Ndugu zangu;
Kila nchi inakopa,na kila mkopo lazima utumike kikamilifu.Hata hivyo hii mikopo ambayo tunaaminishwa kwamba imetumika vizuri ni changa la macho.
IKO hivi.Idadi ya watu Tanzania ni Chini ya Milioni 60.Idadi ya shule ni chini ya elfu 20.Trilioni moja ni sawa na Bilioni 1000.Kamata Trilioni 1.3 ya covid imepelekwa kujenga madarasa,na TOZO ya uzalendo nayo imeenda kujenga madarasa basi inamaana yamejengwa madarasa ya thamani ya milioni 100 kwa kila moja ambayo ni sawa na madarasa 10,000.Kama kila darasa linakaa wanafunzi 40 inamaana wanafunzi laki nne na zaidi wamejengewa madarasa mapya.
Katika hali ya kawaida unaweza fikiri kwamba JOB NDUGAI aliteleza ulimi aliposema kwamba TULIPITISHA TOZO ili TUPUNGUZE KUKOPA lakini MBONA bado TUNAKOPA?Ni swali la msingi sana.Kama serikali imeweka TOZO zenye majina tofauti na kila siku wanabuni majina mapya ya TOZO na kodi .JE inaleta PICHA gani iwapo tunaendelea kupewa mikopo yenye majina TOFAUTI?
Je serikali inafuja PESA zetu?TRA wanasema wamekusanya trilioni 11 kwenye miezi kama 6 iliyopita na wakati huo huo tumechukua mikopo ambayo ni sawa na kiasi hicho cha makusanyo ingawa miradi iliyofanywa bado haijafikia kiwango hicho cha cha makusanyo.JE nani muongo?
Binafsi naamini kabisa NDUGAI alisema ukweli wake na alichagua kuondoka kishujaa pamoja na kwamba alikuwa sehemu ya ufedhuli na unyonyaji.Huyu Ndugai alikaa India kwa Muda mrefu akitumia pesa za walipakodi kula RAHA ukiona mpaka amefikia hatua ya kufunguka UJUE kuna JAMBO
ANYHOW.Nfasi ya kazi ipo WAZI niwakumbushe tu wale vijana ambao wanao mpango wa kuwa SUPIKA kwamba nafasi iko wazi na mtu yeyote anaweza kugombea mradi tu kuwe na chama cha siasa kinachokudhamini..So muanze kazi mapema.
Hivi ni kwamba huwa hatuna kumbukumbu kabisa, hatufuatilii kujua au ni makusudi tuu mpendwa??? Fedha ya UVIKO ni kwaajili ya kumjengea madarasa???? Hebu muwe mnafuatilia ingia hata YouTube tuu ufuatilie ule mchanganuo uone madarasa ni asilimia ngapi ya ule mkopo!!!
Siamini kabisa kabisa kama hatuwezi kujua vitu kwa kiwango hiki?
Mimi kumbukumbu zangu ndogo tuu.. Fedha hizi zililenga sekta ya afya tuu.. Tena kununulia vifaa dhidi ya covid na chanjo tuu hayo ndio yalikuwa masharti ya IMF... Ila wao serikali wakajenga hoja nzito Kwa IMF ili fedha zitumike pia sekta nyingine kwa lengo Hilo Hilo la kupambana na UVIKO.. Walitumia akili ya Hali juu mno mno mimi sikuwahi fikiria Serikalini Kuna watu wanaweza kufikiria jambo jema kiasi hicho.
Maana sote tunajua yaliyofanyika kwa miaka mingi.
1.wamenunua vifaa tiba MRI kwa hospital zote za Kanda.
2.CT scans kwa hospital zote za mikoa.
3.xrays na ultrasound kwa hospital zote za wilaya
4.wamejenga hospital mpya, vituo vipya vya afya na zahanati sijui Mia ngapi?
5.Miradi mingi ya maji vijijini kupitia RUWASA ni vijiji vingi sikumbuki data tufuatilie ule mchanganuo.
6.wamenunua mitambo ya uchimbaji visima.
7.Wamepeleka fedha nyingi TARURA kwaajili ya barabara vijijini na hasa madaraja.
Nilikuwa juzi juzi Katavi, Songwe na Mbeya wilayani na vijijini kwenye project fulani..
Aisee nilishangazwa na hii Habari ya fedha za UVIKO.. Kila sehemu umefanya miujiza.. Madarasa, zahanati au kituo cha Afya, barabara au daraja na miradi ya maji.
Ukitaka ujue kwanini wabunge wamemuandama Spika badala ya kumtetea waulize hiyo fedha imefanya nini kwenye majimbo yao utashangaa mno. Mbunge huwezi mwambia kitu juu ya fedha za UVIKO zimewapa mileage kubwa mno mno kwa wapiga kura wao.
Mtafute Diwani yeyote muulize juu ya fedha za UVIKO utaduwaa. Ni kweli haijawahi tokea toka mimi nipate akili.
KAMA MIKOPO YOTE ILIYOWAHI KUKOPWA HUKO NYUMA INGETUMIKA KWA MCHANGANUO HUO NA KWA UWAZI KAMA HUU. NDANI YA MIAKA 10 TUU TANZANIA INGEKUWA NCHI ILIYOENDELEA KULIKO ZOTE AFRICA.. HASA KWA HUDUMA NA MIUNDOMBINU YA KUTOLEA HUDUMA.
FEDHA ZA TOZO ZINAFANYA KAZI KWENYE SEKTA HIZO HIZO. NA UKIENDA KWENYE HIZI HALMASHAURI ULIZA MKITI AU DIWANI ATAKWAMBIA.. KATA YANGU NIMEPATA FEDHA YA TOZO MILIONI SIJUI 80.KUJENGA VYUMBA 4 VYA MADARASA, MILIONI 50 SIJUI ZAHANATI YA WAPI? SH. KUUNGANISHA BARABARA YA KIJIJI FULANI.
LAKINI MWISHO ATAKWAMBIA FEDHA ZA UVIKO TUMEPATA MILIONI 400..KWAAJILI YA MADARASA SIJUI MANGAPI?
200.M KITUO CHA AFYA WAPI SIJUI?
FEDHA ZA TOZO NI CHACHE SANA.. ZIMEJENGA MADARASA 500 TUU KATI YA ZAIDI YA 10,000 YALIYOKUWA YANAHITAJIKA HARAKA KABLA YA HII JANUARI ILI WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA AMBAO NI TAKRIBANI MILIONI MOJA(yaani form 1 mwaka huu ni kama milioni). Na bado watoto wanaotarajiwa kuingia darasa la kwanza sijui ni milioni ngapi?
TUJIFUNZE SANA SANA KWA WENZETU WAKENYA. HATA WALIOMO HUMU JAMII FORUM YAANI WANAJUA KUTAFUTA DATA NA TAARIFA SAHIHI KWENYE SOURCE MBALIMBALI KULIKO SISI WATANZANIA NI WAVIVU WAVIVU MNO MNO MNO.
NI NGUMU SANA KWA MTANZANIA KU ARGUE NA MKENYA KWENYE LOLOTE MAANA SISI HUWA HATUNA DATA WALA TAARIFA BALI NI KUONGEA NA KUBISHANA KWA MIHEMKO BILA BASE YEYOTE.
MNISAMEHE SANA SANA KWA NILIO WAKWAZA. MIMI HUWA SIPENDI KABISA KUCHANGIA HUMU TENA MASUALA YENYE UELEKEO WA KIASIASA NDIO SIYAPENDI KABISA.
ILA KUNA WAKATI WATU HUWA WANAJADILI VITU VYA AJABU VISIVYO VYA KWELI KABISA NA WANAUNGWA MKONO SANA KWA SABABU HAKUNA ANAYEJISHUGHULISHA KUTAFUTA TAARIFA.
SIPENDI SIASA WALA WANASIASA. MAANA BADALA YA KUTOA HOJA NA KUJIBU HOJA HUWA WANASHAMBULIANA TU.