JKU na POLISI: Lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?

JKU na POLISI: Lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?

Tofauti ya jeshi na mgambo ni the official status, jeshi ni formal mgambo ni informal.
Kuna migambo wako vizuri kuliko majeshi yetu. Kulipozuka moto jengo la Nasaco, fire za jeshi letu la zimamoto zilishindwa kuzima, hawana vifaa vya kuzima moto ghorofani, fire za kikosi cha Bandari na ultimate security zikaokoa jahazi!.

Mradi wa Gesi wa BG group kule Lindi, tenda ya ulinzi imetotelewa kwa kampuni ya ulinzi kutoka SA, polisi wetu wameshindwa.

Tenda ya ulinzi wa meli indian Ocean dhidi ya maharamia wa Kisomali imeshikwa na wazungu kwasababu jeshi letu la navy halina uwezo!.
Hivyo kuna migambo ni wazuri kuliko wenyewe halisi!.
P
Habari Pascali!..
Nimesikitishwa sana na Jibu lako Maana nilitegemea makubwa sana ungejibu kutokana na Swali langu Ukizingatia Wewe ni mmoja wa watu naowaheshimu kwa Hoja nzitonzito za Kisheria na Kiuandishi..

Anywei Ngoja niende kwenye Point..
Nimekuuliza Tofauti ya JKU na JWTZ ila ulichonijibu ni Tifauti ya JWTZ na mgambo... what a shame!..
Nimekuuliza unipe tofaiti yake kimuundo (Insignia), kimafunzo(Training combat) ila umeshindwa kufanya hivyo na ukajitengenezea Swali...

Hata hivyo bado swali ulilojitengenezea na lenyewe umelikosa na kwenda chaka..
Mgambo (Kwa sasa Jeshi la Akibaa)..
Linafahamika kama Kamandi ya Jeshi la Akiba chini ya JWTZ..
56140433_666433220442484_1653338619689041920_n.jpg

Bhasi ngoja niendelee kukufundisha kitu...

Mgambo ni jeshi la Akiba japo si chombo cha dola. Haliundwi na rais kama yalivyo majeshi mengine isipokuwa linaundwa na sheria ndogo ndogo ambazo zinazipa mamlaka halmashauri za miji au wilaya kujiundia vyombo vyao vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusimamia shughuli ambazo zipo chini ya mamlaka yao. Hata hivyo, mamlaka hayo kamwe hayawezi kuzidi au kukiuka yale ya vyombo vya dola ambavyo vinasimamia na kudhibiti masuala ya kitaifa, ikiwamo haki za kikatiba za wananchi....

Nachofahamu mimi, jeshi la mgambo (kwa sasa Jeshi la Akiba) linaongozwa na kuuanzishwa kwa sheria inayoitwa THE PEOPLE'S MILITIA ACT NO.9 ya mwaka 1989,

kama ilivyofanyiwa marekebisho toka awamu hadi awamu ,pia wanaongozwa na sheria inayoitwa THE PEOPLE'S MILITIA(POWER OF ARREST) ACT,1975 na mwisho THE PEOPLE'S MILITIA(Compensation for injuries)ACT ya mwaka 1973.

Sheria hizi ni za zamani sana na zinakuwa complemented na sheria nyingine kama vile za halmashauri na ile inayompa mamlaka mkuu wa wilaya.Na People's millitia imekuwa defined kama;

Peoples Militia'' means an organized group of the people of the United Republic operating with the authority of and under the aegis of the Government and which is receiving any military
training or participating in any military, quasi-military or law enforcement exercise for the protection of the sovereignity of the United Republic or for the protection of the people or the property of the United Republic, but does not include the Police Force, any arm or branch of the Defence Forces, the Prisons Service or
the National Service.

Hakuna katiba Inayowatambua migambo Na kama wangetambulika kikatiba bhasi wangekuwa jeshi kamili..

Tafisiri ya Mgambo Wikipedia...
Screenshot_20240203_115716_Chrome.jpg

Wakati huo huo Jeshi la Kujenga Uchumi liko asigned pale na Rais wa Zanzibar kwa katiba Yenye mamlaka na Ndo hapo unakuja utofauti wao..Kuna moja Lina nguvu ya Kidola na jeshi jingine halina Nguvu ya kidola..
Kuna moja lina Mipaka ya Kiterritory ndani ya nchi na kuna moja halina mipaka ndani ya nchi..

Umeniangusha Sana,Kwa mwanasheria kama wewe kujibu hivyo..Je na sisi tuso wanasheria Tujibuje?
JKU IPO.CHINI YA katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar ibara kuanzia ya 121 mpaka 124..
Kaisome vizuri..
Kama unaita ni mgambo..
Basi mgambo ndo wanaongoza magereza yetu huko zanzibar maana hata askari wa magereza yaani Jeshi la mafunzo huko.zanzibar lipo chini ya katiba na kifungo hicho hocho kilichounda JKU..

Nakukaribisha mkuu...
KWa mjadala zaidi..
Kama unataka jikite kwenyr insignia,Sheria na katiba..

Pia nakuomba Usome sheria ya majeshi na ulinzi wa Umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.49 na Sheria ya 1992 Na.4 ib.36
 
Mkuu kama katiba ya JMT haivitambui bc hivyo ni vikundi vya migambo tu
Vipi zanzbar kuna Jeshi la magereza?
Je na wenyewe ni mgambo kwa sababu hawapo Zanzibar?

Kujiona wewe ni Bora kwa sababu uko upande wa pili wa Muungano Je ni sawa?
 
Civic education kuhusu majeshi yetu, polisi na migambo inahitajika!. Tanzania tuna Majeshi ya Ulinzi, JWTZ, chini ya CDF, chini ya JWTZ kuna Jeshi la Kujenga Taifa, JKT.

Tuna Jeshi la Polisi PT Tanzania, chini ya IGP, chini yake kuna Jeshi la Zimamoto na ukosoaji, chini ya Commissioner, kunaJeshi la Uhamiaji, chini ya Commissioner, kuna Jeshi la Magereza chini ya Commissioner na Tume ya madawa ya kulevya chini ya Commissioner.

Tuna jeshi la Usalama chini ya DGIS, wale 'jamaa zetu'.

Majeshi mengine yote ni majeshi usu or polisi usu, yaani auxiliary army or police, hawa wote ni migambo, wakiwemo askari wanyapori, KMKM, JKU, Vikosi vya SMZ, ziko taasisi kibao zina majeshi yake wakiwemo Ultimate, Group 4 security, walinzi wa mgodi, walinzi wa meli baharini, etc. Wote hawa ni migambo!. Ni lini Vyeo vya Kijeshi (Collar Insignia) vimebadilishwa hapa nchini?

P

No offence kaka mayalla, with all due respect nadhani hufahamu yapi ni majeshi yapi si majeshi.

Nchi ina jeshi moja tu, ambalo ni jeshi la wananchi.
Taasis zingine polisi, uhamiaji, magereza, si jeshi bali majeshi usu. kitaalam paramilitary organizations

Hakuna kitu kinaitwa jeshi la usalama wa taifa. Usalama wa taifa ni intelligence service na si military or paramilitary component
 
Tofauti ya jeshi na mgambo ni the official status, jeshi ni formal mgambo ni informal.
Kuna migambo wako vizuri kuliko majeshi yetu. Kulipozuka moto jengo la Nasaco, fire za jeshi letu la zimamoto zilishindwa kuzima, hawana vifaa vya kuzima moto ghorofani, fire za kikosi cha Bandari na ultimate security zikaokoa jahazi!.

Mradi wa Gesi wa BG group kule Lindi, tenda ya ulinzi imetotelewa kwa kampuni ya ulinzi kutoka SA, polisi wetu wameshindwa.

Tenda ya ulinzi wa meli indian Ocean dhidi ya maharamia wa Kisomali imeshikwa na wazungu kwasababu jeshi letu la navy halina uwezo!.
Hivyo kuna migambo ni wazuri kuliko wenyewe halisi!.
P

Tofauti ni kubwa sana, even kimafunzo mgambo wana light training, tofauti na full military members. na kuna vitu zaidi wanatofautiana
 
This is it. Actions speak louder than words. Endeleeni kuyaita majeshi ya migambo kujifurahisha.

Ni dhahir kabisa kuwa Zanzibar hawautambui wala kuutilia maanani muungano. Wamejiundia katiba na taasisi zinazowapa full autonomy nje ya Tanzania.

KMKM, JKU ni majina tu. Hayo ni majeshi kamili yenye hadhi nzito kule chini ya amiri jeshi mkuu wao.
Ukweli utabakia tu kwamba hii haitawasaidia. Kmkm na jku ni ceremonial kwenye muungano. Hawana hadhi ya kuilonda Zanzibar wala raisi wa Zanzibar. Ukitaka kujua hilo, je mpambe wa raisi wa Zanzibar ni mwana JKU au KMKM?
 
No offence kaka mayalla, with all due respect nadhani hufahamu yapi ni majeshi yapi si majeshi.

Nchi ina jeshi moja tu, ambalo ni jeshi la wananchi.
Taasis zingine polisi, uhamiaji, magereza, si jeshi bali majeshi usu. kitaalam paramilitary organizations

Hakuna kitu kinaitwa jeshi la usalama wa taifa. Usalama wa taifa ni intelligence service na si military or paramilitary component
Na ndo maana Zamani polisi ilikuwa Idara Chini ya Wizara ya mambo ya ndani ila kwa utashi wa Watawala ikabadilishwa na kuwa Jeshi..
 
Ukweli utabakia tu kwamba hii haitawasaidia. Kmkm na jku ni ceremonial kwenye muungano. Hawana hadhi ya kuilonda Zanzibar wala raisi wa Zanzibar. Ukitaka kujua hilo, je mpambe wa raisi wa Zanzibar ni mwana JKU au KMKM?
Unajua kazi za JKU?
Moja ya kazi hizo ni ulinzi Wa wananchi,, Je hiyo sio kazi ya Jwtz..
Unamjua Kiongozi wa JKU...Si ni.trained Officer from JWTZ?
Then unaitofaitishaje JWTZ na JKU?
Wakati baadhi ya Viongozi wake wametoka JWTZ na pengime kuna Viongozi wa JKU wapo JWTZ..
 
Zanzibar ni kama mkoa tu, niliona Dr mwinyi akiapishwa na magufuli kuwa mjumbe wa Baraza la mawaziri na akaahidi kutunza Siri. Niliona magufuli akimtemea Cheche Dr sheni Kwa kuwa mpole sana, akamwambia ashughulikie maendeleo. Suala la ulinzi na usalama amwachie.

Mtaamuni siku rais wa Zanzibar akitoka chama tofauti na kinachotawala bara, migambo wote wa jku na kmkm watapokonywa SMG na jukumu la ulinzi watapewa jwtz na polisi.

Makamanda wote watakuwa wakurua, wasukuma na wahehe. Wajeshi wenye asili ya zenj watapelekwa bara.

Kutakuwa na matumizi ya nguvu na ukatili mkubwa.

Ili kuepusha haya, ZEC itapewa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar kutoka chamwino.

Katiba ya zenj ni kama by law za halmshauri tu.
 
Na ndo maana Zamani polisi ilikuwa Idara Chini ya Wizara ya mambo ya ndani ila kwa utashi wa Watawala ikabadilishwa na kuwa Jeshi..

Jeshi ni lugha tu but si jeshi kitaalam. Wangekuwa jeshi kamili wasingekuwepo chini ya wizara ya mambo ya ndani, hata kisheria hawana power kama waliyonayo jeshi la wananchi ambalo ndio main military.
 
Hv kwenye sherehe ya Muungano hivyo vikosi vya JKU na KMKM huwa vinashiriki kwenye gwaride kama majeshi????
Amini amini nakwambia, ni rahisi kuwakuta vijana wa Scout wakiwa karibu na uwanja wa Gwaride kwenye maadhimisho ya Kitaifa kama Muungano na Uhuru kuliko hao migambo wa visiwani
 
Zanzibar ni kama mkoa tu, niliona Dr mwinyi akiapishwa na magufuli kuwa mjumbe wa Baraza la mawaziri na akaahidi kutunza Siri. Niliona magufuli akimtemea Cheche Dr sheni Kwa kuwa mpole sana, akamwambia ashughulikie maendeleo. Suala la ulinzi na usalama amwachie.

Mtaamuni siku rais wa Zanzibar akitoka chama tofauti na kinachotawala bara, migambo wote wa jku na kmkm watapokonywa SMG na jukumu la ulinzi watapewa jwtz na polisi.

Makamanda wote watakuwa wakurua, wasukuma na wahehe. Wajeshi wenye asili ya zenj watapelekwa bara.

Kutakuwa na matumizi ya nguvu na ukatili mkubwa.

Ili kuepusha haya, ZEC itapewa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar kutoka chamwino.

Katiba ya zenj ni kama by law za halmshauri tu.
NI Mtu asiye na Elimu tu ndo anaweza kuamini ulichosema..
Screenshot_20240203_132730_Adobe Acrobat.jpg

Screenshot_20240203_133301_Adobe Acrobat.jpg

Rais wa zanzibar haamrishwi Na Rais yoyote soma ibara ya 52 ya Katiba ya zanzibar
 
Jeshi ni lugha tu but si jeshi kitaalam. Wangekuwa jeshi kamili wasingekuwepo chini ya wizara ya mambo ya ndani, hata kisheria hawana power kama waliyonayo jeshi la wananchi ambalo ndio main military.
Safi 💯
 
Back
Top Bottom