Muandaji muziki maarufu Joachim Marunda Kimaryo (Master J) ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Rombo akiwa kwenye mahojiano katika redio ya Clouds FM kwenye kipindi cha XXL.
Master J amenukuliwa akisema "Mimi nipo CCM tangu zamani, natangaza nia, uchaguzi wa mwaka huu, Chama kikinipa nafasi nitagombea Rombo, Kilimanjaro kule ndio kwetu, Mbunge wa sasa kule ni Mzee wetu Selasini, naenda Rombo ili kuwatumikia Wananchi”
Master J ambaye amezaliwa (9 Agosti 1973) na amewahi kupata mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) ambao amedumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa, amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2006.