Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Natazama 360 Clouds naona Hassan Ngoma anambana Spika maswali mpaka anajichanganya kuhusu suala la Mbowe.
Kuhusu sheria ya habari analalamika lalamika tu kuwa wapinzani wanapendelewa na mitandao ya kijamii na waandishi wa habari.
=====
Katika Mahojiano ya Spika Job Ndungai na Clouds Media, yaliyofanyika leo Nyumbani kwake Kisasa, Jijini Dodoma na Spika amesema haya;
Tulifika mahali ambapo live camera ikaliharibu bunge, watu wakawa wanatukana, wanakuwa na tabia mbaya. Unakuta mmekubaliana kabisa kwenye kamati kila kitu, jambo lile lile likiingia bungeni inakuwa kama mchezo wa kuigiza.
Hata kwa Mabunge ya nchi zilizoendelea kama Uingezereza si kweli kwamba ni live kihivyo, wanaicheleweshea kama dakika mbili au tatu kati ya kinachotokea live na kinachokuwa live wanajaribu ku-edit kidogo vitu ambavyo ni aibu kwa taifa.
Ni ukweli usiopingika kwamba yako mambo Watanzania hawayajui na huwa hatupendi sana kusema ni kweli baadhi ya wabunge na hasa hao wenye fujo baadhi yao wanatumia madawa ya kulevya, wanatumia bangi, baadhi yao wanakunywa konyagi au gongo gani, wanakuja pale sio yeye.
Tulifika mahali ambapo tumewafungia wabunge wengine mwaka mzima asirudi bungeni, mbunge mwingine mnampeleka kwenye kamati ya maadili anaenda anawaambia mimi nimefanya na nikipata nafasi narudia tena na msinisamehe na viadhabu vyenyewe kwenye vitabu ni vidogo.
Nitumie nafasi hii kuwaomba vyombo vya habari, tumekuwa tukikuza watu wa hovyo, waropokaji ndio wanakuzwa kuonekana ni heroes. Bahati nzuri naamini wapiga kura watawachuja watu wengi katika hawa maana hamna walichokifanya jimboni.
Hakuna ambalo sikufanya kumsaidia Tundu Lissu siku ya tukio nilikuwa Dar nilipotua Dodoma nikaenda Hospitali tuka-mobilize madaktari waliokuwepo Mhe Mbowe na wenzake wakasema si kweli kwamba hawaamini Muhimbili bali ili wapate amani ya moyo wanaomba wampeleke Nairobi.
Sijawahi kuongea na Tundu Lissu kwa simu kwa sababu namjua namfahamu vizuri ni mtu ana imani zake fulani na mapambano, ana ruti yake anayoiendea ambayo yeye ndio anaweza kuielewa vizuri zaidi na anaona sisi wengine ni mashetani, mtu aina hiyo unampa amani, unamuacha.
Bunge la 9 wakati wa kina Mzee Slaa palikuwa na wapinzani ambao walikuwa wakifanya kazi yao, walikuwa wanashusha hoja ambazo tukikaa pembeni kama CCM tunaambiana kuwa tunaharibiana.