hawajazungukwa kila mahali, wameachiwa njia kutoka kaskazini waje kusini, na wengi wamepita njia hiyo. karibia watu 1.1 million wameondoka Gaza ya kaskazini ambako israel ilitoa wito watoke, na wapo kusini ambako misaada inawafikia kupitia mpaka na Misri. kusini kuna geti la mpaka na misri na huko ndiko misaada inaingilia na ndio miaka yote misaada huingilia. wangekuwa wamezungukwa kama unavyosema, hao walioenda kusini wangekuwa wamepita wapi? ukweli ni kwamba, wapalestina ni wabishi sana, wanaiona hatari ila wanasubiri wafe ili dunia iwaonee huruma dhidi ya israel,
wakiona roketi zinarushwa na hamas kwenda israel wanafurahia, israel akisema hapo paliporusha roketi ondokeni nataka kupiga wao wanabaki ili wakifa dunia iwaonee huruma. tangu october 7 hadi usiku wa leo ambao israel imeingia Gaza, roket zimekuwa zikurushwa kwenye makazi ya watu israel, hazirushwi kupiga wanajeshi wa israel, zinarushwa kwenye makazi ya watu, lakini hakuna nchi za kiarabu hata moja zinazosema hamas wasitishe roketi ili mazungumzo yafanyike, wao wanaitaka israel isitishe mashambulizi, utasitishaje mashambulizi wakati adui anaendelea kurusha roketi kwenye makazi ya raia wako?
wanasema wapalestina wanauawa ni kweli wanakufa na ni kitu kibaya lakini kwanini wanatetewa tu wapalestina na kuwaacha raia wa israel (ambao sio wanajeshi) waendelee kupigwa na roketi?umeshaona hata nchi moja ya kiarabu imelaumu hamas kuendelea kurusha roketi? ungelikuwa na akili ungefikiria kichwani mwako kwamba wote wawili wanafanya mabaya na wanatakiwa kusitisha mapigano. Hamas ambao ndio walikuwa wachokozi wanatakiwa kusitisha roketi na warudishe mateka ambao sio wanajeshi ni raia, ili nchi zinazoheshimika ziiendee israel zikimwambia ndugu angalia hamas wamesitisha mashambulizi na wamerudisha mateka, wewe tu ndio unapiga, hebu sitisha mashambulizi. israel ingekataa kila mtu angeishangaa, lakini mtu anasema isitishe wakati hamasi hawasitishi mashambulizi, kwanini wasitishe israel tu wasisitishe na hamas? mmejiona msivyo na akili za kufikiri?
hivi chukulia mfano, idi amin dadaa alivyoishambulia Tanzania, sisi tukampa kipigo, angekuwa hajakimbia uganda akaendelea kurusha makombora mwanza na kagera, na sisi tukawa tunamshushia kipigo, nchi za nje zikasema Tanzania sitisheni mashambulizi, bila kulaani kile amini anachofanya na wala kumwambia amni pia kwamba na yeye asitishe mashambulizi, ungewaelewa? si ungejiona kama dunia nzima imekutelekeza wapo upande wa adui sasa kilichobaki ni wewe kujipigania peke yako kwasababu hakuna atakayekuamulia hatma ya maisha yako? hicho ndicho kinachoendelea pale. hamas wasitishe roketi kwenye makazi ya watu na warudishe mateka ili israel iamue kusitisha mashambulizi kwasababu hata wao wanajua mauaji yameshafanyika sana, wangetamani kusitisha lakini utasitishaje wakati wananchi wako wako mateka gaza na roketi hata leo usiku bado zinarindima kupiga Ashkelon kwenye makazi ya raia?