Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
...hawana idea hao na mawazo yao ya ukomunisti wa 17 century...JKT my azz!
Kama vile Obama alivyokuwa hana idea......eti sasa hivi anasema inflate your tires na ita solve matatizo ya energy.....Mr. Community Organizer has no clue whatsoever!!!
Kuna watu walioenda jeshini na wengine hawakwenda. Kuna stori nyingi za kutoka jeshini. Hivi kulikuwa na sababu gani ya kuwapeleka vijana na kuwalazimisha kujiunga na jeshi na kuwapotezea muda ambao wangeweza kuendelea na masomo ya juu. Naamini kama kuna vitu ambavyo vimepoteza muda sana kwa wananchi ni suala la JKT.
Kulikuwa na mazuri lakini siamini kama Nyerere angefanya hivyo kwani wale vijana wote wangekuwa wanafundishwa mambo ya biashara na sayansi badala ya kusota Mpwapwa, Mafinga, Oljoro, Maramba, Ruvu n.k
Kuna vitu ambavyo namuunga mkono Nyerere lakini hili lilitupotezea muda wa mwaka mzima kusota kwenye mitaro na yare "maafande".
Kenya hawakuwa na JKT na wamekuwa nchi nzuri tu, tena iliyoendelea kiuchumi. Muda mrefu ambao wengi wetu tungekuwa tumeshamaliza elimu ya juu tulitakiwa kwenda kuchimba mitaro, mahandaki, kujenga nyumba, kuchoma matofali na wale waliokuwa ruvu watakumbuka mpunga!
Kama ningetaka kujenga nyumba au kulima mashamba ningefanya ya kwangu mwenyewe. Mbona sasa hivi watu hawalazimishwi kwenda JKT lakini bado wana uzalendo? Nadhani ile ilikuwa ni hofu ya vita baridi zaidi kuliko kitu kingine chochote.
mhhhhh ha ahaha haha haha...hapa najua tutasikia mengi na kudanganywa tutadanganywa najua...haya ongezeni chumvi mtutie wivu!
Kwa mtazamo wangu JKT kweli ni kupoteza muda na wakati kama si kujifunza wizi, uongo, umalaya na kugombana na maafande.
Umoja na mshikamano katika Tanzania tumefundishwa toka tukiwa mashuleni kwa kupitia somo la siasa kwa wale wazee wenzangu na kwa sasa wanaita jina lingine.
Tanzania ilikuwa inahimiza sana umoja na mshikamano (Pitia katiba ya TANU) na kidogo pia katika katiba ya CCM.
Nyimbo nyingi tulizoimbishwa JKT pia tulikuwa tunaimba mashuleni katika Mchakamchaka nk. Pia katika baadhi ya mikoa tulikuwa na chipukizi, game scouts, Tanu youth league nk.
JKT ni kupoteza muda na wala si lolote zaidi.
Ulikuwepo sana hasa kwenye ngono, watu kibao walivunja uchumba na inasemekana kama ingeendelea hali ya VVU ingekuwa mbaya zaidi.
Nurujamii,
Sisi tulikuwa Mafinga kwa Afande (CO) Mlay. Basi tulikuwa tunazalisha sana mahindi, mboga na kujenga nyumba za jenshi na licha ya baridi ya Mafinga- sikumbuki mda I enjoyed my life ktk nikiwepo JKT!
Basi siku moja tulitoka shamba Idetero kule Saw Hill tumechoka- wakawa wamemwandika CO kwenye magazeti- sasa tulipigwa 'Dril' kali wote- basi tukakubaliana watu watatu wajifanye 'wafaint' watatu- ndo yule CO akaotuonea huruma- ndo tukapona!
Sikuwahi kuona mtu strict kama CO Mlay- na hii imenifundisha uvumivilvu sana wa kupambana ktk maisha!
Actually ile miezi 3 ya mwisho tulinenepa sana na hata nilipofika home- watu hawakuamini kama jeshi kuna mateso!
Well JKT was a good opportunity- a must to Tanzanian youth- those who were not given such opportunity=- they must be missing something!
Je mnakumbuka 'green vest ya kijani?' na ukisema huna 'appetite' basi afande anakuambia azima kwa mwezio?? JKT ilikuwa burudani tupu!
Mimi nyimbo za kizalendo kama 15 au zaidi nazozijua leo hii tulijifunza JKT!
Kama vile Obama alivyokuwa hana idea......eti sasa hivi anasema inflate your tires na ita solve matatizo ya energy.....Mr. Community Organizer has no clue whatsoever!!!
Nyie mliopita JKT tuambieni nini mlijifunza huko na mmekitumia kwa manufaa ili kujikwamua na huu umasikini.
Nothing
je Watanzania Wenye Asili Ya Asia Sheria Hii Itawahusu...?