei vitendo hivyo vya talaka kwasababu ya mambo ya kisiasa, amemalizia Habib.

SHUHUDA WA ALIEACHWA
Fatma Khamis Rashid (sio jina lake halisi) mkaazi wa Kaskazini Pemba ni mmoja wa walioachwa, na mume wake kwa sababu tu aligombea ‘’Aliniacha mume wangu kisa niligombea,’’anasema.
Uchaguzi ni mchezo wa kidunia kusiwe na migogoro ya ndoa kama hiyo, hivyo ni wakati kwa wanaume kubadilika na badalayake waweze kuwaruhusau wake zao waweze kugombea, ili waweze kuleta mabadiliko majimboni mwao.
Ni vyema kwa vyama vya siasa pamoja na mashirika kama Chama cha Wandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya uongozi kwa mwanamke, ili waweze kutoa fursa kwa wanawake.

WANAHARAKATI
Tatu Abdulla Mselem ni mwanaharakati wa masuala ya Utetezi kwa wanawake, watoto, mayatima na wanaoishi katika mazingira magumu Tujipe Pemba anasema sio jambo la busara katika ulimwengu huu wa uwatandawazi kusikia kama kuna mwanamme amemuacha mkewake kwa sababu tu ameingia kwenye kinyan’ganyiro cha uongozi.

Mwanamke nayeye anaweza kuwakiongozi na akaweza kuleta mabadiliko, hivyo ipo haja kwa viongozi wa vyama vya siasa kuwaelimisha wanachama wao kufahamu madhara ya kukosekana kiongozi mwanamke, ili waweze kuwapa ruhusa.

‘’Ili kuona wanawake wamekuwa na uthubutu wa kuingia kwa wingi majimboni katika uchguzi mkuu ujao, ni lazima vyama vya siasa kufanya jitihada za makusudi kuwelimisha umma hususan wanaume, ili wawpe fursa wenza wao waingie kwenye mchakato wa uongozi bila ya vikwazo vyovyote,’’anasema .

Kaimu Mratibu wa Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Ofisi ya Pemba Amina Ahmed Mohamed anasema moja ya mkakati walioufanya wameanzisha wanaume mabadiliko, kwa ajili ya kuwaelimisha wanaume wenzao, wafahamu umuhimu wa uwongozi kwa mwanamke.

‘’Tumeanzisha timu ya wanaume mabadiliko , ambao watawahamasisha wanaume wenzao, waweze kuwaruhusu wake zao, waweze kuingia kwenye majimbo na kugombania,’’naeleza.

Kombo Khatib Bakar (60) mkaazi wa Kiuyu minungwini anasema ni vyema wanaume kuiga mfano wake, kwani yeye baada ya mke wake kumpa wazo la kutaka kugombea hakumkatalia, bali alimuunga mkono.

Anasema alijitoa kihali na mali na kumsaidia mke wake ambae aligombea udiwani jimbo la Wingwi kwa kipindi chote cha Uchaguzi, ili wweze kupata nafasi ya Udiwani ambayo ndio aliyogombea.

‘’Simkumzui wala sikua na hisia mbaya nae, bali nilimuunga mkono kwa kipindichote, kwani nilikua namini anaweza kupambana,’’ anafahamisha.

Hivyo amewashauri wanaume wenzake kuwa na uthubutu kama yeye, wawaruhusu wenza wao kuingia kwenye fursa mbalimbali za maendeleo ili walete mabadiliko kwenye jamii,’’ anafahamisha.

Na Fatma Hamad-Pemba
 
Back
Top Bottom