Unacho sema ni uongo mtupu au nawewe ni moja ya wanufaika wa hizo hela kwa njia ya kifisadi. Madarasa unayo yasema tumetumia nguvu kubwa kabisa michango ya wananchi kufikia Renta alafu wanakumbia serikali itanamalizia kule juu.
Darasa moja lenye vyumba vinne unasomewa bajeti ya m.25 kama siyo kichwa cha mwendawazimu ni nini. Hizo zahanati unazo sema juzi tarehe 5 watu wamewekwa ndani kwa ajili ya michango kwamba hawajalipa
Leo mtu unakuja unamkosoa Ndugai kwa issue ya mikopo utakuwa na lako jambo. Kila binadamu anaudhaifu wake lakini kwenye hili Ndugai yupo sahihi. Tozo zipo na wametuaminisha zinajenga madarasa, mikopo ya nini? Kama tunaamua kujenga taifa letu wenyewe kwa nguvu zetu tuachane na mikopo ambayo itakuja kutuumiza baadaye.
Umefanya vyema kuanza kuweka data ulizo nazo. Sijajua ni Halmashauri ipi hayo yalipotokea. Ila tuache ushamba wa mtu akiwa tofauti na wewe unamwita fisadi sijui nini. Humu hata hatufahamiani Nani yupo wapi a nafanya nini?
Ndugai kwa kuongea kile unachokiamni wewe kuwa ni ukweli na kuwashambulia waliomdhihaki... Halafu ukasahau mimi nimefafanua yale yanayohusu mchanganuo wa hizo fedha upoje kuwa sio za madarasa tuu unaniita fisadi...
Sasa mpendwa wewe na hao wanaomshambulia Ndugai utofauti wenu ni nini?
Wote hamtaki kusikia nje ya yale mnayotaka muambiwe...
JE kama wewe ungekuwa kiongozi mkubwa na mimi nikaongea hivi kutoa ufafanuzi si ungeniua kabisa?
Ni somo kubwa sana kuwa tunataka wengine wakosolewe wasijibu ila sisi tukikosolewa ni mbogo kweli kweli.
Nimesisitiza juu ya takwimu na taarifa sahihi.
Kuwa fedha haikuwa kwaajili ya madarasa tuu kama mtoa hoja alivyochanganua juu ya matumizi ya hiyo 1.3 trioni kuwa inajenga madarasa sijui mangapi?
Mimi nimetoa mfano wa maeneo nilipitia tukiwa na shughuli nyingine kabisa nikakutana na hayo huko vijijini na mimi siishi hiyo mikoa na ni mara yangu ya kwanza kufika.
Hoja ni kujua tozo tunayoipigia chapuo inakusanywa sh. Ngapi ambazo zinaweza kufanya nini na nini?
Lakini kwa mimi ambae napenda sana kufuatilia taarifa sahihi na kutunza kumbukumbu najua ninachokisema.
Sipendi Siasa Maana zimejaa uongo na uzushi. Lazima uongo uwe ukweli na ukweli uwe uongo.
POLE KWA YOTE AMINI UNACHOAMINI MAADAM HAWEZI KUBADILI UHALISIA.
KWA SASA KWA TABIA ILIYOONESHWA TANZANIA.. TUTARUDI KULE KULE KWA VIONGOZI WETU KUKOPA MIKOPO MIKUBWA MIKUBWA NJE NA KUFANYIA WANAVYOONA WAO INAFAA KIMYA KIMYA. KAZI YETU ITAKUWA KULIPA TUU.
MAANA UKIWAAMBIA KAMA ILIVYOFANYIKA NI NONGWA. MBONA VIONGOZI MIAKA YOTE WALIKUWA HAWASEMI WAMEKOPA NINI? WAPI? KWAAJILI YA NINI? KWA RIBA GANI? KWA MIAKA MINGAPI? HAYAKUTUHUSU.
NISAMEHE NIMEJIINGIZA KWENYE JAMBO NISILO LIPENDA.