Job Ndugai: Sijamisi Uspika, nina amani, haya ni mapito katika maisha

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai amezungumzia maamuzi yake ya kutogomea Ubunge katika uchaguzi ujao akisema kuna watu wanapotosha kwa kuwa wanaona kuna jina lake.

Mbali nah apo ameulizwa kuhusu kama amemisi kiti cha Uspika ambacho alikuwa akikikalia kwa miaka kadhaa kabla ya kujiuzulu mwaka huu, amesema hajamisi kiti hicho.

“Hapana, ile ni huduma (Uspika), unafanya inapokuwa ni wajibu wako, Mtanzania mwingine anafanya inapokuwa wakati wake, nina amani nipo salama.”

Kuhusu kauli yake ya kutogomea uchaguzi ujao kutafsiriwa tofauti na baadhi ya watu, anasema:

“Ni kawaida yao wakiona kitu cha Ndugai lazima wapotoshe, jimboni kwangu wanaelewa hilo, nilichofanya niliwakumbusha tu kuhusu uamuzi wangu kuhusu kutogombea 2025, hilo jambo lilikuwepo na siyo jambo baya.

“Nikimaliza Ubunge tarudi kwenye asili yangu, nalima kidogo, nafuga kiasi, siyo kila jambo kuna nia mbaya, wito wangu tuwe na upendo, siyo kila jambo kupotosha, unafiki na kuchonganisha.”

Kuhusu kupotea kwake kipindi cha hapo kati baada ya kutangazwa kujiuzulu Uspika, Ndugai anasema:

“Ni maisha tu, ni sehemu ya mapito katika maisha, Mungu atajalia, ni vitu vya kawaida, tuendeleze umoja wetu lakini kubwa zaidi tuboreshe hali ya uchumi wetu, uchumi ya familia mojamoja… nawapenda sana Watanzania, viongozi wangu wa kitaifa mimi nawapenda sana na niwahakikishie hakuna sintofahamu yoyote kati yangu na Chama changu, ni mambo ya mitandao tu.”

CHANZO: JAHAZI – CLOUDS FM
Mzee ULIUACHA VIBAYA USPIKA ndio MAUMIVU ULIYONAYO

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Tangia uhuru, bunge la jamhuri halijawahi kupata spika wa hovyo kama marehemu andunje ndugai.
Kuwa binadamu. Unaona fahari kumuita mwenzako aliye mzima kuwa ni marehemu? Ndugu yangu wote pumzi tuliyo nayo ni kwa neema tu ya Mwenyezi Mungu. Huna la kujivunia
 
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai amezungumzia maamuzi yake ya kutogomea Ubunge katika uchaguzi ujao akisema kuna watu wanapotosha kwa kuwa wanaona kuna jina lake.

Mbali nah apo ameulizwa kuhusu kama amemisi kiti cha Uspika ambacho alikuwa akikikalia kwa miaka kadhaa kabla ya kujiuzulu mwaka huu, amesema hajamisi kiti hicho.

“Hapana, ile ni huduma (Uspika), unafanya inapokuwa ni wajibu wako, Mtanzania mwingine anafanya inapokuwa wakati wake, nina amani nipo salama.”

Kuhusu kauli yake ya kutogomea uchaguzi ujao kutafsiriwa tofauti na baadhi ya watu, anasema:

“Ni kawaida yao wakiona kitu cha Ndugai lazima wapotoshe, jimboni kwangu wanaelewa hilo, nilichofanya niliwakumbusha tu kuhusu uamuzi wangu kuhusu kutogombea 2025, hilo jambo lilikuwepo na siyo jambo baya.

“Nikimaliza Ubunge tarudi kwenye asili yangu, nalima kidogo, nafuga kiasi, siyo kila jambo kuna nia mbaya, wito wangu tuwe na upendo, siyo kila jambo kupotosha, unafiki na kuchonganisha.”

Kuhusu kupotea kwake kipindi cha hapo kati baada ya kutangazwa kujiuzulu Uspika, Ndugai anasema:

“Ni maisha tu, ni sehemu ya mapito katika maisha, Mungu atajalia, ni vitu vya kawaida, tuendeleze umoja wetu lakini kubwa zaidi tuboreshe hali ya uchumi wetu, uchumi ya familia mojamoja… nawapenda sana Watanzania, viongozi wangu wa kitaifa mimi nawapenda sana na niwahakikishie hakuna sintofahamu yoyote kati yangu na Chama changu, ni mambo ya mitandao tu.”

CHANZO: JAHAZI – CLOUDS FM
Kweli dunia tambala bovu, leo ndugai anahamasisha upendano.
 
Back
Top Bottom