JKU na POLISI: Lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?

Kwa itifaki za kijeshi hawatumii neno 'hadhi' maana yote ni majeshi. Tofauti ni kwamba kuna majeshi ya ULINZI na majeshi ya USALAMA. Hapa nchi tuna Jeshi moja la Ulinzi, lakini limegawanyika katika kamandi kadhaa ambazo ni majeshi kamili; kama Anga, Maji, Nchi kavu na JKT. Ndiyo maana unaweza kuona kama JWTZ ni Jeshi moja, lakini Mkuu wake huitwa "Mkuu wa Majeshi. Majeshi ya Usalama ni Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uhifadhi. Kwa kule Zanzibar, jeshi la ulinzi ni hilihili moja; lakini kwa muundo wa Vikosi vya SMZ, wale KMKM kiutendaji ni sawa na Jeshi la Maji (Navy) na hao JKU ni sawa na JKT. Kwa hiyo ni wazi JKU na KMKM ni vikozi vya Ulinzi.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, majukumu ya JKU ni yapi?
 
Unafurahisha Sana kwa majibu haya Mkuu!
NIlikuomba unijibu Kwa Kutumia combat officers Na insignia Utifautishe unakuja kitofautisha na biyu vya ajabu?
Unanijibu kwa ultimate security Really?
Msomi wa sheria?
Mgambo Sio jeshi na wala sio waajiriwa..
Ila JKU ni waajiriwa Unajua tifauti?
Kigezo cha jeshi usu na jeshi kweli sio ajira, jeshi la uhifadhi wameajiriwa na bado ni migambo tuu!. Naendelea kusisitiza, jeshi ni jeshi na mgambo ni mgambo!
P
 
Aint no such thing brother, tofauti imo sana. labda kama hujapita huko.
Eti mgambo better trained kuliko service member wakikusikia watakucheka sana kaka, sijawahi kuona hilo jambo kwa miaka niliyo tumikia taasisi hiyo. First you need to know mgambo wana receive light training version tofauti na full military training
Mkuu Detective J, tofauti pekee ya jeshi na migambo ni usajili tuu, jeshi ni formal, mgambo ni informal, nimekutolea mfano wa mercenaries ni migambo, wako well trained kuliko jeshi la kawaida!, most ni ma commandos!. JKU wana training ya seals sisi navy wetu hatuna!. Meli za utafutaji gesi Lindi zinalindwa na migambo kutoka South Africa, kwasababu jeshi letu tumeshindwa!. Hivyo wako migambo wako well trained kuliko jeshi!, NB, ukisikia migambo, usidhanie ni hawa mgambo wa jiji!.
P
 
Pascal! hatuna Jeshi la Usalama wa Taifa.

Tuna Idara ya Usalama wa Taifa.
Mkuu Lubengera , mimi ni product ya wana Idara hiyo kwa baba na mama, Cheo cha Amiri Jeshi Mkuu, ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Idara ya Usalama wa Taifa, ni jeshi la usalama na wana vyeo vya kijeshi kabisa tofauti ni moja tuu!, hawavai uniforms ili wasitambulike lakini ni wajeshi!.

Ukisikia neno dola ujue ni jeshi, polisi na usalama wa Taifa!. Ukisikia Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ujue usalama ndio hao TISS.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni sio TISS wote ni trained kijeshi, wengine ni informes tuu hivyo wako recruited from ordinary people with no military training. Uwepo wa untrained TISS hakuifanyi TISS kutokuwa jeshi, kuitwa Idara ya Usalama ni jina tuu, hata Idara ya Wanyapori inaitwa Idara na ni jeshi la wanyamapori.
P
 
Mkuu Detective J, tofauti pekee ya jeshi na migambo ni usajili tuu, jeshi ni formal, mgambo ni informal, nimekutolea mfano wa mercenaries ni migambo, wako well trained kuliko jeshi la kawaida!, most ni ma commandos!. JKU wana training ya seals sisi navy wetu hatuna!. Meli za utafutaji gesi Lindi zinalindwa na migambo kutoka South Africa, kwasababu jeshi letu tumeshindwa!. Hivyo wako migambo wako well trained kuliko jeshi!, NB, ukisikia migambo, usidhanie ni hawa mgambo wa jiji!.
P
Mkuu Pascal Tangu mwanzo nakusikiliza na kukusoma Sioni Chochote unachokitoa,Kukiandila wala kuthibitisha kuwa Jeshi la JKU sio Formal..
Zaidi ya maneno yako tu kusema sio Formal..

Formality hailetwi na Maneno yako bali na sheria na katiba..
Ambavyo vyote vimethibitisha na kuiba nguvu ya Dola Idara hizo na Jeshi hilo..

Bhasi tuseme kweli kuwa Formality ya Zanzibar haihusiki Bara..
Na vipi kuhusu Jeshi la Magereza La bara Kutokuwepo Zanzibar?

Na kuwa chinu ya hizi Idara ambazo zimeanzishwa chini ya Katiba ya zanzibar?
Unafahamu kuwa hizo idara zina Nguvu ya Dola?

Kwani jeshi la magereza si lipo chini ya katiba ya Tanzania Ibara ya 147 sasa kwanini Zanzibar Likose nguvu na kutokuwepo.huko?

na Jiulize kwanini Jeshi la magereza lisiwe na Ngivu huko ila Jeshi la Mafunzo lililo chini ya Idaya maalumu kwa Ibara ya 121 (2) Kipengele C Ya katiba ya Zanzibar iliyoanzisha JKU liwe na nguvu?

Pascal Mayalla Unaniangusha ndugu Nsomba Mwichane
 
Mkuu Lubengera , mimi ni product ya wana Idara hiyo kwa baba na mama, Cheo cha Amiri Jeshi Mkuu, ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Idara ya Usalama wa Taifa, ni jeshi la usalama na wana vyeo vya kijeshi kabisa tofauti ni moja tuu!, hawavai uniforms ili wasitambulike lakini ni wajeshi!.

Ukisikia neno dola ujue ni jeshi, polisi na usalama wa Taifa!. Ukisikia Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ujue usalama ndio hao TISS.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni sio TISS wote ni trained kijeshi, wengine ni informes tuu hivyo wako recruited from ordinary people with no military training. Uwepo wa untrained TISS hakuifanyi TISS kutokuwa jeshi, kuitwa Idara ya Usalama ni jina tuu, hata Idara ya Wanyapori inaitwa Idara na ni jeshi la wanyamapori.
P
Hapa umejibu Vyema sana 👏👏👏
Mimi Ni Product ya kijeshi Kiukoo😀😀
Karibia watu wa ukoo wangu wote kuanzia Babu na wengine Kama sio Maafisa wa Jeshi walikuwa/Wapo TISS..

Na huo ni ukweli wote uliosema..
Hao watu wasio na Military Training Wanaitwa Military Provocateur au Agent Provocateur..

wengi wapo Jeshini,Wengine Polisi na wengine hata kama Raia Wa kawaida pia, Na hata Kuna baadhi ya Sehemu wapo kama vyama vya siasa nk..
Sitaki kuelezea kazi zao leo ila Wanafanya kazi vizuri sana na ndo inaliweka Taifa kwenye amani mpaka leo..
Hata ndani na MIU pia wapo...
 
Ngoja kwanza!
Labda mimi ndo Sijaelewa Hebu nipe tofauti ya JWTZ na JKU kwa sheria za kijeshi na hata kimafunzo na Ki-insignia na nipe utofauti wake na Mgambo..
Mkuu andika migambo siyo mgambo 😃😂!.
 
Mkuu Pascal Tangu mwanzo nakusikiliza na kukusoma Sioni Chochote unachokitoa,Kukiandila wala kuthibitisha kuwa Jeshi la JKU sio Formal..
Zaidi ya maneno yako tu kusema sio Formal..

Formality hailetwi na Maneno yako bali na sheria na katiba..
Ambavyo vyote vimethibitisha na kuiba nguvu ya Dola Idara hizo na Jeshi hilo..

Bhasi tuseme kweli kuwa Formality ya Zanzibar haihusiki Bara..
Na vipi kuhusu Jeshi la Magereza La bara Kutokuwepo Zanzibar?

Na kuwa chinu ya hizi Idara ambazo zimeanzishwa chini ya Katiba ya zanzibar?
Unafahamu kuwa hizo idara zina Nguvu ya Dola?

Kwani jeshi la magereza si lipo chini ya katiba ya Tanzania Ibara ya 147 sasa kwanini Zanzibar Likose nguvu na kutokuwepo.huko?

na Jiulize kwanini Jeshi la magereza lisiwe na Ngivu huko ila Jeshi la Mafunzo lililo chini ya Idaya maalumu kwa Ibara ya 121 (2) Kipengele C Ya katiba ya Zanzibar iliyoanzisha JKU liwe na nguvu?

Pascal Mayalla Unaniangusha ndugu Nsomba Mwichane
Maadam Tanzania ni nchi moja ya JMT chini ya Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu, na ulinzi ni issue ya muungano, majeshi rasmi ni yale tuu yanayotambulika rasmi chini ya command ya CinC, majeshi mengine yote chini ya mtu mwingine yeyote, ni majeshi usu, kwa fasiri rasmi ya jeshi. JKU, KMKM na vikosi vya SMZ sio jeshi, ni jeshi usu!, ni auxiliary na para military na militia!, wote hawa ni migambo tuu!.

NB. Tafsiri ya mgambo sio lazima wawe kama mgambo wa jiji!.
P
 
Mkuu Lubengera , mimi ni product ya wana Idara hiyo kwa baba na mama, Cheo cha Amiri Jeshi Mkuu, ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Idara ya Usalama wa Taifa, ni jeshi la usalama na wana vyeo vya kijeshi kabisa tofauti ni moja tuu!, hawavai uniforms ili wasitambulike lakini ni wajeshi!.

Ukisikia neno dola ujue ni jeshi, polisi na usalama wa Taifa!. Ukisikia Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ujue usalama ndio hao TISS.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe ni sio TISS wote ni trained kijeshi, wengine ni informes tuu hivyo wako recruited from ordinary people with no military training. Uwepo wa untrained TISS hakuifanyi TISS kutokuwa jeshi, kuitwa Idara ya Usalama ni jina tuu, hata Idara ya Wanyapori inaitwa Idara na ni jeshi la wanyamapori.
P
Aya yako ya mwisho imetoa tafsiri halisi ya nini maana ya Jeshi.

Ndio mana wenzetu wanatofautisha majeshi kwa kutumia misamiati ya military force na enforcement agencies, na hii yote inachagizwa na wingi wa misamiati (utajiri) wa lugha ya Kiingereza.

Pengine nawe utusaidie, ni sehemu gani Katiba yetu inatambua TISS kama Jeshi?
 
Maadam Tanzania ni nchi moja ya JMT chini ya Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu, na ulinzi ni issue ya muungano, majeshi rasmi ni yale tuu yanayotambulika rasmi chini ya command ya CinC, majeshi mengine yote chini ya mtu mwingine yeyote, ni majeshi usu, kwa fasiri rasmi ya jeshi. JKU, KMKM na vikosi vya SMZ sio jeshi, ni jeshi usu!, ni auxiliary na para military na militia!, wote hawa ni migambo tuu!.

NB. Tafsiri ya mgambo sio lazima wawe kama mgambo wa jiji!.
P
Nimekuelewa ila kumbuka JKU,KMKM inaweza ikawa paramilitary na Auxiliary ila hailiwezi kuwa Militia..
Na ndo nilichokuwa napinga Tangu Mwanzo..

Kuweka JKU,KMKM kuwa Militia ni kulikosea adabu Taifa la zanzibar ila ukisema kuwa ni Paramilitary na auxillay nitakuelewa vizuri..

Militia ni hilo jeshi la Akiba liliopo Bara...
Na ukizungumzia CinC unajua pia Rais wa zanzibar kwa mujibu wa akatiba yao ni CinC wa hayo majeshi..

Na nimekuuliza swali unalikwepa..
Vipi kuhusu Magereza maana lipo Chini ya CinC wa Muungano/Nchi na Halipo Zanzibar na lenyewe ni Militia?
 
Migambo ni wingi mgambo ni umoja. Jeshi likiwa moja kama la mgambo linaitwa mgambo, majeshi yakiwa mengi kama JkU na KMKM wanakuwa migambo!.
P
Narudia tena JKU na KMKm sio Migambo wala Mgambo Ni Paramilitary na auxilliary ambao ni dola kwa mujibu wa katiba ya zanzibar na wala Sio militia..
 
Aya yako ya mwisho imetoa tafsiri halisi ya nini maana ya Jeshi.

Ndio mana wenzetu wanatofautisha majeshi kwa kutumia misamiati ya military force na enforcement agencies, na hii yote inachagizwa na wingi wa misamiati (utajiri) wa lugha ya Kiingereza.

Pengine nawe utusaidie, ni sehemu gani Katiba yetu inatambua TISS kama Jeshi?
TISS sio Jeshi ni Intelligent Agency ni kama Zanzibar mwaka 2013 chini ya Rais Shein alianzisha Enforcements Agency chini ya JKU..
So kuita Polisi Jeshi ni uongo..Hii ni department kama ilivyokuwa Zamani tu!
Kuweka Intimidation ya language ili kuogopwa kwa sababu wanajua Watu wengi wa Africa.wanaogopa neno Jeshi
 
Narudia tena JKU na KMKm sio Migambo wala Mgambo Ni Paramilitary na auxilliary ambao ni dola kwa mujibu wa katiba ya zanzibar na wala Sio militia..
Basi tufike mahali tukubaliane kutokubaliana,
1. Mimi nasimama na katiba ya JMT inayosisitiza Tanzania ni nchi moja ya JMT ina Amiri Jeshi Mkuu Mmoja wa majeshi ya ulinzi na usalama. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT. JKU na KMKM sii miongoni mwa majeshi hayo, Rais wa Zanzibar sio Amiri Jeshi, ni kamanda tuu JKU, KMKM na vikosi vya SMZ. Ki Tanzania hao ni migambo!.
2. Wewe simama na katiba ya Zanzibar inayojidanya kuwa Tanzania ni nchi ya muungano wa nchi mbili, za Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ni nchi yenye majeshi yake ya JKU, KMKM na vikosi vya SMZ, Rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo, JKU, KMKM na vikosi vya SMZ ni majeshi yenye hadhi sawa na JWTZ, Polisi na Usalama.

Ukweli huwa ni mmoja tuu!, hakuna kweli mbili!. Mimi nasimama na ukweli, Tanzania ni nchi moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu mmoja.

P
 
Back
Top Bottom