Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Ndugai ana hoja kubwa bahati mbaya watanzania hawapendi kufikiri wamempuuza sana, hatupendi kuchambua bali kushabikia.

Ndugai nasema ana hoja kubwa naomba ajibiwe kitaalamu, sitaki kuamini kuwa ndugai kajiropokea tu
Wajukuu watamsaidia kupata majibu
 
Hoja ya ndugui ni unafiki ...

Watanzania hatuwezi kukaa kujadili unafiki ....

Watanzania tunaakili Sana mseee[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Tupo zaidi ya million 56 ,inamaana wewe pekee yako ndio umeona ndugai anahoja ???[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Dah!
Ukweli mchungu!
 
Ukweli kwa sasa mama anasifia anaupiga mwingi lakini hali ni tete! Kwanza katika uongozi wake mimi siwezi kumsifia kwa lolote kwani ni mzembe kufatilia mambo ya kitaifa anawaamini watendaji wake huku wakimpa taarifa za uongo bila kuzifanyia kazi kwa sasa baadhi ya miradi haiendi ipasavyo, mheshimiwa raisi kwa muangalia yeye hana tabia za udokozi lakini hao vijana wake angewafatilia sana wasimpotoshe kwani kwa sasa malalamiko ni makubwa katika nyanja mbalimbali zinazohusu nchi.
 
There is a dark fate from the speech. Mpaka 2025 mengi yatatokea.
 
Kama Ndugai aliomba msamaha akasamehewa kwanini hakuna sehemu yoyote ya dunia hii iliyokiri kwamba yuko huko? Mbona kosa la Ndugai ni dogo kuliko la Mbowe lakini Mbowe tunaye mitaani yuko huru, kasamehewa (maana hawezi kushindikana kufungwa)?
 
Magaidi hutetewa mno
 
Halafu kuna watu walikuwa wanawadharau Wagogo! Ona sasa utabiri wa Job, na haya yanayotokea sasa!

Sema tu alizingua kuomba ule msamaha wake uliofeli. Bora angekomaa na msimamo wake mwanzo mwisho.
 
Halafu kuna watu walikuwa wanawadharau Wagogo! Ona sasa utabiri wa Job, na haya yanayotokea sasa!

Sema tu alizingua kuomba ule msamaha wake uliofeli. Bora angekomaa na msimamo wake mwanzo mwisho.
Ilibidi zombie msamaha ili kuokoa mafao yake.
La sivyo Nabii Ndugai angeambulia patupu.
 
Hao UN walipinga ujenzi wa bwawa la umeme kwamba ni kuharibu mazingira lakini sasa hivi wanapinga kuwahamisha wamasai ili kulinda mazingira!

Mtu mweusi amka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…