Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

Lililopitishwa na Mungu tuliache lipite. Poleni wafiwa haya yote ni kazi ya Mungu haina makosa.
 
Zuga yao ni utabiri, kumbe biashara yao kubwa ni kuuza uchawi/majini
 
Kikwete aongoza mazishi ya Sheikh Yahya Send to a friend
Saturday, 21 May 2011 21:34
0
digg

Hussein Issa
VIONGOZI mbalimbali wa siasa na dini akiwamo Rais Jakaya Kikwete, jana walijitokeza kumzika mtabiri maarufu wa nyota Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia juzi.

Wakati viongozi wengine wakijitokeza msibani hapo tangu asubuhi, Rais Kikwete alishiriki msiba huo kwenye mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Tambaza yaliyoko jijini Dar es Salaam saa 10:00 jioni.

Viongozi wengine wa siasa walioshiriki mazishi hayo jana ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Nec Mkoa wa Dar es Salaam, Adam Madabida na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Kabla ya kupelekwa kuzikwa mwili wa marehemu ulipelekwa katika Msikiti wa Manyema Kariakoo, kuombewa kwa maandamano yaliyojumuisha maelfu ya watu, yaliyoanzia nyumbani kwake Magomeni Mwembechai saa 9:00 alasiri.
Baadaye mwili huo ulipelekwa katika Makaburi ya Tambaza kwa maziko huku ukiwa umebebwa na mamia ya watu waliojitokeza huku wakitembea kwa miguu.

Baada ya kufika katika makaburi, Rais Kikwete aliongoza umati wa watu kuuzika mwili wa marehemu.
Mzee wa upako ahudhuria
Baadhi ya viongozi wa kidini waliofika nyumbani kwa marehemu mapema asubuhi ni pamoja na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba na Mchungaji Adamu Lusekelo, maarufu kwa jina la 'Mzee wa Upako'.

Akizungumza katika msiba huo, Sheikh Simba alisema taifa limepoteza mtu muhimu ambaye pengo lake haliwezi kuzibika kiurahisi.Alisema anamfahamu Sheikh Yahya Hussein siku nyingi na alikuwa mtu wa karibu sana kwake wakishauriana na kutiana moyo katika mambo mbalimbali.

"Hili ni pengo bwana, halizibiki leo wala kesho. Nilimtumia huyu (Sheikh Yahya) kama mshauri wangu wa karibu. Moja ya mambo niliyoyapenda kwake ni kusikiliza anavyosoma Qur'an," alisema Mufti Simba.Akizungumza msibani hapo jana, Mchungaji Lusekelo alisema alioteshwa katika ndoto kifo cha Sheikh Yahya siku moja kabla.

Alisema Mungu alimwotesha kwamba Sheikh Yahya kapanda daraja na alipozunduka kutoka usingizini, akawa anaitafakari na kesho yake saa tano asubuhi, alipigiwa simu kujulishwa msiba huo. "Niliooteshwa na Mungu kuhusu kifo hiki hivyo huyu rafiki yangu ataenda kulala sehemu aliyoandaliwa," alisema

Viongozi CCM, Chadema, CUF
Mwakilishi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Adam alisema marehemu Sheikh Yahya alikuwa mtu wa watu hivyo ni vizuri akaenziwa kwa uchapakazi wake.

Alisema taifa limempoteza mtu mashuhuri na hata kwa upande wa chama (CCM) pia kimepoteza kada wake kwani Sheikh Yahya alikuwa mkereketwa chama hicho siku zote., alisema kwa sababu marehemu alikuwa hapendi unafiki na chuki, ni vizuri vyama vya siasa vikamuenzi kwa kuacha siasa za chuki.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema Sheikh Yahya alikuwa mtu mnyenyekevu hivyo ni bora kila mtu amuenzi kwa matendo yake.Alitaka pia vyama vya siasa kuacha chuki baina yao ili kumuenzi Sheikh Yahya ambaye katika siku ya uhai wake hakupenda chuki na unafiki.

Masheikh wamlilia
Katika tukio jingine vilio na majonzi vilivyotawala msibani hapo jana viliwafanya baadhi ya masheikh kushindwa kusoma Qur'an.Hata hivyo habari zilizopatikana msibani hapo jana zimeeleza kuwa masheikh wengi walioshindwa kusoma Qur'an ni marafiki wa karibu wa marehemu.

Kila walipokuwa wakisoma, walikatizwa na kelele za vilio na simanzi kutoka kwa waombolezaji.Sheikh Yahya Hussein alifariki dunia juzi saa nne asubuhi katika Hospitali ya Mount Ukombozi alikopelekwa kwa matibabu, baada ya kuugua ghafla.
SOURCE MWANANCHI JPILI
 
huyu bwana ni mtoto wa uswazi aliyebahatika kwa nguvu za majini, sasa asipoenda kuaga mshauri wake mkuu na mkuu wake wa majeshi ya giza unafkir itawezekana kweli?
mwacheni tu, hana tumaini pengine popote zaid ya hao majini waliowekwa guard
 
wadau hii imekaaje? i guess haina anya relation na kifo cha Sheikh Yahaya

Mimi naona ina relation, kwa nini?
1. Utabiri aliotoa Sheikh Yahya wa atakayempinga JK kufa haukutimia!
2. Uchaguzi Mkuu, 2010 haukuahirishwa!
3. Mch Gwajima alimpa masharti ambayo Sheikh Yahya aliyapuuza na kweli mauti yalimfika!
4. Katika Biblia tunaona kwamba Mungu anasema kwamba Nabii atakayenena kwa majina ya miungu mingine (kama alivyofanya Sheikh Yahya) atakufa! (Kumb. 18:20).
 
Lililopitishwa na Mungu tuliache lipite. Poleni wafiwa haya yote ni kazi ya Mungu haina makosa.
Nilifikiri wachawi huishi mda mrefu kumbe nao hufa kabla ya kuzeeka sana kweli hapo Mungu ametufumba.
 
Rest In Trouble
Mfuga majini, Kigagu. Mshirikina Sheikh Yahya!
 
Nakushukuru kwa kunikumbuka. Humu Jf nazipata changa moto tu.
Hoja ndio muhimu katika ilmu.
 
Nadhani uwanja wa siasa sasa utabakia kuwa salama! No more threats!
 
Zuga yao ni utabiri, kumbe biashara yao kubwa ni kuuza uchawi/majini

Jamani!
Hizo ni chuki za binafsi.
Toa facts zako...ulienda kwa mtabiri gani akakuzuga na akakuuzia majini?
Majini si Mbuzi kaka/dada!!!
Jitahidi ukutane na watabiri wa kweli upate faida za ilmu hii...!
 
Tupe ushahidi kuwa utabiri si ramli na kuwa imeruhusiwa katika uislam.
Kawaida unapoanza kukosoa ndipo unaweka ushahidi wako.
Wekeni huo ushahidi wenu...ili tuone ufahamu au niwape ushahidi wangu...sio kuleta ubabaishaji.
 
mtabiri wa nyota anafanya kazi hiyo kwa nguvu gani? ilm gani inamsaidia kutabiri?
 
Innalillah wainailaih rajiuun, SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.
 
Siku chache baada ya mtabiri mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein wa Dar es Salaam kutangaza katika vyombo vya habari kuwa mwana CCM atakayejitokeza kuchuana na Rais Jakaya Kikwete katika kinyang'anyiro cha kugombea urais mwaka huu, atakufa ghafla, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Ubungo ametoa masharti matatu kwa mtabiri huyo vinginevyo naye atakufa ghafla.

Katika mahubiri kanisani hapo jana, Mchungaji Kiongozi, Gwajima alisema demokrasia ya Tanzania imo hatarini endapo mtu mmoja ataachiwa kuamua hatma ya taifa kinyume na mapenzi ya Mungu asiyekuwa na upendeleo kwa mtu yeyote.

"Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu. Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake," alisema.

Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.

Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.

Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafa nya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka.

Kwani nae amekufa ghafla!?
 

Mbowe, kitendo cha huyo "Mtakatifu" Yahya kuleta vitisho vya mara kwa mara kwa manufaa ya Wakubwa ndiyo unyenyekevu unaozungumzia?
Anyway, Marehemu hana sifa mbaya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…