Job Ndugai: Anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye

Job Ndugai: Anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Spika Mstaafu wa Bunge, Job Ndugai amewataka Watanzania kuacha tabia kutothamini mafanikio au juhudi za watu mbalimbali wanazozionesha katika taifa hasa katika sekta ya biashara, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mgahawa wa Chakula katika Taarafa ya Pandambili Iliyopo njia Kuu ya Kutoka Dodoma Owenya Morogoro.

Amesema "Kijana anza kufanya biashara halali, kazi ni kazi, achaneni na yule anayesema watu wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye, yule anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa, sasa ule si wenzawazimu tu."

Chanzo: GlobalTV
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Job Ndugai amewataka Watanzania kuacha tabia kutothamini mafanikio au juhudi za watu

Hakuna mahali alisema vijana wa bodaboda wamelaaniwa bali alisema kazi ya bodaboda ni laana,mana haina matumaini na nikazi inayoumiza vijana wengi,job aache unafiki akae kutulia mana ametengeneza taifa la hovyo.
 
Acheni unafki huyo ni spika aliyefurushwa na sio mstaafu... bodaboda hawajalaaniwa ila waliofukuzwa kwenyevyeo ndiyo!

Sasa hivi anafungua vimigahawa navimamalishe huko vijijini? Amakweli roho mbaya hainaga uchoyo hukulipa ustahilicho...

Hata umaskini ni laana walakini maskini sio kwamba wamelaaniwa tatizo bongo akili ndogo zinakalia viti vikubwa kisa mdomo na kujipendekeza
 
Kama wafanya kazi mazingira magumu kwa afya yako, kazi ambayo hauna uhakika wa kurudi nyumbani, kazi ambayo huna uhakika wa matibabu na wanasiasa wako upande wako, jua kabisa wewe ni daraja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Risk imetuzunguka kila mahali, hata ukipanda balloon kwenda kazini kwako bado upo kwenye risk ya ajali tu, no safe zone, hata unaweza unatembea kwa miguu ajali ikakufuata hapo ulipo,
KAZI NI KAZI.
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Job Ndugai amewataka Watanzania kuacha tabia kutothamini mafanikio au juhudi za watu mbalimbali wanazozionesha katika taifa hasa katika sekta ya biashara, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mgahawa wa Chakula katika Taarafa ya Pandambili Iliyopo njia Kuu ya Kutoka Dodoma Owenya Morogoro.

Amesema "Kijana anza kufanya biashara halali, kazi ni kazi, achaneni na yule anayesema watu wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye, yule anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa, sasa ule si wenzawazimu tu."

Chanzo: GlobalTV
Hata mimi naungana na Lema, kazi ya Bodaboda sio ya staha (descent). Ni vile tu kijana anamaliza chuo hana mishe ya kufanya anaingia kwenye shughuli ya Bodaboda. Halafu mbona hatuwaoni watoto wa vigogo wakifanya shughuli za Bodaboda, walau hata mtoto wa DC.
 
Risk imetuzunguka kila mahali, hata ukipanda balloon kwenda kazini kwako bado upo kwenye risk ya ajali tu, no safe zone, hata unaweza unatembea kwa miguu ajali ikakufuata hapo ulipo,
KAZI NI KAZI.
Nadhani mchangiaji alimaanisha probability ya kupata ajali ni kubwa kwenye Bodaboda ukilinganisha na ya kwenye Balloon unayosema wewe.
 
Jobu Ndugai mgogo halisi! Anaakili njema kuliko Lema

Lema wa kabla ya kupanda pipa kwenda ughaibuni, alikuwa mtu sahihi! Sielewi huyu aliyerudi, sijui kimerudi kimvuli Chake na Lema halisi kubaki huko Canada!! 🤗
 
Lema ameishi Ulaya mwka tu amepoteza reality ya Tanzania, ameshau haraka sana maisha ya mtanzania anataka watu waishi kama Dunia ya kwanza bila mchakato wa maendeleo jambo ambalo haliwezekani, hata hizo boda boda Miaka ya 90 mtu kumiliki tu kama usafiri binafsi ilikua sio rahisi

Bodo bodo kama Wanapata hela waizitumie kama mbegu ya kuboresha maisha Yao hapo mbeleni kwa kuwekeza kwenye kazi zenye staha zaidi.
 
Back
Top Bottom