Uchaguzi 2020 Joachim Marunda Kimaryo (maarufu kama Master J) atangaza nia ya kugombea ubunge Rombo

Uchaguzi 2020 Joachim Marunda Kimaryo (maarufu kama Master J) atangaza nia ya kugombea ubunge Rombo

Khee! Kumbe jamaa nae ni mchagga Yesuu! Basi Wachagga noma, kila tasinia wamo.
 
Acheni utani wazee!

Master J
Mwana FA
Harmonize
Steve Nyerere
nk

Kama kuna washauri wao humu ndani wasaidieni hawa jamaa, waambieni siasa kama haipo damuni watapata shida bila sababu ni vema wakaendelea na maisha yao ya muziki!
Prof Liquid.
 
Ni haki yake.

Akipitishwa na chama chake sijui atanyoa hizo nywele au ataenda nazo mjengoni? binafsi ningependa aende nazo.

Anaweza kuwa na "madini" sana kichwani, kuwa msanii hakuna maana uwezo wa kufikiria nao unakuwa mdogo.

Hayo mawazo mgando tuyaache.
Alishazinyoa
 
Huyu master j mjinga sana yeye anadhani ubunge ni bongo star search.

Ila baadhi ya watz ni washenzi. Kwani yeyw sio mtanzania? Mnaanza kumwongelea ya marehemu Baba yake mara mke wake nk. Hv mna kitu gani nyie masknin wakubwa?
 
Muandaji muziki maarufu Joachim Marunda Kimaryo (Master J) ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Rombo akiwa kwenye mahojiano katika redio ya Clouds FM kwenye kipindi cha XXL.

Master J amenukuliwa akisema "Mimi nipo CCM tangu zamani, natangaza nia, uchaguzi wa mwaka huu, Chama kikinipa nafasi nitagombea Rombo, Kilimanjaro kule ndio kwetu, Mbunge wa sasa kule ni Mzee wetu Selasini, naenda Rombo ili kuwatumikia Wananchi”

Master J ambaye amezaliwa (9 Agosti 1973) na amewahi kupata mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) ambao amedumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa, amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2006.
KILA MROMBO MWENYE AKILI TIMAMU ANAWEZA KUTIA NIA, NAMWOMBA MASTER J ATUELEZE NI KIPI AMBACHO AMESHATUFANYIA WANAROMBO KAMA MUANDAAJI MKUBWA WA MUZIKI TANZANIA? kama ameshindwa kuisaidia rombo akiwa kwenye bongoflavour, hata awe raisi sembuse ubunge tusitarajie lolote kutoka kwake
 
Back
Top Bottom