ukweli wa nchi za jordan na misri kuwakataa wakimbizi wa israel ni kutokana na sababu kubwa zifuatazo
1-usalama wa egypt na jordan - egypt a jordan wanaogopa kuwa wakiwakaribisha wakimbizi wa palestine wanaotokea katika ukanda wa gaza,wakiamini wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi zao kwani wakimbizi hao wanaweza kujiunga upya na kufanya mashambulizi katika adhi ya isarael na Israeli anaweza akalazimika kujilinda kwa kurudisha mashambulizi ambapo atalazimika kupiga ardhi za egypt na jordan kitu ambacho kinaweza kuingiza jordan na egypt kaika mgogoro na israel na kumbuka israel na egypt tayari walishaini mkataba wa amani wa miaka 40 kati yao (40 years old peace treaty)
2- kujirudia kwa historia ya NAKBA,NAKBA ni neno la kiarabu lenye maana ya janga kwa kimombo wanaita catastrophe mwaka 1948 wakati taifa la Israeli linaanzishwa Zaidi ya wapelestine 700,000 walihamishwa katika makazi yao ya awali na ya asili ya jesuralem,westbank na mengineyo. na baada ya vita kuisha wapalestine hawa walikataliwa kuruid na kuishi katika maeneo hayo waliyokuwa wameyakimbia,na hivyo kulazimika kubaki kuishi katika eneo la Gaza,na Gaza ni miongoni mwa eneo ambalo lipo overpopulated kwani Zaidi ya watu milioni 1.5 wanaishi katika eneo lisilizoidi kilometa za mraba 400 (367) na wengi wao wakiwa wakimbizi na wakiishi katika kambi za wakimbizi,hivyo kitendo cha israel kutaka wakazi wa gaza kuodoka inaaminika ni mpango wa Israel wa kutaka kufanya NAKba ya pili kitu ambacho baadhi ya nchi za kiarabu hawataki kitokee
3 wingi wa wakimbizi – nchi kam Egypt tayari ina mzigo mkubwa wa wakimbizi ambao inawahudumia kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo wakimbizi 300,000 iliyowapokea kutokea sudan waliokimbia machafuko wa mwaka huu tu,hivyo kupokea wakimbizi wengine ni pigo kwa uchumi na,usalama wa Egypt na pia jordan tayari ina mzigo mkubwa wa wakimbizi iliyowapokea wakipalestine kabla hata ya machafuko ya wakati huu