JK na maadili ya viongozi

JK na maadili ya viongozi


By The Citizen Team and Agencies

He called upon the public to be patient as state organs continue with investigations. I believe this work will be completed in a six month period as I ordered, he affirmed.

The president, however, expressed his concern on misleading reports about the scandal, urging wananchi to disregard them as truth will come out from the investigation team.


Mr President there is no one to blame for those rumours but yourself. The reasons for those rumours are as follows:

1. Without any valid reason, you have refused to release BoT report in regards to EPA scandal.

2. Officials from US Govt told you in public that if you need Ballali to be returned to Tanzania they are ready to help, but to the surprise of many Tanzanians so far you have not said anything about that offer.

3. There are so many scandals in your goverment such as mikataba ya madini, Richmonduli, BoT and on top of that some of your ministers including Meghji, Karamagi, Mramba, Msolla, Magufuli etc were involved in one way or another in those scandals or they were unable to perform their duties to the satisfaction of many Tanzanias. Again to the surprise of many of us, those ministers are still in office.

Therefore due to your inability to act according to Tanzanians expectations you allow people to speculate so many things in regards to awamu ya tatu as well as awamu ya nne.

There is a possibility you don't have the ability to lead Tanzanians as well as to deal with so many scandals that occured during Mkapa's era as well as awamu ya nne. If you unable to act Mr president, it is better for you to RESIGN for the benefit of our beloved country.
 
Jamani katika hili JK kasema ukweli. Inawezekana ameliona sasa hivi ingawa lilikuwepo toka mwanzo lakini kila kitu kina mwanzo, na hakuna mwanzo mzuri kama kujua tatizo.

Tokana na hali iliyopo hapa Tanzania kwa sasa, bila shaka kabisa JK ameweza kuona kwamba viongozi wengi wanafanya ufisadi kwa kutumia kofia zao za uongozi na kwa faida ya biashara zao wenyewe nk. Bila shaka alichosema ni kweli na inabidi kifanyike ili kuinusuru Tanzania. Na kwa msingi huo JK inabidi mara moja abadilishe baraza la mawaziri lote na wabunge kwani walio wengi ni wafanya biashara wakubwa.
 
Mtambo:
Usisahau kuwa tatizo hili la 'conflict of interest' limezungumziwa mara nyingi, tokea Mkapa alipodhihirika kuanzisha biashara akiwa Ikulu; na juzi limezungumzia tena humu baada ya Mkono kujipigapiga kifua kama nyani akidai kampuni yake kumtetea Ballali akihitaji huduma hiyo atakaporejea nchini.

Kikwete hakudondoka toka mbinguni jana, kana kwamba hali ya nchi inavyoyumbishwa na hawa wanasiasa wafanyabiashara hakuijua. Amekuwa katika serikali hiyo hiyo tokea angali mtoto, itakuwaje asijue hali halisi.

Hizi zote ni dalili zilizo wazi zinazoonyesha udhaifu wake katika uongozi. Wengi tulikuwa na matumaini makubwa kwake; lakini tumeanza kukata tamaa.
 
Mnasahau kwamba JK kuanzia TANU na kivukoni kote alikuwa ndaniya Chama ? Mnasahau kwamba yeye siasa za kileo hajui ila za uzushi na kutaka kusifiwa ? Kasema mangapi na mangapi yametendwa ? Mimi siamini hadi nione . Na hii ni janja tu ya kuwaokoa wana CCM maana hapatakuwa na verification kwamba theirinfuency as MP and Ministers were not used . Hapa ni pabaya zaidi tunako taka kwenda .JK anataka kukisafisha Chama kijanja .
 
jamani tusiandikie mate na wino upo.
tusubiri tuangalie jee haya yaliosemwa yatatekelezwa au ndio kutufanya ss ni wananchi wa kudanganyika kazi yetu kuamini kila alisemalo mkuu ni sawa


ila tujaribuni kumpa muda then ndio tutajua kama tumpambe kwa maua au kwa tumpambe kwa kumuumbua
 
jamani tusiandikie mate na wino upo.
tusubiri tuangalie jee haya yaliosemwa yatatekelezwa au ndio kutufanya ss ni wananchi wa kudanganyika kazi yetu kuamini kila alisemalo mkuu ni sawa


ila tujaribuni kumpa muda then ndio tutajua kama tumpambe kwa maua au kwa tumpambe kwa kumuumbua

Mtu wa Pwani,
Heshima yako ndugu.

Subira unayoitaka inaweza kuwa sawa kabisa na utabiri wa mambo ya kenya kama mtu angeufanya miezi 12 iliyopita. Kamwe asingejua matabaka yaliyojijenga yanaweza kuwafikisha hapo walipo, kamwe asingelitabiri jirani walioishi miaka nenda rudi wanakatana mapanga.

Miaka miwili katika Urais kwa kiongozi aliyetumikia chama na serikali yake miaka nenda rudi ni mingi mno, isitoshe kipindi chake cha Urais kwa hapa nyumbani ni miaka mitano. Ila inaonekana umenena kuhusu subira ukitegemea na kuwa na mwelekeo kuwa Rais wetu ni lazima atumikie miaka 10. Na hili ndilo lililo kubwa na limejengeka vichwani mwetu tuliowengi. Hapana. Rais anaingia pale akiwa ameshatoa ahadi mbalimbali ambazo ni hima kwake kuzitekeleza zote ndani ya miaka mitano. Jambo kama hilo la kutokomeza rushwa na kuondoa migongano ya kimaslahi, ni jambo ambalo lipo na ninauhakika alikuwa analijua kabla hata ajawa Rais. Watanzania tumechoka na hizi ahadi. Mpaka lini jamani?!!

Kama tu vile Kalamu, Lunyungu na Bubu walivyotangulia na kusema, ni kashfa baada ya kashfa zinazidi kufichuka na nyingine kutokea... kwa mtu ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu kama Mh. Kikwete, ni sharti anajua yote. Inaction yake ni kielelezo tosha kuwa either anahusika kinamna katika hizo scandal au basi kashindwa jinsi ya kutatua kutokana na kutokuwa na washauri wa kutosha au kutokuwa mtu mwenye kuamua kwa moyo wake, au basi kwa nia mbaya iliyojificha ya kuwastahi wenzake anaowajua kuhusika hizo kashfa.

Mtambo, kubadili baraza la mawaziri tu bila kuweka misingi bora au kutekeleza ambayo yapo tayari kama mihimili ya kulinda Taifa letu hakuta leta maana sana, itakuwa mambo ya recycling tu hayo. Ni kiongozi yupi ambaye atakuwa msafi kiasi cha kubalika kulinganisha na waliomo tayari... ni wachache kwa kweli. Kinamna lakini, naweza kukubaliana nawe katika kubadilisha baraza la mawaziri, kama anaamua kuwaondoa wote mara moja wanaoonekana kuhusika na kashfa zilizopo moja kwa moja. Au basi alipunguze baraza la mawaziri, ni kubwa mno na ufanisi wake wala hauonekani ukilinganisha na gharama zitumikazo na hali ya uchumi wa nchi. Lakini kama kwa misingi ya kuondoa migongano ya maslahi ya kibiashara, basi kanuni na maadili ya viongozi yaanze kutekelezeka mara moja na siyo kutoa matamshi au ahadi kuwa tutaanza tutaanza tutaanza na muda ukifika tunaambiwa tena kuna tume itachaguliwa kushughulikia swala hio hilo. Tumechoka na subira.

SteveD.
 
Bongolander;133256[SIZE="3" said:
]..For sure kutokana na Azimio la Zanzibar, naweza kusema sasa hivi ukiangalia uchumi binafsi wa mawaziri wetu unapaa, EL alivyosema uchumi unapaa, kwa maoni yangu alikuwa anazungumzia uchumi wake binafsi, which is very true, wake na wa mawaziri wengine unapaa haswa.

JKN alisema sasa hivi ukizungumzia Azimio la Arusha (miiko ya uongozi) utakuwa kama mwendawazimu.Mimi binafsi sikubaliani na vipengele vingi vya Azimio la Arusha, kwa sababu vingi ni very utopian,.. lakini nakubaliana sana na vya miiko ya uongozi. Lakini navyo leo hii havitekelezeki. [/SIZE]

Heshma, Bongolander:

Tuanze "Azimio la Arusha kuwa ni Utopian". Pls Tuanze kwa kupitia post zangu tulizofanya a very deep disxn kuhusu hilio Thread: Kumbe Nyerere alifanikiwa?
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9324

Tunahitaji muda wa kutosha kuja kugundua kuwa Azimio la arusha sio Utopian. Ni utopian Tu kwa kuwa Muda na expirince ya wananchi hawajapitia kwa vitendo maisha ambayo yangedai azimio la arusha kama jibu.

Miaka 6-7 Baada ya Uhuru. Viongozi wale waliopigania uhuru. Waligeuka Kuwa mafisadi. Kama hawa tuliona o leo Hii hapa tanzania. Ndipo azimio likaja kureguate. leo hii azimio litaanza kuleta maana, kuna situation zilizowahi kuweko zimejirudia.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9324
 
..For sure kutokana na Azimio la Zanzibar, naweza kusema sasa hivi ukiangalia uchumi binafsi wa mawaziri wetu unapaa, EL alivyosema uchumi unapaa, kwa maoni yangu alikuwa anazungumzia uchumi wake binafsi, which is very true, wake na wa mawaziri wengine unapaa haswa.
JKN alisema sasa hivi ukizungumzia Azimio la Arusha (miiko ya uongozi) utakuwa kama mwendawazimu. Mimi binafsi sikubaliani na vipengele vingi vya Azimio la Arusha, kwa sababu vingi ni very utopian, lakini nakubaliana sana na vya miiko ya uongozi. Lakini navyo leo hii havitekelezeki. CCM wamelease chama kwa wafanya biashara, sasa hivi wanataka returns na faida juu, kama ukileta miiko sasa hivi hakuna atakayerudisha investment yake na kupata returns. Ninachokiona sasa hivi ni kuwa tunazungwa tu, na tutaendelea kuzugwa hadi tutakapoamua na kuweza kuchukua hatua, lakini wakati huo watu watakuwa wameneemeka sana, in our expense.

BLandder:

MUDA WA KUFUFUKA KWA AZIOMIO LA ARUSHA KWA VITENDO UMEKARIBIA: Nini kitalazimisha Azimio lifuatwe nafikiri kwa thread hiyo hapo juu umeshaona.
Ona Mwananchi huyu anavyokiri kuwa awali watanzania walikuwa hakuelewa Umuhimu wa Azimio La Arusha. Lakini ni matendo ya Ufisadi amabayo Nyerere alifaikuw akuwa na vision nayo yatakayo Proove kuwa Azimio is still very valid.

Bwana Chris Kalembo alisema...Hayati Baba wa Taifa mwalimu Julias Nyenyere aliwahi kuupitisha “Si jambo la ajabu kwani hata mwaimu Nyenyere aliliona hilo, ndiyo sababu ya Azimio la Arusha. Lakini kwa wakati ule, Wananchi hawakumuelewa, sasa ndiyo umuhimu wake unaonekana” alisema Chris Kalembo, mfanya biashara wa jijini Dar es Salaam.
Makala nzima hii hapa. haitofautina sana na hii ya Citizen tuliyonayo kwnye thread hii:

WENGI WAAFIKI VIONGOZI KUJITENGTA NA BIASHARA
.

“Profesa asema asilimia kubwa ni wafanyabiashara.”
Wananchi wameupongeza msimamo wa Rais Jakaya Kikwete wa kuwataka Mawaziri na wabunge kuchagua moja kati ya siasa na biashara.

Badhi ya wanachi waliozungumza na uhuru jana. Walisema uamuzi huo wa Rais umechelewa kuchukuliwa. Wakizungumza kwa nyakati fofauti, wananchi hao wakazi wa Dar es Salaam walisema, uamuzi huo sijambo la ajabu kwani hata Hayati Baba wa Taifa mwalimu Julias Nyenyere aliwahi kuupitisha “Si jambo la ajabu kwani hata mwaimu Nyenyere aliliona hilo, ndiyo sababu ya Azimio la Arusha. Lakini kwa wakati ule, Wananchi hawakumuelewa, sasa ndiyo umuhimu wake unaonekana” alisema Chris Kalembo, mfanya biashara wa jijini Dar es Salaam.

Kalembo alisema kwa wakati ule mwalimu Nyerere alijua fika kuwa, huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
“alijua mwisho wake utakavyokuwa, alitaka udhibiti na usawa viongozi kwa maslahi ya nchi” alisema. Kalembo alisema kwa Rais Kikwete kuiona hilo na kwa kuwa bado hajachelewa, anaweza kulibadilisha ili kurudisha imani kwa wanachi.aliamua uamuzi huo utaepusha kujengeka kwa matabaka kutokana na uroho wamadaraka, ambapo baadhi ya viongozi wangeweza khilimnikizia mali kutokana na kuwa na umiliki wa viwanda na kuwa mawaziri.

Naye Profesa Khalidi Aman Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alipoongeza uamuzi huo akisema inavyoonekana sasa, kwa asilimia kubwa ya wabunge na mawaziri niwafanyabiashara.

Alisema ili kuwadhibiti wasichanganye siasa na biashara m wataje miradi waliyonayo na jinsi walivyoipata.

Kila kiongozi anapaswa kutaja mtaji wa mradi wake na ameupaata vipi, hii ni katika kuweka maadili ya uongozi sawa na mapato yao pia yawe wazi.
Lakini kama na hili litakuwa ngumu, Rais ana uamuzi kuna wanasiasa wengi wasio wafanyabishara aweteue hao alisema.

Kwa upande wake Mboga Segia, ambaye ni mtumishi wa umma alisema iwapo Rais asingechukua hatua za haraka kwa Baraza lake la Mawaziri na wabunge kujihusisha na biashara baadaye Tanzania ingeweza kujikuta katika machafuko kama ya Kenya.

“kinachoendelea hivi sasa Kenya ni matunda ya udhaifu mdogo uliodharauliwa awali kama Rais asipodhibiti hali hii, kuna hatari ya machafuko kama ya Kenya kujitokeza,” alisema Mboga.
Jongo Rubeni mfanya biashara wa jijini Dar es Salaam akipongeza msisimamo huo wa Rais, alisema ndiyo njia pekee ya kuokoa Taifa kwani wabunge na mawaziri wakiachwa kuendelea na kazi na wakati huo huo kujihusisha na biashara, kuna kila sababu ya kutanguliza maslahi yao binafsi.

Unapompa mtu madaraka wakati ana biashara ni lazima atafanya kile chenye faida kwake. Mfumo huo ukiachwa uendelee Taifa litaangamia, hatutafika mbali tayari madhara yamesha anza kuonekana, alisema. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) Wilfred Lwakatare alisema Rais Kikwete afuatilie na kutikeleza agizo hilo, ili kurijesha imani ya wanchi kwa serikali.

Alisema endapo ametangaza na baadaye akikaa kimya wananchi wataona ni hali ya kawaida.alitahadharisha kuwa mipango bila ya utekelezaji ni kazi bure hivyo ni vyema Rais akasimamia agizo hilo litekelezeke kwa ufsaha.

Akizungumzia tamko hilo, mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema, alilsema si la ajabu kwa kuwa lilianza tangu wakati wa Azimio la Arusha.

Juzi kwenye hotuba yake ya kila mwezi kwa wanachi Rais Kikwete alisema wakati umefika kwa viongozi wa siasa serikalini kuchagua kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama ubunge, uwaziri na kufanya marekebisho ya sheria ya maadili ya viongozi ili kuingiza utaritibu huo.

Raisi Kikwete alisema viongozi kuwa wafnyabiashara inaonyesha wazi mara nyingi kumekuwa na migongano ya kimaslahi pamoja na kutumia nafasi walizonazo kujinufaisha.upo ushaidi wa kuwepo migongano ya kimaslahi kwa baadhi lakini hat pale ambapo hakuna dalili za wazi,hisia za kupata manufaa yanyuotokana na nafasi zao hutawal, alisema Rais Kikwete
.
Alisema viongozi wa namna hiyo wamekuwa ni chanzo cha wananchi kupoteza imani na kutilia shaka uadilifu wao.

Sorce: Gazeti La Uhuru.
Tarehe 2. February 2008
 
Yafuatayo ni matamshi ya REV KISHOKA.

YANASISITIZA KWA UNDANI, UMUHIMU NA NAFASI YA A LA ARUSHA LEO
Azimio la Arusha labidi kuelimishwa na kupitiwa. Kama Mwalimu Nyerere alisema lahitaji mabadiliko kadhaa na kuhamasisha utekelezaji wake.

Watanzania tumepotoka kufikiri kuwa Azimio lilituletea Umasikini. La hasha! Ni sehemu moja ya Azimio ambayo ilitafsiriwa vibaya na kushindwa kufanyika vizuri ni kwenye kupambanua suala la Kujitegemea na haswa kuhusu kutegemea Umilikajji wa Uzalishaji mali kupitia mikono binafsi na hasa ile ya Wageni.

Azimio bado lipo hai, kinadharia na hata kivitendo. Tusipotoshwe na danganya toto ya Zanzibar 1992 ambayo ilifuta miiko ya Uongozi kuhusiana na kujilimbikizia mali!

Kwanini azimio litafufuka kutokana na mahitaji ja jamii kipindi hiki:
Pitia kwa makini thread hii:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9034&page=2





:
 
Kuna hii habri ya jinsi vingozi wetu, mawaziri, mabalozi, wabunge, Spika n.k wanavyoshiriki kwenye biashara

Ni habari ya siku nyingi kidogo but worth reading it to get insight nani anafanya biashara hadi sasa, ana share wapi n.k
 

Attachments

JK azua mjadala

na Peter Nyanje, Dodoma
Tanzania Daima

HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kuwabana zaidi viongozi wa umma kupitia sheria ya maadili, haitokuwa na manufaa makubwa iwapo utekelezaji wake utasuasua.
Aidha, manufaa ya hatua hiyo yataonekana zaidi kutokana na uwajibikaji wa viongozi wenyewe na tafsiri sahihi ya yaliyomo kwenye sheria hiyo.

Maoni hayo yalitolewa kwa nyakati tofauti jana na wanasiasa na wasomi mbalimbali waliozungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam na Dodoma.

Baadhi ya waliozungumzia suala hilo, ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid (CUF) aliyesema kuwa, iwapo utekelezaji wa kauli za Rais Kikwete utafanyika nchi itarajie mabadiliko.

Alisema, mabadiliko anayoyataka Kikwete hayatakuwa na maana iwapo watu watakaowania uongozi hawatafanya hivyo kwa dhamira ya kuwatumikia wananchi.

Hamadi Rashid alisema kuwa pamoja na hayo, ili sheria hiyo iweze kuleta mafanikio yanayotakiwa, ni vema kukawa na tafsiri sahihi ya nini hasa ni biashara.

Akifafanua, alisema kuwa zamani viongozi walikuwa wanakatazwa hata kumiliki kuku na baadaye masharti hayo yalilegezwa na kuruhusiwa kulima, na kutakiwa kuwa mfano kwa wananchi wengine katika kilimo.

"Sasa kama mimi kiongozi nikiwa namiliki ekari 100 za ardhi na ninazitumia kwa kilimo, hii itahesabiwa kama biashara au vipi?" alihoji.

Aidha, alisema kuwa, kwa mujibu wa sheria ya maadili iliyopo, mwenzi wa ndoa wa kiongozi, naye anahesabika kama kiongozi na kutaka kufahamu haki ya wenzi hao itakuwaje wakati wenzi wao, ambao ndio viongozi, watakapotakiwa kuacha kufanya biashara wakati wana haki ya kikatiba kujishughulisha.

Hamad Rashid alisema kuwa, hata sheria iliyopo sasa inaweza kusaidia sana kuleta mabadiliko iwapo itafanyiwa marekebisho madogo na kutumiwa ipasavyo.

"Tatizo letu ni kuwa hata sheria iliyopo hatuitumii ipasavyo… inapasa imlazimishe kiongozi si tu kutaja mali zake, bali kutangaza hadharani na kumpa uhuru mwananchi yeyote kwenda kuhoji mali hizo.

"Pia inatakiwa tuwe na utaratibu utakaotuwezesha kila mwaka viongozi watangaze mali zao na kueleza wamezipata vipi ili wanapomaliza muda wao wa uongozi isiwe shida kuona mtu amepata wapi mali anazozimiliki ambazo hakuwa nazo wakati anaingia katika uongozi," alisema.

Hamad Rashid alisema viongozi wengi wanajiingiza katika biashara kwa sababu hawana uhakika wa maisha yao baada ya kustaafu kwa kuwa hawana mishahara mizuri na mafao bora.

Alisema ili kurekebisha hali hiyo, ni vema sheria itakaporekebishwa kuliangalia suala hilo, ili kiongozi aandaliwe maisha yake baada ya kumaliza utumishi ili kumfanya awe muadilifu anapokuwa madarakani.

"Viongozi wengi tuliokuwa waadilifu, akiwemo Hamad Rashid mwenyewe, tunaishi maisha ya dhiki," alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto (Chadema), alisema hatua ya kuiboresha sheria ya maadili ni nzuri, lakini hofu yake ni kasi ya kufanya hivyo, jambo ambalo linaweza kuchelewesha utekelezaji wa azma hiyo.

Akitoa mfano, alisema kuwa katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge mwaka juzi, Rais Kikwete aliahidi kulifanyia kazi suala la fedha zinazotumika katika kampeni za kisiasa, lakini hadi sasa haieleweki limefikia wapi.

Alisema, wakati muswada wa sheria mpya ya rushwa ulipoletwa bungeni, yeye na mbunge mwenzake wa upinzani walitumia fursa hiyo kuibana serikali kueleza ilipofikia katika suala hilo, hata hivyo, hawakupata ufafanuzi wa kuridhisha.

Zitto alisema kuwa katika majadiliano hayo, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliahidi kuwa suala hilo lingeshughulikiwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

"Kwa kweli masuala haya, ambayo ni muhimu sana yanachukua muda mrefu kushughulikiwa kiasi kwamba yanapoteza maana yake," alisema Zitto na kuongeza kuwa mwaka juzi, alitumwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwenda kwenye Bunge la Canada kujifunza zaidi kuhusu utekelezaji wa sheria ya maadili.

Aliporudi, aliandaa muswada binafsi unaolenga kufanya marekebisho makubwa katika sheria ya maadili na kuuwasilisha bungeni, hata hivyo Katibu wa Bunge alimfahamisha kuwa muswada huo hauwezi kuwasilishwa bungeni kwa sababu utekelezaji wa mabadiliko aliyoyapendekeza yanahitaji mabadiliko ya katiba kwanza.

"Sasa baada ya rais kuonyesha dhamira ya kuibadilisha sheria ya maadili, nitakaa chini na kuangalia la kufanya kuhusu muswada wangu binafsi," alisema.

Kutoka Dar es Salaam, Mwandishi Happiness Katabazi anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alisema anachotakiwa kufanya Kikwete ni kuwafukuza watendaji wasio waadilifu kwanza, wanaotuhumiwa kushiriki kwenye mikataba yenye utata.

"Rais amekuwa na tabia ya kutoa lugha ya kufurahisha Watanzania kwa sababu ni Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiyo ilizika Azimio la Arusha, uamuzi ambao ulilalamikiwa na wananchi wengi kwamba siasa imekuwa biashara na mnada wa kula, lakini walipuuzwa.

"Anachotakiwa kufanya rais ni kuwafukuza watendaji wake wasio waadilifu wanaotoa tenda za ‘kishikaji' kwa wafanyabiashara walanguzi ambao ni wafadhili wakuu wa CCM wakati wa uchaguzi.

"Ni lazima atofautishe walanguzi na wafanyabiashara. Nyerere alipoanzisha Azimio la Arusha hakuwa mwendawazimu, lakini ni hawa hawa CCM walimpuuza na kwenda kulizika huko Zanzibar…hivyo waliruhusu siasa kuwa ya wafanyabiashara," alisema Mbowe.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema kazi ipo kwenye maadili kwa viongozi na watendaji wa serikali ili waweze kuaminika kwa wananchi na kutunga sheria kwa kuwa sheria haitengenezi maadili bali siasa safi.

Kuhusu kauli ya rais ya kuwataka wabunge na mawaziri kushika moja kati ya siasa au biashara, Baregu alisema upo ushahidi wa mgongano wa kimaslahi kwa viongozi kwa baadhi ya mawaziri au wabunge katika suala hilo na si geni kwa sababu limeainishwa kwenye Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Kitendo cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alipokuwa madarakani kujiuzia kampuni ya makaa ya mawe Kiwira na mawaziri ni mgongano wa wazi wa kimaslahi, lakini Watanzania tulihoji na Rais Kikwete akamtetea kwa madai kuwa tumwache apumzike na kwamba siyo vema kumchunguza rais aliyemtangulia…hapa tunategemea nini kama siyo mgongano wa kimaslahi," alisema Profesa Baregu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Agustine Mrema, alimtaka rais awatajie Watanzania majina ya mawaziri wake ambao maslahi yao yamegongana na maslahi ya umma kisha aanzishe mchakato huo.

"Rais aache nadharia hapa…kwanza atutajie hao mawaziri wake ambao maslahi yao yamegongana na ya umma. Hivi ina maana alikuwa hajui athari zake? Na aliyemwambia wafanyabiashara peke yake ndiyo wanahujumu nchi hii ni nani? Kwani hajui kwamba kuna watu wanahujumu nchi hii kwa kutumia kalamu na karatasi tu tena bila ya kuwa wafanyabiashara?" alihoji Mrema.




 
Hivi hili suala limezungumzwa kwenye Kamati ya Kuu ya CCM, sisi Watanzania wengine linatuhusu vipi? Uamuzi wao wa kuwakataza viongozi wao (CCM) utahusiana vipi na viongozi wasio wana CCM au wasio na chama chochote. Je, Mbunge wa Upinzani anayefanya biashara zake anahusika vipi na uamuzi unaotolewa ndani ya CCM? Je yawezekana kwa mtindo huu athari kubwa zaiti zitakuwa kwa watu kama kina Ndesamburo na Cheyo?
 
Asema kukabidhi biashara yako kwa mtu ni kutaka kufilisika

Na John Daniel, Dodoma

KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kutaka wabunge na mawaziri kuchangua moja biashara ama siasa imepokelewa kwa hisia tofauti huku baadhi ya wafanyabiashara wanasiasa akiwemo Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz (CCM) akibainisha kuwa imemweka njiapanda.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana Bw. Aziz alipongeza hotuba hiyo na kusema Rais Kikwete amepania kuwatumikia Watanzania na hataki dosari katika uongozi wake kwani wanasiasa kuwa wafanyabiashara, kunaweza kuleta mgongano ndani ya chama.

Bw. Aziz ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini aliyewahi pia kuwa Mtunza Hazina wa CCM, alisema endapo sheria hiyo itapitishwa itamwathiri moja kwa moja kwani katika nchi inayokua kiuchumi kama Tanzania, ni vigumu kumwachia mtu asimamie biashara zako, vinginevyo kufanya hivyo, ni kutaka kufilisika.

"Kwanza naheshimu sana maamuzi ya Rais, nadhani amejitoa kwa kuwa anataka kuwatumikia Watanzania na hataki dosari, kwa kweli suala la wafanyabiashara kuwa wabunge linaweza kuleta mgongano ndani ya chama hivyo ni hatua nzuri lakini..."

“Mimi binafsi kama mbunge mfanyabiashara inaniathiri moja kwa moja, ametupa changamoto kubwa sana... Kwa mtazamo wangu katika uchumi wa nchi yetu kumwachia mtu asimamie biashara yako bila wewe mwenyewe ni kufilisika moja kwa moja… Kwangu hili ni ngumu sana kwa kweli bado tunatafakari,”alisema, Bw. Rostam Aziz

Alipoulizwa maoni yake kuhusu uamuzi huo wa Rais kama ni ishara ya kurejea kwenye misingi ya Azimio la Arusha ya mwaka 1967 alisema "Unajua Rais Kikwete ni mwanafunzi wa Mwalimu Nyerere, ni mtu anayetaka kutenda haki, si kwamba anataka kurejea kwenye Azimio la Arusha ila anataka uwanja wa haki na usawa kwa Watanzania, huenda ni mwanasiasa wa mrengo wa kushoto," alisema Mbunge huyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Bw. Yussuf Makamba, alisema hana mjadala wowote na alichosema Rais kwa kuwa ni maamuzi sahihi ya chama kupitia kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichomalizika hivi karibuni mjini hapa.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kama huo ni mwanzo wa CCM kurejea kwenye msingi wa Azimio la Arusha alisema "Kwani ni lini tuliacha Azimio la Arusha? Tuliboresha tu kulingana na wakati na tunazidi kuliboresha zaidi.”

Alipoulizwa sababu za kuanzisha Azimio la Zanzibar kama si ishara ya kuzika Azimio la Arusha alisema; “He !heee ! Azimio la Zanzibar lilikuwa moja ya njia ya kuboresha zaidi Azimio la Arusha kulingana na wakati, hata kule Urusi, Uchina na kwingineko wamepitia njia mbalimbali si kwamba bado wako vile vile,”alisisitiza Bw. Makamba.

Alipoulizwa maoni yake kama Mbunge mbali alisema, “ Hata Yesu alisema ukitaka kunifuata kauze mali yako yote, kisha uje unifuate na Mwalimu Nyerere alisema ‘Heshima na tamaa havikai nyumba moja,’ ni safi mtu kama anataka kuwatumikia wananchi aache moja na kama anataka kufanyabiashara aache moja.

“Ukipata kashfa au tatizo lolote kazini ukiwa unafanya biashara watu watasema hata biashara yako imetokana na kashfa hiyo, hata kama uko msafi lakini wao watasema tu ghorofa yako hiyo imejengwa kutokana na hilo, ili kuondoa hilo ni vizuri tuchukue hatua hiyo, hatutaki chama chetu kipakwe matope,”alisema Bw. Makamba.

Alipotakiwa kueleza athari za umauzi huo ndani ya CCM kwa kuzingatia kuwa baadhi ya wafanyabiashara wabunge na mawaziri wanatoa mchango mkubwa kusaidia CCM hususan wakati wa kampeni, Bw. Makamba, alisema “ Hakuna athari zozote kwa chama kuhusu hili, kwanza ni uamuzi wa chama, pili chama chetu kinaendeshwa kwa michango ya wanachama.

“CCM ina wapenzi wengi ambao wengine hata siyo wana chama wetu, wengine hawana hata uongozi wa tawi lakini wanakipenda chama na wanakisaidia, hata hao wakiacha madaraka yao wataendelea kusaidia chama kama wanachama wengine, ni wakati muafaka kuchagua ubunge au uwaziri au biashara,”alisisitiza Bw. Makamba.

Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki Bw. John Cheyo (UDP), alisema “Kwa kweli mimi namwonea huruma sana Mheshimiwa Rais. Chama chake ndio kitaathirika zaidi, ndio kina matajiri wengi wafanyabishara na wako karibu naye,”alisema.

Alipotakiwa kueleza anavyochukulia uamuzi huo kwa maslahi ya Taifa, alisema “Tena mimi nashangaa Rais angeweza kutekeleza hilo hata bila kutunga sheria, angeweza kuwaondoa wale wafanyabiashara aliowateu kuwa mawaziri moja kwa moja, angeweza kufanya tu,”alisema Bw. Cheyo.

Alidai Rais Kikwete kueleza masuala ya sheria kutekeleza suala hilo ni njia ya kutaka kusafisha chama chake na kwamba ikiwa itakuwa sheria, inaweza kuwa mwiba kwa Watanzania wasio waaminifu na kuongeza kuwa kinachotakiwa ni kuwaengua waliopo bila kusubiri kutungwa sheria.

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime Bw. Chacha Wangwe (CHADEMA), alisema “ Nadhani alichotakiwa kufanya Rais ni kushughulikia ufisadi na si wafanyabiashara, kinachotakiwa hapa ni uaminifu na si suala la biashara, zile bilioni 133 zingeweza kujenga shule za sekondari 1,000 na kuwakomboa wananchi.

“Kwanza wafanyabiashara wa Tanzania bado wanahitaji msaada wa mtaji na kuwezeshwa zaidi, kinachotakwia hapa ni uaminifu na si kuzuia mfanyabishara kuwa mbunge au waziri, zile bilioni 133 wangekopeshwa wafanyabishara wangepiga hatua kubwa sana, ”alisema Bw. Wangwe.

Kwa upande wao wananchi wa mjini hapa walionesha hali ya matumaini mapya na kufurahishwa na hotuba ya Rais Kikwete kuhusu uamuzi huo huku wakidai kuwa amechelewa kuwaondoa wafanyabiashara katika baraza lake la mawaziri.
 
Ukiyapitia vema hayo majarida, Indian ocean newsletter, Uhuru, Mwanachi na TZ daima. Unapata picha nzima ya responce ya jamii kuhusiana na forces Mbili!

1."UONGOZI KAMA NGUVU YA MTAJI" WA KIBIASHA NA KIMASLAHI na

2."UONGOZI KAMA NGUVU YA KUONGOZA" WATU ILI KUJITEGEMEA KIUCHUMI NA KIJAMII.

Hizo nguvu mbili haziwezi kuopparate kwa wakati mmoja. Ni kama Giza na Mwanga havichanganyiki. Huwezi kuelekea juu huku ukiwa unaelekea chini:

Mmachinga anatwanga peku peku mchana mzima, amebeba products zake, anapigwa na jua kali na mvua inamnyeshea...mpaka jioni hajauza.

Kwa nini asigombee Ubunge na autwae UWAZIRI MKUU. Ngazi hiyo ya Uongozi itampa nafasi WAZI kabisa ya kuuza PRODUCTS zake. Hatasota juani, mvua ikimnyeshea, kukimbizwa na askari wa jiji, na anaweza hata asilipe kodi.

Mmachinga huyo anaweza kuboresha bishara ya products zake, kama akiboresha kuweka mikataba na wawekezaji kutoka USA. Watampa exposure ya kuuza product zake.

Sasa Kwa nini mmachinga asipigane kufa na kupona KUUKWAA UBUNGE NA UWAZIRI MKUU? Kwa post hiyo hahitaji kufanya advertisment yeyote wala promotion ya aina yeyote.

Maswali ya msingi naomba majibu?

1. Vipi kuhusu wamanchinga ambao hakuupata ubenge na Uwaziri?
2. Vipi kuhusu watu waliompigia kura kumpa UONGOZI WA PM?
 
Wamekosa pa kushikilia,Cha msingi naomba warudi na kutekeleza maadili ya Uongozi yaliyowekwa na mwalimu nyerere.
 
Hivi hili suala limezungumzwa kwenye Kamati ya Kuu ya CCM, sisi Watanzania wengine linatuhusu vipi? Uamuzi wao wa kuwakataza viongozi wao (CCM) utahusiana vipi na viongozi wasio wana CCM au wasio na chama chochote. Je, Mbunge wa Upinzani anayefanya biashara zake anahusika vipi na uamuzi unaotolewa ndani ya CCM? Je yawezekana kwa mtindo huu athari kubwa zaiti zitakuwa kwa watu kama kina Ndesamburo na Cheyo?

Mwanakijiji,

CCM ndio chama tawala na wana Wabunge wengi bungeni. Walichokubaliana huko kwenye CC ndio kitakuwa sheria ya nchi huko mbeleni.

Wasiwasi ni juu ya utekelezaji wa hii sheria. Kuwazuia wabunge wote wasifanye biashara itakuwa kazi kweli kweli na hata ngumu kutekeleza na pia huenda kusilete mafanikio makubwa kwa taifa. Kama ni mawaziri sawa naweza kuelewa.

Hilo la kuweka mali ya mhusika chini ya trustees, kwa UK kama sikosi linatumika kwa PM tu. Wabunge wanaendesha biashara zao na ni directors kwenye boards mbalimbali. Muhimu tu inabidi wa declare hizo interests zao huko na hata pesa wanazolipwa.

Mbunge akipewa uwaziri au kuwa shadow minister hapo kikawaida inatakiwa aachie kuwa director kwenye boarsd mbalimbali.

Muhimu hapo ni kutunga hizo sheria za conflict of interest na ziwe kali na pia ziwe na meno. Kuwazuia wabunge wote kufanya kazi za biashara au kwenye professions zao naona haitakuwa na faida kwa nchi. Ina maana mtu akiwa na muda wa ziada hawezi kwenda kufundisha, hawezi kwenda kulima shamba lake na kuuza mazao, hawezi kufungua ofisi yake ya ushauri nk.
 
Hivi hili suala limezungumzwa kwenye Kamati ya Kuu ya CCM, sisi Watanzania wengine linatuhusu vipi? Uamuzi wao wa kuwakataza viongozi wao (CCM) utahusiana vipi na viongozi wasio wana CCM au wasio na chama chochote. Je, Mbunge wa Upinzani anayefanya biashara zake anahusika vipi na uamuzi unaotolewa ndani ya CCM? Je yawezekana kwa mtindo huu athari kubwa zaiti zitakuwa kwa watu kama kina Ndesamburo na Cheyo?

Mzee MwanaKijiji,

You got it wrong!!!, the reason he said he propose "to start a process of trying to eliminate that conflict of interests of those politician-business-persons through legal framework i.e. eventually enacting a law is for all MPs and probably DCs, RCs etc...

As President, he needed note to come/provide all details, it is up to the Tanzanians to brainstorm, discuss, challenge and decided whom should be included and whom should be excluded...in that law.

So simply if it was was only for CCM, they could finish the issue themselves. In this case, current MPs, from oppositions and rulling part will be affected if after...

Mind you, I'm afraid that the enacting of the law may be till post 2010 election! Taking into consideration that the rules were not in place during 2005 election from which the current MPs and Minister was selected... just thinking aloud with you!!!
 
Mwanakijiji,

CCM ndio chama tawala na wana Wabunge wengi bungeni. Walichokubaliana huko kwenye CC ndio kitakuwa sheria ya nchi huko mbeleni.

Wasiwasi ni juu ya utekelezaji wa hii sheria. Kuwazuia wabunge wote wasifanye biashara itakuwa kazi kweli kweli na hata ngumu kutekeleza na pia huenda kusilete mafanikio makubwa kwa taifa. Kama ni mawaziri sawa naweza kuelewa.

Hilo la kuweka mali ya mhusika chini ya trustees, kwa UK kama sikosi linatumika kwa PM tu. Wabunge wanaendesha biashara zao na ni directors kwenye boards mbalimbali. Muhimu tu inabidi wa declare hizo interests zao huko na hata pesa wanazolipwa.

Mbunge akipewa uwaziri au kuwa shadow minister hapo kikawaida inatakiwa aachie kuwa director kwenye boarsd mbalimbali.

Muhimu hapo ni kutunga hizo sheria za conflict of interest na ziwe kali na pia ziwe na meno. Kuwazuia wabunge wote kufanya kazi za biashara au kwenye professions zao naona haitakuwa na faida kwa nchi. Ina maana mtu akiwa na muda wa ziada hawezi kwenda kufundisha, hawezi kwenda kulima shamba lake na kuuza mazao, hawezi kufungua ofisi yake ya ushauri nk.

Nadhani mimi nimeelewa kwamba Mbunge au Waziri huyo muhusika hatakuwa active participant kwenye biashara, shughuli hiyo yake!!! anaendelea kumiliki... etc... lakini sio CEO, COO... and probably not chairman... (hili la chairman sijui)... lakini asijihusishe na uendeshaji wa biashara in terms of day-2-day operations....

Nadhani RA ameliweka vizuri zaidi kwenye magazeti ya end of the week. Nadhani nimesoma Ndesamburo amesema atawaachia say Ndugu zake wazi-run...

In terms ya kujua wanajihusisha kwa karibu na biashara hiyo ni jambo rahisi kwa wanasiasa... si wanaonekana!!!

I like the statement from Karamagi quote from Nipashe

``Hii hoja nzuri kama katika biashara zako wewe ndiye Mkurugenzi Mtendaji, Ofisa Mtendaji Mkuu, bila wewe kazi haziendi, pia ni kiongozi wa Serikali, ni lazima uchague moja ,`` alisema.
 
JK uamuzi wako umechelewa
Tanzania Daima

NIA ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka viongozi kuchagua ama kuwa wanasiasa au wafanyabiashara, aliyoitangaza katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Januari kwa wananchi ni nzuri, ambayo sisi wa Tanzania Daima Jumapili, tunadhani kwamba alipaswa kuitekeleza mapema kabisa wakati akiingia Ikulu.
Pamoja na uzuri wa nia hiyo, tunasita kuupongeza uamuzi huo wa sasa, wa kuwataka viongozi kuchagua kutumikia kitu kimoja, kati ya siasa na biashara, ili kuondoa shaka iliyojengeka kwa wananchi kwamba viongozi wanaojihusisha na biashara, si waadilifu katika kutekeleza majukumu yao.

Tunasita kuupongeza uamuzi huo kutokana na imani yetu hiyo kwamba umechelewa kuchukuliwa.

Tunaamini kuwa siku zake za mwanzo akiwa Ikulu, alipaswa kuzitumia kufanya kazi hii, kwa sababu wakati wa kampeni asingeweza kuzitekeleza, kutokana na ukweli kwamba kabla hajaingia madarakani, alikuwa amezungukwa na utitiri wa wafanyabiashara waliokuwa wakihaha huku na huko kuhakikisha kuwa anaupata urais.

Aidha, kipindi hicho kilikuwa kizuri kwake kuifanyia kazi nia yake hiyo, kwa sababu tayari alishapata kile alichokuwa akikitafuta, 'urais' wa Tanzania.

Kinyume chake, amechelewa kuitekeleza nia yake hiyo njema, mpaka wakati huu ambapo serikali yake imekosa imani kwa wananchi na umaarufu wake alioingia nao madarakani kupungua kwa kiwango cha kusikitisha.

Hata hivyo, ingawa sisi tunaamini kwamba Rais Kikwete amechelewa kutekeleza jambo hili, tunapenda kumshauri kwamba; wakati mchakato wa kurekebisha sheria na maadili ya viongozi ukiendelea, awaondoe mawaziri wasioaminika mbele ya umma, hasa kama anadhani kutokuaminiwa kwao kunatokana na biashara zao.

Awaondoe pia wateule wake aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali, ukiwamo ubunge, ambao kwa nafasi zao wanaleta mgongano wa kimasilahi na kuhatarisha masilahi ya nchi.

Sambamba na hatua hizo, aitishe uchunguzi wa kina dhidi ya mawaziri walioshika wizara nyeti ambazo zinasimamia moja kwa moja baadhi ya vitengo vyenye biashara zao binafsi, marafiki zao au familia zao.

Hapa azingatie mawaziri ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuzipendelea biashara zao ambazo ziko chini ya wizara wanazozisimamia.

Pia akamilishe mchakato wa kuondoa sheria zote mbaya za zamani zilizopigiwa kelele tangu enzi za Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi. Zifutwe, na nyingine zirekebishwe.

Akubali kuanzishwa kwa mchakato wa kikatiba na kisheria wa kuondoa kinga kwa rais mstaafu, ambayo inawazuia wananchi kumshitaki na kumwajibisha kwa ubadhirifu alioutenda akiwa madarakani. Mchakato huo uondoe hata utata unaowekwa kwenye tafsiri za kinga hizo.

Tunaamini kuwa, iwapo rais ataufanyia kazi ushauri huu, imani ya wananchi kwa serikali yake itarejea kwa kasi na hata umaarufu wake nao utapanda kama ulivyokuwa hapo awali.

Aidha, tetesi na tuhuma ambazo zimekuwa zikisambaa kila siku kuhusu shaka iliyopo dhidi ya usafi wa wasaidizi wake katika nafasi walizonazo, nayo itatoweka kutokana na kuwaondoa wote wanaoshukiwa kujinufaisha wao zaidi kwa kutumia madaraka waliyopewa, badala ya kunufaisha umma.



 
Hata hivyo, ingawa sisi tunaamini kwamba Rais Kikwete amechelewa kutekeleza jambo hili, tunapenda kumshauri kwamba; wakati mchakato wa kurekebisha sheria na maadili ya viongozi ukiendelea, awaondoe mawaziri wasioaminika mbele ya umma, hasa kama anadhani kutokuaminiwa kwao kunatokana na biashara zao.

Awaondoe pia wateule wake aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali, ukiwamo ubunge, ambao kwa nafasi zao wanaleta mgongano wa kimasilahi na kuhatarisha masilahi ya nchi.

Sambamba na hatua hizo, aitishe uchunguzi wa kina dhidi ya mawaziri walioshika wizara nyeti ambazo zinasimamia moja kwa moja baadhi ya vitengo vyenye biashara zao binafsi, marafiki zao au familia zao.

Ni muhimu ieleweke kwamba hapakuwa na sheria kama hiyo! hivyo... angefanya maamuzi kabla ya sheria angekuwa anakinzana na sheria zilizopo sasa... inshort angekuwa Rais mbaguzi...

Kumbuka wakati wa kuunda baraza la mawaziri,,, huenda ya muhimu ni composition ya baraza kikanda,kidini etc... as opposed to Kibiashara... Na ni muhimu ieleweke hapa kwamba biashara in this context means shughuli inayokufanya uwe mtendaji wa karibu wa shamba lako, kiwanda chako, ranchi yako etc.
 
Back
Top Bottom