Uchaguzi 2020 Job Ndugai asema CCM inahitaji 2/3 ya wabunge ili tuamue chochote kinacholetwa na Serikali

Uchaguzi 2020 Job Ndugai asema CCM inahitaji 2/3 ya wabunge ili tuamue chochote kinacholetwa na Serikali

Ndungai yuko desperate, anajua uspika unaenda kwa tall-lady.
 
Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM huwa wanapitisha miswada kwa kufuata mkumbo! Pia kuna mambo hata kama ni ya msingi ila kwakuwa yameongewa na mpinzani basi wanayafukia!Mifani michache ni hii.

*Zitto na hoja ya mikataba ya madini na mrahaba(hapa alifukuzwa hadi bungeni kwa miezi minne)!Baadae akaibuka shujaa!

*Mbatia na hoja ya mitaala(hapa alipigwa vita ila baadae kikaeleweka).

*Mnyika na hoja ya maji.

*Kafulila na hoja ya Escrow
 
Sasa huo wingi wao una faida gani maana wengi wao huwa wanawaza waganga wapya na hirizi za kujilinda dhidi ya maccm menzao
 
Spika Sitta R.I.P katika bunge lake alizingatia sana Ubora ( Quality) na Viwango ( standards) lakini inavyoonekana Spika Ndugai msisitizo wake uko kwenye Quantity (wingi) wa wabunge wa CCM...
Nilishasema ccm una akili peke yako.
 
Ndugai anajinasibu kutaka kujenga bunge linalojiweka chini ya serikali na linalowakilisha serikali na maslahi yake badala kuisimamia serikali na kuwakilisha wananchi na maslahi yao!!!

Spika Sitta R.I.P katika bunge lake alizingatia sana Ubora ( Quality) na Viwango ( standards) lakini inavyoonekana Spika Ndugai msisitizo wake uko kwenye Quantity (wingi) wa wabunge wa CCM...
Inawezekana Ndugai anajifanya hajuwi mfumo na anafikiri kile anakiwaza kitakuwa rahis ila nataka kusema amini amin na waambia ole wake aletae makwazo maana MTU huyo imempasa kufungwa Jiwe kubwa nakutupwa baharini...
 
Wanataka wapitushe uongozi wa kiimla. Mark this post
 
Nipo pembeni nimejibanza nakunywa Alkasusi, nakumbuka maneno ya Pro-Chadema dhidi ya Jk, kuwa rais dhaifu anacheka cheka tu.
 
"Mimi kama Spika katika demokrasia ya Kibunge suala siyo ujuzi wa kusema na kupanga hoja, ni muhimu sana Wabunge wa @ccm_tanzania wakazidi theluthi mbili ya Wabunge wote ili tuweze kuamua jambo lolote linaloletwa Bungeni na Serikali yetu" - Spika Ndugai.

#UzinduziKampeniCCM https://t.co/qf2YzvUA24

Sasa naamini hizi figusu kumbe lengo wapate wabunge wa kwenda kubadili katiba na mtu kuwa rais wa milele na zanzibar ndio kwa heri ya kuonana.
Ndio maana wanachukulia mezani
 
Hawawezi kuthubutu kuongeza muda, hata Magufuli alishakataa hiyo kitu, wanapenda kujaza bunge kwasababu tu ya tabia yao ya uroho wa madaraka.
Kama wameweza kupitisha wagombea bila kupingwa hilo la katiba linawezekana kabla jogoo hajawika asubuhi
 
"Mimi kama Spika katika demokrasia ya Kibunge suala siyo ujuzi wa kusema na kupanga hoja, ni muhimu sana Wabunge wa @ccm_tanzania wakazidi theluthi mbili ya Wabunge wote ili tuweze kuamua jambo lolote linaloletwa Bungeni na Serikali yetu" - Spika Ndugai.

#UzinduziKampeniCCM https://t.co/qf2YzvUA24

Sasa naamini hizi figusu kumbe lengo wapate wabunge wa kwenda kubadili katiba na mtu kuwa rais wa milele na zanzibar ndio kwa heri ya kuonana.

Hivii bado Ndugai ni spika wa bunge ;a JmT?
 
Unajua ccm hawawezi tena kufanya uchaguzi ?

Lakini kuna kundi kubwa sana linalomzunguka Magufuli limejaa wanasiasa wajinga wajinga na wenye uchu na madaraka tu.

Nchi sasa hivi haina viongozi ina wahuni tu sasa wahuni watashindwa kubadili katiba ?
Huyo Magufuli akijaribu hilo atakumbana na upinzani toka ndani ya chama chake, na nje, type za kina Membe zitaibuka tena, ukiongeza na presha toka nje hataweza himili.

CCM wataendelea kuiba kura na kulindana mpaka pale watz tutakapoamka tuwafurushe kwa nguvu, lakini sio kwa box la kura.
 
Ikiwa kweli ndio mpango wao wa kufanya watakayo na kuna watu wanajua wanapaswa kufanya nini na wakakaa kimya tu, basi kama inakula kwetu wakulima wa kawaida basi itakula hata kwake yeye anayejiona yuko salama.
 
Sidhani, pressure watakayoipata toka ndani na nje hawataweza ihimili, kama Amsterdam pekee anawapelekesha wataweza kukabiliana na serikali za mataifa ya magharibi ambao ndio wafadhili?! Never.

Mbona Kagame na Museveni wameweza? Au kwa nini Putin aweze hawa washindwe? Hapa ni wananchi ndio wanatakiwa wasimame kidete wakisaidiwa kwa karibu na vyombo vya usalama.

Ila vyombo vya usalama vikisapoti haya, I tell you ktk nchi yetu hii tunaenda kuwa na tofauti kubwa sana kati ya mwenye nacho na asiyekuwa nacho.

Vilivyotokea awamu ya kwanza, itakuwa ni cha mtoto, maana miungu watu watakuwepo wengi wasiogusika na wenye kinga kuwalinda.
 
Huyo Magufuli akijaribu hilo atakumbana na upinzani toka ndani ya chama chake, na nje, type za kina Membe zitaibuka tena, ukiongeza na presha toka nje hataweza himili.

CCM wataendelea kuiba kura na kulindana mpaka pale watz tutakapoamka tuwafurushe kwa nguvu, lakini sio kwa box la kura.
Hakuna mwanaccm wa kumkoromea Magufuli mle ndani.

Usichokijua ni kwamba ccm imejaa wanawake watupu mbele ya mwenyekiti wao.

Wanachokilinda kwa nguvu zote wanaccm ni kula yao na wakitoka ccm hawana ulaji tena.

Narudia tena hakuna mwanaccm wa kumfanya chochote mwenyekiti wao Magufuli hata akitaka awabadili jinsia hakuna wa kumbishia wote wataitikia kwa makofi.
 
Huyo Magufuli akijaribu hilo atakumbana na upinzani toka ndani ya chama chake, na nje, type za kina Membe zitaibuka tena, ukiongeza na presha toka nje hataweza himili.

CCM wataendelea kuiba kura na kulindana mpaka pale watz tutakapoamka tuwafurushe kwa nguvu, lakini sio kwa box la kura.
CCM mwenyekiti wao ni Mungu wao sasa wataweza kumbishia Mungu wao ??
 
"Mimi kama Spika katika demokrasia ya Kibunge suala siyo ujuzi wa kusema na kupanga hoja, ni muhimu sana Wabunge wa @ccm_tanzania wakazidi theluthi mbili ya Wabunge wote ili tuweze kuamua jambo lolote linaloletwa Bungeni na Serikali yetu" - Spika Ndugai.

#UzinduziKampeniCCM https://t.co/qf2YzvUA24

Sasa naamini hizi figusu kumbe lengo wapate wabunge wa kwenda kubadili katiba na mtu kuwa rais wa milele na zanzibar ndio kwa heri ya kuonana.
Hapo unajitengezea mambo tu; hakuwa na maana hiyo na elewa kuwa mabadiliko ya katiba siyo rahisi kama unavyodhani, yeye alisema kuhusu mandate ya kutoa maamuzi. Hata Marekani huwa nao wanapiga kampeini kuwa tunataka chama chetu kiwa na maseneta 60 ili tuweza kuwa na mandate ya kuamua lolote bila mapingamizi.
 
Back
Top Bottom