Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 8,024
- 11,546
Du mzee acha kujitoa ufahamu, Mimi nikitoka Zanzibar kuja Dar na mizigo yangu nachajishwa Kodi hata Jagi moja la umeme TRA wanakuzunguka kama umetoka ughaibuni, lakini nikitoka na bidhaa Dsm kuja nayo Mbeya hakuna Kodi ,Basi tufike mahali tukubaliane kutokubaliana,
1. Mimi nasimama na katiba ya JMT inayosisitiza Tanzania ni nchi moja ya JMT ina Amiri Jeshi Mkuu Mmoja wa majeshi ya ulinzi na usalama. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT. JKU na KMKM sii miongoni mwa majeshi hayo, Rais wa Zanzibar sio Amiri Jeshi, ni kamanda tuu JKU, KMKM na vikosi vya SMZ. Ki Tanzania hao ni migambo!.
2. Wewe simama na katiba ya Zanzibar inayojidanya kuwa Tanzania ni nchi ya muungano wa nchi mbili, za Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ni nchi yenye majeshi yake ya JKU, KMKM na vikosi vya SMZ, Rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo, JKU, KMKM na vikosi vya SMZ ni majeshi yenye hadhi sawa na JWTZ, Polisi na Usalama.
Ukweli huwa ni mmoja tuu!, hakuna kweli mbili!. Mimi nasimama na ukweli, Tanzania ni nchi moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu mmoja.
P
Zanzibar ni nchi yenye mamlaka kamili , ndo mana uwezi Kuta Mtz yupo kama kiongozi katika serikali ya Zanzibar ,
Wenzetu wanakitambulisho Cha uzanzibar