Job Ndugai ni Shujaa wa Historia-Anatuonesha Matobo na Udhaifu wa Samia Suluhu

Job Ndugai ni Shujaa wa Historia-Anatuonesha Matobo na Udhaifu wa Samia Suluhu

Kumbuka pia huku vijijini watu tunatozwa michango ya maendeleo ya kufa mtu nchi hii ni hatari
Watanzania tuache kupenda vya bure , haya nchi hii nikubwa sana na tunazid kuzaliana huwe tegemea kila kitu serikali ikufanyie huo ni ujinga kuna mazingira lazima uumie kwa ajili ya taifa
 
Huyu ni mnafiki na amelipwa laana alizozitenda sioni kama kuna chembe ya utetezi unatakiwa ufanywe juu yake na bado laana zimfike zaidi.
na Kuna mtu anaitwa Msajili wa vyama vya siasa Mutungi na yeye asubir laana za watanzania.
 
Watanzania tuache kupenda vya bure , haya nchi hii nikubwa sana na tunazid kuzaliana huwe tegemea kila kitu serikali ikufanyie huo ni ujinga kuna mazingira lazima uumie kwa ajili ya taifa
Siku zote ukiwa huishughulishi akili yako utakuwa unafikiri chini ya kiwango.
 
eti ndugey ni shujaa!!?.
giphy.gif
 
Tatizo la Ndugai ni kwamba alikuwa mlezi na wakati Fulani alikuwa kinara wa kufuja fedha za Umma.

Ndugai aliwakumbatia wabunge ambao hawatambuliki na Chama chao,wala majina yao hayakuwasilishwa na Katibu mkuu wa Chama chao,lakini aliendelea kuwalipa fedha za walipa kodi.

Madege yalinunuliwa na hayati Magufuri bila Bunge kupitisha na wala kujua gharama zake,lakini Ndugai alimuunga mkono katika yote hayo.

Ndugai na Magufuri walifikia kuunda umoja wao husio rasmi wazi wazi wa kuwashughulikia wapinzani.Kwamba wewe washughulikie Bungeni Mimi niwashughulikie huku nje,na walifanya hivyo.

Ndugai anaweza kuwa na hoja nzuri tu lakini hakuwa na moral authority ya kuisimamia.
 
Kama bunge lingekuwa na wabunge wa upinzani, Ndugai asingejiuzulu maana angejua anao wa kuunga mkono hoja yake ya mikopo.
Kikatiba Spika anaweza kuondolewa iwapo theluthi mbili ya wabunge itamkataa. Lakini kwa kuwa Bunge lina wabunge wa ccm ambao wanajua kuwa rais ambaye ndiye mwenyekiti wao ndiye roho yao ya kuwa pale bungeni, na hivyo lazima wakubaliane nae kwa kila jambo, hakuwa na option nyingine tofauti na kujiuzulu au asubiri kuondolewa na Bunge
 
Siku zote ukiwa huishughulishi akili yako utakuwa unafikiri chini ya kiwango.
Yaan hapa wewe ndio unaonekana mjinga, inamaana wewe hutaki kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi yako hivyo umebweteka kusubiri serikali ikufanyie kila kitu.
 
Yaan hapa wewe ndio unaonekana mjinga, inamaana wewe hutaki kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi yako hivyo umebweteka kusubiri serikali ikufanyie kila kitu.
Kaa na utahira wako maana inaonekana ni mchumia tumbo wewe
 
Ndugai hoja yake ni nzuri sn tatizo la Ndugai ni ukatili wake na maovu
Hoja yake ni nzuri kweli sema uwasilishaji wake ndio haukuwa sawa angeongelea mikopo kwa ujumla sio kumshambulia Samia na hizi 1.3bn. Na aliongea kwa kibri sana pia body language yake ilionyesha dharau ya wazi wazi.
 
Ni kweli Ila ndugai Ana mabaya yake.mengi tu.
Mwanzo aliona nini leo kaona nini?
ebu tukumbuke miaka 5 nyuma ndugai alikuwaje kwanini iwe Leo ndo kaja kuyaona hayo aliyoyaona?
Anamchukia Samia?
Kwanini huu mnaouita utetezi wa raia aje kuufanya kipindi Cha Samia?
Unajua watu wangapi wameteseka kipindi Cha magufuli na yeye akiwa spika wa bunge?
Aliongea nini?
yaani mateso ya watu na vifo vya watu havikuwa na umuhimu Ila mikopo ya Samia ndo Ina umuhimu?
TUACHE UNAFIKI SIMUONEI HURUMA NDUGAI HUYO ATAPANDA ALICHOVUNA
Kipindi cha mwendazake hakukuwa na tozo ila kwa sasa tuna tozo lukuki, sasa kama tunatozwa kila uchwao kwa nn serikali iendelee kukopa mamikopo makubwa makubwa basi tozo waziondoe ili tuendelee kukopa. Ukimsikiliza vzuri bila kuwa na chuki utaiona point yake.
 
Hatukuwa na TOZO Ila kulikuwa na mateso lukuki na spika wa bunge alikaa kimya.
Watu waliteswa,kupigwa, kufilisiwa kutekwa
Yaani mikopo ya Samia inamuumiza sanaaa kuliko maishaa ya watu na mateso yao?
Kipindi cha mwendazake hakukuwa na tozo ila kwa sasa tuna tozo lukuki, sasa kama tunatozwa kila uchwao kwa nn serikali iendelee kukopa mamikopo makubwa makubwa basi tozo waziondoe ili tuendelee kukopa. Ukimsikiliza vzuri bila kuwa na chuki utaiona point yake.
 
Kaka tatizo la watanzania wengi uwezo wao wakufikiri ni mdogo sana. Kila kitu kimegeuzwa ni siasa kuchafuana ukisema ukweli unachukiwa ukisema uongo unashangiliwa ni taabu tupu.

Nimefatilia mijadala mingi kwenye mitandao kabla spika hajachukua uamuzi wa kuachia ngazi.

Wako wengi walimshauri ajiuzuru kulinda heshima Yake. Lakini chakushangaza baada ya kuomba kuachia ngazi hao hao tena wamegeuka kwenye mitandao na kuanza kumkejeli sasa najiuliza hivi Tanzania tuna wapinzani hau vioja vya upinzani?

Mimi naamini upinzani wa kweli utatoka ndani ya chama cha mapinduzi lakini hawa wapinzani bado hawaja tambua nini maana ya upinzani.

Nimakizie kwa kuunga mkono Mh Spika mstaafu na alichokiongea ni ukweli mtupu. Nayeye kama kiongozi wa bunge Anawakilisha wananchi ambao mikopo inayokopwa kwa kulazimisha itawaumiza wananchi moja kwa moja katika kuilipa.

Pia watanzania nilazima tuwe makini na wahuni maana kama bunge litaongozwa na watu wasiolitakia mema taifa tujue sheria kandamizi zitaanzia hapo hivyo tuachane na siasa za kijinga na tushikamane kutetea watanzania wanyonge ambao Magufuli aliwapigania kwa nguvu zote.
 
Ccm wanashangalia kuanguka kwa ndungai wanasahau tayar alishamwanga Mchele kwenye kuku wengi, Na wanasahau ni kwa jinsi gani Watanzania wameumia kuhusiana na Tozo hizi
 
Mleta mada omba sana hekima na busara maishani mwako, sidhani kama unajua ulichoandika utashi ni sifuri.
Anyway, huenda umeandika kwa mihemko.
 
aliyasababisha mwenyewe kwa udhaifu wake wa kuitetea serikali badala ya kuisimamia na kuishauri
both mkuu wa mahakama na mkuu wa bunge wamekua wakijipendekeza mnoo kwa serikali ndiyo maana wakijaribu kutimiza wajibu wao kama mihimili inayojitegemea wanakua wanaonekana wamesaliti serikali.

Katiba mpya pekee ndiyo suluhisho la huu upumbavu wa bunge na mahakama kuwa wapambe wa serikali.
 
Ndugu zangu;

Kila nchi inakopa,na kila mkopo lazima utumike kikamilifu.Hata hivyo hii mikopo ambayo tunaaminishwa kwamba imetumika vizuri ni changa la macho.


IKO hivi.Idadi ya watu Tanzania ni Chini ya Milioni 60.Idadi ya shule ni chini ya elfu 20.Trilioni moja ni sawa na Bilioni 1000.Kamata Trilioni 1.3 ya covid imepelekwa kujenga madarasa,na TOZO ya uzalendo nayo imeenda kujenga madarasa basi inamaana yamejengwa madarasa ya thamani ya milioni 100 kwa kila moja ambayo ni sawa na madarasa 10,000.Kama kila darasa linakaa wanafunzi 40 inamaana wanafunzi laki nne na zaidi wamejengewa madarasa mapya.

Katika hali ya kawaida unaweza fikiri kwamba JOB NDUGAI aliteleza ulimi aliposema kwamba TULIPITISHA TOZO ili TUPUNGUZE KUKOPA lakini MBONA bado TUNAKOPA?Ni swali la msingi sana.Kama serikali imeweka TOZO zenye majina tofauti na kila siku wanabuni majina mapya ya TOZO na kodi .JE inaleta PICHA gani iwapo tunaendelea kupewa mikopo yenye majina TOFAUTI?

Je serikali inafuja PESA zetu?TRA wanasema wamekusanya trilioni 11 kwenye miezi kama 6 iliyopita na wakati huo huo tumechukua mikopo ambayo ni sawa na kiasi hicho cha makusanyo ingawa miradi iliyofanywa bado haijafikia kiwango hicho cha cha makusanyo.JE nani muongo?

Binafsi naamini kabisa NDUGAI alisema ukweli wake na alichagua kuondoka kishujaa pamoja na kwamba alikuwa sehemu ya ufedhuli na unyonyaji.Huyu Ndugai alikaa India kwa Muda mrefu akitumia pesa za walipakodi kula RAHA ukiona mpaka amefikia hatua ya kufunguka UJUE kuna JAMBO

ANYHOW.Nfasi ya kazi ipo WAZI niwakumbushe tu wale vijana ambao wanao mpango wa kuwa SUPIKA kwamba nafasi iko wazi na mtu yeyote anaweza kugombea mradi tu kuwe na chama cha siasa kinachokudhamini..So muanze kazi mapema.
Hivi ni kwamba huwa hatuna kumbukumbu kabisa, hatufuatilii kujua au ni makusudi tuu mpendwa??? Fedha ya UVIKO ni kwaajili ya kumjengea madarasa???? Hebu muwe mnafuatilia ingia hata YouTube tuu ufuatilie ule mchanganuo uone madarasa ni asilimia ngapi ya ule mkopo!!!
Siamini kabisa kabisa kama hatuwezi kujua vitu kwa kiwango hiki?

Mimi kumbukumbu zangu ndogo tuu.. Fedha hizi zililenga sekta ya afya tuu.. Tena kununulia vifaa dhidi ya covid na chanjo tuu hayo ndio yalikuwa masharti ya IMF... Ila wao serikali wakajenga hoja nzito Kwa IMF ili fedha zitumike pia sekta nyingine kwa lengo Hilo Hilo la kupambana na UVIKO.. Walitumia akili ya Hali juu mno mno mimi sikuwahi fikiria Serikalini Kuna watu wanaweza kufikiria jambo jema kiasi hicho.
Maana sote tunajua yaliyofanyika kwa miaka mingi.
1.wamenunua vifaa tiba MRI kwa hospital zote za Kanda.
2.CT scans kwa hospital zote za mikoa.
3.xrays na ultrasound kwa hospital zote za wilaya
4.wamejenga hospital mpya, vituo vipya vya afya na zahanati sijui Mia ngapi?

5.Miradi mingi ya maji vijijini kupitia RUWASA ni vijiji vingi sikumbuki data tufuatilie ule mchanganuo.

6.wamenunua mitambo ya uchimbaji visima.

7.Wamepeleka fedha nyingi TARURA kwaajili ya barabara vijijini na hasa madaraja.

Nilikuwa juzi juzi Katavi, Songwe na Mbeya wilayani na vijijini kwenye project fulani..

Aisee nilishangazwa na hii Habari ya fedha za UVIKO.. Kila sehemu umefanya miujiza.. Madarasa, zahanati au kituo cha Afya, barabara au daraja na miradi ya maji.

Ukitaka ujue kwanini wabunge wamemuandama Spika badala ya kumtetea waulize hiyo fedha imefanya nini kwenye majimbo yao utashangaa mno. Mbunge huwezi mwambia kitu juu ya fedha za UVIKO zimewapa mileage kubwa mno mno kwa wapiga kura wao.

Mtafute Diwani yeyote muulize juu ya fedha za UVIKO utaduwaa. Ni kweli haijawahi tokea toka mimi nipate akili.

KAMA MIKOPO YOTE ILIYOWAHI KUKOPWA HUKO NYUMA INGETUMIKA KWA MCHANGANUO HUO NA KWA UWAZI KAMA HUU. NDANI YA MIAKA 10 TUU TANZANIA INGEKUWA NCHI ILIYOENDELEA KULIKO ZOTE AFRICA.. HASA KWA HUDUMA NA MIUNDOMBINU YA KUTOLEA HUDUMA.

FEDHA ZA TOZO ZINAFANYA KAZI KWENYE SEKTA HIZO HIZO. NA UKIENDA KWENYE HIZI HALMASHAURI ULIZA MKITI AU DIWANI ATAKWAMBIA.. KATA YANGU NIMEPATA FEDHA YA TOZO MILIONI SIJUI 80.KUJENGA VYUMBA 4 VYA MADARASA, MILIONI 50 SIJUI ZAHANATI YA WAPI? SH. KUUNGANISHA BARABARA YA KIJIJI FULANI.
LAKINI MWISHO ATAKWAMBIA FEDHA ZA UVIKO TUMEPATA MILIONI 400..KWAAJILI YA MADARASA SIJUI MANGAPI?
200.M KITUO CHA AFYA WAPI SIJUI?

FEDHA ZA TOZO NI CHACHE SANA.. ZIMEJENGA MADARASA 500 TUU KATI YA ZAIDI YA 10,000 YALIYOKUWA YANAHITAJIKA HARAKA KABLA YA HII JANUARI ILI WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA AMBAO NI TAKRIBANI MILIONI MOJA(yaani form 1 mwaka huu ni kama milioni). Na bado watoto wanaotarajiwa kuingia darasa la kwanza sijui ni milioni ngapi?

TUJIFUNZE SANA SANA KWA WENZETU WAKENYA. HATA WALIOMO HUMU JAMII FORUM YAANI WANAJUA KUTAFUTA DATA NA TAARIFA SAHIHI KWENYE SOURCE MBALIMBALI KULIKO SISI WATANZANIA NI WAVIVU WAVIVU MNO MNO MNO.

NI NGUMU SANA KWA MTANZANIA KU ARGUE NA MKENYA KWENYE LOLOTE MAANA SISI HUWA HATUNA DATA WALA TAARIFA BALI NI KUONGEA NA KUBISHANA KWA MIHEMKO BILA BASE YEYOTE.

MNISAMEHE SANA SANA KWA NILIO WAKWAZA. MIMI HUWA SIPENDI KABISA KUCHANGIA HUMU TENA MASUALA YENYE UELEKEO WA KIASIASA NDIO SIYAPENDI KABISA.

ILA KUNA WAKATI WATU HUWA WANAJADILI VITU VYA AJABU VISIVYO VYA KWELI KABISA NA WANAUNGWA MKONO SANA KWA SABABU HAKUNA ANAYEJISHUGHULISHA KUTAFUTA TAARIFA.

SIPENDI SIASA WALA WANASIASA. MAANA BADALA YA KUTOA HOJA NA KUJIBU HOJA HUWA WANASHAMBULIANA TU.
 
Back
Top Bottom