Ndugai akiwa hana madaraka ana akili sana na busara zote na heshima zote na anaongea vitu very clear, Ila sasa akipewa tu madaraka analewa madaraka alafu anakuwa mjinga sana na kuwa Mungu mtu, tena atakupiga na rungu kubwa kichwani na matusi kibao, atakwambia nitakuua mbwa wee na hatanii atakuua kweli na atakwambia chezea kitu kingine, sio Ndugai, yaani hatari sana huyu akiwa na madaraka.
Ila sio Ndugai tu, wengi wa watanzania washamba wakiwa hawana madaraka wanaongea na kuonekana watu wenye akili na busara sana, balaa apate madaraka au fedha nyingi, wanakuwa wajinga sana na wanaota mapembe na mabega wanatembea juu juu, hata ardhi hawaoni wanapokanyanga, yaani wanaona watu wengine ni takataka baada ya madaraka, hili ndio kosa kubwa sana binadamu tunafanya...
Binadamu halisi utamjua baada ya kupewa madaraka au awe na fedha nyingi, je atalewa ufahari au fedha na kuona wengine ni takataka au atajiona yeye ni Mungu mtu, so hicho ndicho kipimo halisi cha binadamu wa kweli.