Uchaguzi 2020 Job Ndugai asema CCM inahitaji 2/3 ya wabunge ili tuamue chochote kinacholetwa na Serikali

Uchaguzi 2020 Job Ndugai asema CCM inahitaji 2/3 ya wabunge ili tuamue chochote kinacholetwa na Serikali

Wabunge wa ACT pemba wanatolewa ili bunge la CCM tupu Mzee meko atawale mpaka kifo
 
Kuna taratibu miiko na sheria .Sheria mbaya na viongozi wabaya hupatikana pia.Ndugai ni mmoja wa viongozi ambao sijawahi kumweleww kabisa.

Ila kwasasa sheria za nchi zinageuzwa geuzwa tu..wasisukume watu kwenye mambo mabaya ya hovyo.
 
Inawezekama Ndugai anatoa siri kiujanja kwa watanzania anajua kinacho endelea.

Na kupelekwa mwinyi Zanzibar ni kazi maalum.

Kuigeuza Zanzibar mkoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi kuthubutu kuongeza muda, hata Magufuli alishakataa hiyo kitu, wanapenda kujaza bunge kwasababu tu ya tabia yao ya uroho wa madaraka.

Kwani ikiongeza muda kuna ubaya gani ? mradi aongeze kisheria. Katiba sio msahafu au bilbia.
 
Hakuna mwanaccm wa kumkoromea Magufuli mle ndani.

Usichokijua ni kwamba ccm imejaa wanawake watupu mbele ya mwenyekiti wao..

Mnataka wana CCM wamfanye nini Magufuli? wakati ninyi mnatuambia yeye muoga, myonge, dahifu kwa sisi wanachama na wapenzi tumeridhika na myonge wetu.

Na nyinyi mnaendelea na mapenzi yenu kwa Mbowe mpenda Faru John na pupuchi , endeleeni taabu iko wapi?.
 
"Mimi kama Spika katika demokrasia ya Kibunge suala siyo ujuzi wa kusema na kupanga hoja, ni muhimu sana Wabunge wa @ccm_tanzania wakazidi theluthi mbili ya Wabunge wote ili tuweze kuamua jambo lolote linaloletwa Bungeni na Serikali yetu" - Spika Ndugai.

#UzinduziKampeniCCM https://t.co/qf2YzvUA24

Sasa naamini hizi figusu kumbe lengo wapate wabunge wa kwenda kubadili katiba na mtu kuwa rais wa milele na zanzibar ndio kwa heri ya kuonana.
Kwani ukishachaguliwa na kuwa mbunge. Pale bungeni unakuwa mwakilishi wa nani. Unakuwa mwakilishi wa chama au wananchi waliokuchagua??. Kwa maneno ya Ndugai inamaana watakaochaguliwa na Wanacvm hawatakuwa wabunge wa wananchi, watakuwa wabunge wa chama na serikali hivyo hawataweza kuwatetea wananchi waliowachagua.

Watakuwa pale kwa ajili ya kupitisha sheria na posh zao kwa ajili ya matumbo yao na kupitisha sheria kandamizi dhidi ya wapenda demokrasia. Hivyo tunatakiwa kwa umoja wetu kuhakikisha opposition wanapata wabunge wa kutosha hili Tanzania iweze kupata watetezi wao wa kuwaletea maendeleo.

TUACHANENI NA CCM. CCM WAMESHAJIAKIKISHIA KUTOKUTETEA. AKINA NDUGAI WANATAKA KUPITISHA KILA KINACHOTOLEWA NA SERIKALI BILA KUFUATA SHERIA, WANATAKA KUBADILISHA KATIBA ILI MAGUFULI ATAWALE MILELE, WANATAKA KUIMEZA ZANZIBAR. TUNASEMA KWA HILI HAPANA TUNATAKA MFUMO WA SERIKALI IBADILIKE, TUNATAKA KATIBA MPYA TUANZIE ALIPOISHIA JAJI WARIOBA. HATUTAKI MATAMSHI YA ONE MAN SHOW
 
Ndugai lilikuwa kama zezeta, tokea amekatwa kichwa ameamua kulifukia kwenye mchanga anagugumia kimyakimya tu.
Bahati mbaya sana wananchi wengi wanadhani kuwa viongozi wao mifuko yao imejaa ili waanze kuwatumikia lakini wapi...kwa taarifa, nyie wananchi tambueni kuwa viongozi wenu mifuko yao hazijajaa bado ili waanze kuwarushia mabaki...na mbaya zaidi hakuna dalili ya mifuko kujaa leo wala kesho.
 
Back
Top Bottom