Kuna watu walioenda jeshini na wengine hawakwenda. Kuna stori nyingi za kutoka jeshini. Hivi kulikuwa na sababu gani ya kuwapeleka vijana na kuwalazimisha kujiunga na jeshi na kuwapotezea muda ambao wangeweza kuendelea na masomo ya juu. Naamini kama kuna vitu ambavyo vimepoteza muda sana kwa wananchi ni suala la JKT.
Kulikuwa na mazuri lakini siamini kama Nyerere angefanya hivyo kwani wale vijana wote wangekuwa wanafundishwa mambo ya biashara na sayansi badala ya kusota Mpwapwa, Mafinga, Oljoro, Maramba, Ruvu n.k
Kuna vitu ambavyo namuunga mkono Nyerere lakini hili lilitupotezea muda wa mwaka mzima kusota kwenye mitaro na yare "maafande".