Habari Pascali!..
Nimesikitishwa sana na Jibu lako Maana nilitegemea makubwa sana ungejibu kutokana na Swali langu Ukizingatia Wewe ni mmoja wa watu naowaheshimu kwa Hoja nzitonzito za Kisheria na Kiuandishi..
Anywei Ngoja niende kwenye Point..
Nimekuuliza Tofauti ya JKU na JWTZ ila ulichonijibu ni Tifauti ya JWTZ na mgambo... what a shame!..
Nimekuuliza unipe tofaiti yake kimuundo (Insignia), kimafunzo(Training combat) ila umeshindwa kufanya hivyo na ukajitengenezea Swali...
Hata hivyo bado swali ulilojitengenezea na lenyewe umelikosa na kwenda chaka..
Mgambo (Kwa sasa Jeshi la Akibaa)..
Linafahamika kama Kamandi ya Jeshi la Akiba chini ya JWTZ..
View attachment 2892829
Bhasi ngoja niendelee kukufundisha kitu...
Mgambo ni jeshi la Akiba japo si chombo cha dola. Haliundwi na rais kama yalivyo majeshi mengine isipokuwa linaundwa na sheria ndogo ndogo ambazo zinazipa mamlaka halmashauri za miji au wilaya kujiundia vyombo vyao vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusimamia shughuli ambazo zipo chini ya mamlaka yao. Hata hivyo, mamlaka hayo kamwe hayawezi kuzidi au kukiuka yale ya vyombo vya dola ambavyo vinasimamia na kudhibiti masuala ya kitaifa, ikiwamo haki za kikatiba za wananchi....
Nachofahamu mimi, jeshi la mgambo (kwa sasa Jeshi la Akiba) linaongozwa na kuuanzishwa kwa sheria inayoitwa
THE PEOPLE'S MILITIA ACT NO.9 ya mwaka 1989,
kama ilivyofanyiwa marekebisho toka awamu hadi awamu ,pia wanaongozwa na sheria inayoitwa
THE PEOPLE'S MILITIA(POWER OF ARREST) ACT,1975 na mwisho
THE PEOPLE'S MILITIA(Compensation for injuries)ACT ya mwaka 1973.
Sheria hizi ni za zamani sana na zinakuwa complemented na sheria nyingine kama vile za halmashauri na ile inayompa mamlaka mkuu wa wilaya.Na People's millitia imekuwa defined kama;
Peoples Militia'' means an organized group of the people of the United Republic operating with the authority of and under the aegis of the Government and which is receiving any military
training or participating in any military, quasi-military or law enforcement exercise for the protection of the sovereignity of the United Republic or for the protection of the people or the property of the United Republic, but does not include the Police Force, any arm or branch of the Defence Forces, the Prisons Service or
the National Service.
Hakuna katiba Inayowatambua migambo Na kama wangetambulika kikatiba bhasi wangekuwa jeshi kamili..
Tafisiri ya Mgambo Wikipedia...
View attachment 2892834
Wakati huo huo Jeshi la Kujenga Uchumi liko asigned pale na Rais wa Zanzibar kwa katiba Yenye mamlaka na Ndo hapo unakuja utofauti wao..Kuna moja Lina nguvu ya Kidola na jeshi jingine halina Nguvu ya kidola..
Kuna moja lina Mipaka ya Kiterritory ndani ya nchi na kuna moja halina mipaka ndani ya nchi..
Umeniangusha Sana,Kwa mwanasheria kama wewe kujibu hivyo..Je na sisi tuso wanasheria Tujibuje?
JKU IPO.CHINI YA katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar ibara kuanzia ya 121 mpaka 124..
Kaisome vizuri..
Kama unaita ni mgambo..
Basi mgambo ndo wanaongoza magereza yetu huko zanzibar maana hata askari wa magereza yaani Jeshi la mafunzo huko.zanzibar lipo chini ya katiba na kifungo hicho hocho kilichounda JKU..
Nakukaribisha mkuu...
KWa mjadala zaidi..
Kama unataka jikite kwenyr insignia,Sheria na katiba..
Pia nakuomba Usome sheria ya majeshi na ulinzi wa Umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.49 na Sheria ya 1992 Na.4 ib.36