Uchaguzi 2020 Joachim Marunda Kimaryo (maarufu kama Master J) atangaza nia ya kugombea ubunge Rombo

Uchaguzi 2020 Joachim Marunda Kimaryo (maarufu kama Master J) atangaza nia ya kugombea ubunge Rombo

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
AMASTER-JAY-333555-585x400.jpg

Muandaji muziki maarufu Joachim Marunda Kimaryo (Master J) ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Rombo akiwa kwenye mahojiano katika redio ya Clouds FM kwenye kipindi cha XXL.

Master J amenukuliwa akisema "Mimi nipo CCM tangu zamani, natangaza nia, uchaguzi wa mwaka huu, Chama kikinipa nafasi nitagombea Rombo, Kilimanjaro kule ndio kwetu, Mbunge wa sasa kule ni Mzee wetu Selasini, naenda Rombo ili kuwatumikia Wananchi”

Master J ambaye amezaliwa (9 Agosti 1973) na amewahi kupata mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) ambao amedumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa, amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2006.

===
Master J, ni mtoto wa kwanza katika familia ya marehemu Sylvan Kimaryo na mama yake, Scholastica Kimaryo, ambaye alikua ni afisa wa UNDP nchini South Africa ambapo dada yake Catherine Kimaryo anaishi nchini Tanzania akiwa mfanyabiashara mwenye kampuni yake Nchanasaa Consulting Limited (NCL).

Master J alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Upanga lakini aliishia darasa la PILI na kuhamishiwa Botswana baada ya familia yake kuhamishiwa nchini huko kikazi.

Mwaka 1996 alipata digrii ya electronics katika chuo cha City University Of London kilichopo bara Ulaya mbali na shughuli za kimuziki.
 
Ni haki yake.

Akipitishwa na chama chake sijui atanyoa hizo nywele au ataenda nazo mjengoni? binafsi ningependa aende nazo.

Anaweza kuwa na "madini" sana kichwani, kuwa msanii hakuna maana uwezo wa kufikiria nao unakuwa mdogo.

Hayo mawazo mgando tuyaache.
 
Ni haki yake.

Akipitishwa na chama chake sijui atanyoa hizo nywele au ataenda nazo mjengoni? binafsi ningependa aende nazo.

Anaweza kuwa na "madini" sana kichwani, kuwa msanii hakuna maana uwezo wa kufikiria nao unakuwa mdogo.

Hayo mawazo mgando tuyaache.
Alishanyoa siku nyingi sana.!
 
Back
Top Bottom