JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

Hakuna maoni ya ccm wala chadema katiba ni ya watu wote tatizo ya chadema ni kujiona kuwa katiba ni ya kwao.

Acha ujinga wewe!chadema wanatetea kile wanacho amini na wamefafanua kwa kina tofaut ya serekal 3 wanazotaka na serekal mbili za maccm mbona ccm wasije hadharan wakaeleza faida na hasara za serekal mbili,wao wanabak kusema garama garama,fichen ujinga nyie ccm tanzania ni zaid ya ccm na makada wake,katiba ni ya wa tz achen tujiamulie katiba tuitakayo
 
Tuache utoto wa kuwashabikia akina slaa wenye malengo kama ya kagame kwenye nchi hii watanzani ndiyo wenye maamuzi ya katiba yao wala siyo chadema kama wanavyodhani.

kwan hayo maoni yanayopendekeza serekal 3 tume waliyapata wapi kama sio kwa wana nchi??ficha ujinga wako wewe
 
kwan hayo maoni yanayopendekeza serekal 3 tume waliyapata wapi kama sio kwa wana nchi??ficha ujinga wako wewe
Watu ni akina nani kwani we ni mtu au binadamu,hujapona bado sisitiza tiba mbadala zaidi.
 
Ccm wanaogopa serikali tatu ksababu wanajua kabisa kwny uchaguzi wa 2015 zanzibar watachukua Cuf na tanganyika watachukua Cdm na hawana uhakika wa kushnda ktk kumpata rais wa shirikisho, issue ya gharama haina mashiko hata kidogo,mfumo wa serikali serikali mbili wanafkri utawabeba kwa sababu wanaweza kutia fitina zao kwa zanzibar na kuiba kura kdogo tanganyika na kuilaghai tume na kuwatangaza washindi thus why hawataki hata tume huru ya uchaguzi.
 
Wana JF;
Ili kuondoa manung'uniko na kero za Muungano uliopo kwa nini CCM isikubali Muundo wa serikali tatu? Wazanzibari wanataka Zanzibar huru yenye mamlaka kamili, Tanzania bara wanataka Tanganyika yao maana Zanzibar angalau wana bunge lao japo bado kuna kero kadhaa za Muungano. Kwani kuna siri gani kwa CCM kung'ang'ania serikali mbili huku wanaona hali si shwari malalamiko hayaishi na ni ya muda mrefu? Mi nadhani jibu la kero zote hizi ni serikali tatu.
Wadau mnaonaje katika hili?

kama zenji hawataki serikali mbili basi tuvunje huu muungano kwanza hauna faida yoyote
 
CHAMA CHA Mapinduzi (CCM) kimeshindwa
kushinikiza kuondolewa kwa kipengele
kinachopendekeza uwepo wa mfumo wa serikali tatu katika Katiba Mpya ijayo, MTANZANIA Jumapili limebaini. Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba zinaeleza kuwa, kipengele hicho hakijabadilishwa na badala yake, kimepitishwa kama kilivyo kwenye rasimu ya pili ya Katiba, ambayo tayari
imekamilika.
Kubainika kwa taarifa hizo
kumekuja wakati
Rais Jakaya Kikwete kesho
anatarajiwa
kukabidhiwa rasimu ya pili ya
Katiba Mpya,
hatua inayompa fursa ya kuunda
Bunge la
Katiba. Chanzo cha habari cha
MTANZANIA
Jumapili kimedokeza kuwa
wajumbe wa Tume
ya Katiba Mpya wameshindwa
kukiondoa
kipengele hicho, kwa sababu
kinabeba utashi
wa watu wengi.
Kuainishwa kwa kipengele hicho
katika rasimu
ya kwanza, kulisababisha
msigano mkali baina
ya vyama vya siasa na watu wa
kada na rika
mbalimbali katika jamii.
Pengine hatua hiyo ya sasa,
inaweza kupokewa
kwa furaha na vyama vya
Chadema, CUF na
NCCR-Mageuzi, ambavyo tangu
awali vimekuwa
vikiunga mkono kipengele cha
serikali tatu.
Aidha kupitishwa kwa kipengele
hicho pia
kunaweza kuwa pigo kubwa kwa
CCM, ambayo
imekuwa ikiamini katika uwepo
wa serikali
mbili.
Mbali na kufanya kila juhudi,
ikiwemo kutumia
mabaraza ya Katiba kushinikiza
hoja yake ya
kuhakikisha kipengele cha
serikali tatu
hakipewi nafasi katika rasimu ya
pili ya Katiba,
baadhi ya wanasiasa na wasomi
wanaoheshimika wa aina ya
Cleopa Msuya na
Issa Shivji nao wamewahi
kusikika wakionya
kuhusu kupitishwa kwa kipengele
cha serikali
tatu, kwa maelezo kuwa ni
gharama
kuziendesha, lakini pia
kitahatarisha
Muungano.
Hata hivyo, hatua iliyofikiwa
sasa inakuja
wakati ambapo huko nyuma,
Rais Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa
CCM, aliwahi
kuwatahadharisha wanachama
wenzake
kujiandaa kisaikolojia kwa
mabadiliko yoyote
yatakayotokea kinyume na
matakwa yao.
Rais Kikwete anaaminika kuitoa
kauli hiyo
mwishoni mwa Agosti, mwaka
huu, ndani ya
kikao cha Baraza la Kikatiba la
Halmashauri
Kuu ya CCM, ambalo lilipata
fursa ya kupitia
vifungu vya rasimu ya kwanza ya
Katiba Mpya.
Akitumia hoja ya kutoepuka
mazingira ya sasa
kujenga utetezi wake kuhusu
serikali tatu, Rais
Kikwete anadaiwa kuutumia
mfano wa mwaka
1992, kwamba licha ya idadi
kubwa ya wana-
CCM kukataa mfumo wa vyama
vingi, lakini
mfumo huo ulipita.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete
ilipingwa vikali na
wanachama wenzake wa CCM,
huku baadhi yao
wakiifananisha na ile ya usaliti.
Taarifa zaidi
zilizolifikia MTANZANIA Jumapili
zimedokeza
kuwa katika rasimu hiyo ya pili
ya Katiba
Mpya, Rais wa Jamhuri ya
Muungano
ameongezewa mamlaka zaidi,
ambapo vikosi
vyote vya Ulinzi na Usalama
pamoja na Idara
ya Usalama wa Taifa vitakuwa
chini yake.
Ikumbukwe katika rasimu ya
kwanza kulikuwa
na mkanganyiko wa maelezo ya
baadhi ya
vipengele, kikiwemo kipengele
cha Jeshi la
Polisi kutojumuishwa katika
mambo saba ya
Muungano ambapo ibara ya 232
(1) ilielekeza
kuwa nchi washirika wa Jamhuri
ya Muungano
wa Tanzania wanaweza kuanzisha
vikosi vya
ulinzi vitakavyosimamia masuala
ya usalama
wa watu na mali zao.
Mkanganyiko huo pia
ulikuwapo katika ibara ya 235,
ambayo
inahusiana na Idara ya Usalama
wa Taifa,
kwamba nchi washirika wa
Muungano
wanaweza kuanzisha Idara au
Taasisi
zinazoshughulika na usalama.
Profesa Issa Shivji aliwahi
kuvichambua
vipengele hivyo kwa kusema
vinaweza
kusababisha mgogoro wa
kiusalama ndani ya
Jamhuri ya Muungano. Katika
hatua nyingine,
jana serikali ilitoa tamko la
kuzitaka taasisi na
vikundi vya kijamii kuwasilisha
majina ya
wawakilishi wao kwa ajili ya
uteuzi wa
wajumbe wa Bunge la Katiba kwa
Rais Kikwete
au kwenye ofisi za Katibu Mkuu
Kiongozi, Ikulu
Dar es Salaam au Zanzibar.
Kwamba uteuzi huo unatakiwa
kufanywa
haraka iwezekanavyo na Januari
2 mwakani
itakuwa tamati ya kupeleka
majina hayo.
Uamuzi huo, unatokana na
taarifa ya Rais
Kikwete iliyotolewa na Ofisi ya
Katibu Mkuu
Kiongozi, ikitoa mwaliko kwa
mujibu wa
mamlaka iliyopewa ambapo
mwaliko huo
ulitangazwa katika Gazeti la
Serikali namba 443
la Ijumaa, Desemba 13, 2013.
Waziri wa Katiba na Sheria,
Mathias Chikawe,
alisema kulishatolewa mwongozo
wa namna ya
kupatikana kwa wajumbe hao,
ambao
watawakilisha wananchi wa
Tanzania Bara na
Visiwani. Akifafanua agizo hilo la
serikali,
Chikawe alisema Bunge la Katiba
linatarajiwa
kuwa na wajumbe 201 kutoka
makundi
mbalimbali katika jamii.
"Majina ya makundi
yanayotakiwa kutumwa ni
yale yaliyosajiliwa kisheria,
ambapo wajumbe
20 watatoka katika Taasisi
zisizokuwa za
Kiserikali, Wajumbe 20 kutoka
Taasisi za
Kidini, Wajumbe 42 kutoka
vyama vyote vya
siasa vyenye usajili wa kudumu,
wajumbe 20
kutoka Taasisi za Elimu ya Juu,
Wajumbe 20
kutoka makundi ya watu wenye
Ulemavu.
“Makundi mengine ni wajumbe
19 kutoka
vyama vya wafanyakazi,
wajumbe 10 kutoka
vyama vya wafugaji, wajumbe 10
kutoka
vyama vya wavuvi, wajumbe 20
kutoka vyama
vya wakulima pamoja na
wajumbe 20 kutoka
makundi mengine yote ambayo
yana malengo
yanayofanana,” alisema Chikawe.
Chikawe
aliongeza kuwa idadi ya wajumbe
katika makundi hayo itakuwa sawa kati
ya Zanzibar na Tanzania bara, pia
kutakuwapo na usawa
wa kijinsia.
 
umekopi na kupesti bila hata kuangalia fomati??? ila hongera kwa kutujuza tena juu ya hili
 
Ni kama Kizenji tu, ujumbe ndo umeshafikisha CDMhub, hakuna matata, acha akili za watu zifikirie juu ya hilo
 
katiba siyo ya ccm wala serekali katiba ni ya wananchi na matakwa yao ndicho kinachoitajika
 
Kawaida ya ukweli huwa unatabia ya kujitokeza hata kama utachukua miaka 20 kujulikana lakini bado utajitokeza tu.
Kwa upande wa hili la serikali tatu lilitabiliwa kitambo na ukweli wenyewe ndio huo hata kama utaufunika na kufukia kwa namna yoyote huwa una njia nyingi za kujitokeza.
 
Katiba nyenyewe sio agenda ya CCM, kila kinachoendelea ni kinachowezekana.
 
Shamsi Vuai naye jana amedai mamlaka yake ya Zanzibar., wacha tuone itakuwaje tutazidi kupambana huko kwenye bunge la katiba na hayo mengine ya benki kuu, uraia na fedha yatajulikana inshaalah.,
 
Shamsi Vuai naye jana amedai mamlaka yake ya Zanzibar., wacha tuone itakuwaje tutazidi kupambana huko kwenye bunge la katiba na hayo mengine ya benki kuu, uraia na fedha yatajulikana inshaalah.,

la serikali tatu haliepukiki...
 
Back
Top Bottom