Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

 
Spika wa Bunge ameonya kitendo cha serikali kuendelea kutegemea mikopo kutoka nje kuendesha nchi kitu ambacho kimefanya deni la taifa kuwa kubwa maradufu "Ipo siku hii nchi itapigwa mnada,kopeni tu".

View attachment 2060343
Kati ya hizo pesa za mikopo tunamdai BILION 26 na ushee zilizotumika kumtibia maradhi yake India na kumfanya kuwa mgonjwa ghali zaidi duniani anayetarajiwa kuingia kwenye kitabu cha Guiness book of world records
 
Suala la msingi siyo deni limetoka wapi, bali pesa zilizokopwa zimetumikaje. Kama kuna miradi inayowiana na deni husika, nasema wazi kama chenga na shuti za Ronaldo: ^Heri deni refu lenye tija kuliko mrundikano bubu wa makaratasi pale BOT.^
 
1. Mama anaonewa maana ni wazi madeni makubwa aliyaleta mwendakuzimu.
2. Spika ameonyesha waziwazi hayuko pamoja na mama, sio tu leo, hata 2025.
3. Mama amezungukwa na wengi ambao hawataki afanikiwe na hapa ni kama amechelewa kuchukua hatua.
4. Spika ameshtukia bungeni hamna issue na ameamua kufanya siasa mtaani kama wanasiasa wengine ili awe relevant, kama tu Polepole alivyokuwa anafanya.

Ila ujumbe wa spika ni wa msingi sana na niwakuzingatiwa sana... sema tu, kama kawaida ujumbe hautaangaliwa na ataangaliwa spika.. na ni haki aangaliwe maana kwa muda mrefu amekuwa bendera fuata upepo..hajawahi kuwa consistent!
 
Huenda kavuta harufu ya mtu wa Zanzibar kuwa spika huko mbele,kaamua kumwaga mboga.
Hangaya akiendelea kuwepo na kutaka kutawaka si ajabu akawepo na rais hajaye baada ya Hangaya akawa Mzanzibar wakaendelea kulithishana, watakuja kustuka sekta zote za juu wamejaa wazanzibar
 
Sasa wahuni wameanza kutoka mapangoni. Ni mwendo wa kamati, kamati, kamati. Ndiyo maana hakuna haja ya kuwa na viongozi husika kama kuna uteuzi mwingine wa kamati. Nonsense!

#^Car-taaWar-who-knee^
 
Back
Top Bottom