yakowazi
JF-Expert Member
- Feb 9, 2012
- 1,765
- 624
anaona sisi wengine ni mashetani,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
anaona sisi wengine ni mashetani,
Spika-"S"Natazama 360 Clouds naona Hassan Ngoma anambana Spika maswali mpaka anajichanganya kuhusu suala la Mbowe.
Kuhusu sheria ya habari analalamika lalamika tu kuwa wapinzani wanapendelewa na mitandao ya kijamii na waandishi wa habari.
=====
Katika Mahojiano ya Spika Job Ndungai na Clouds Media, yaliyofanyika leo Nyumbani kwake Kisasa, Jijini Dodoma na Spika amesema haya;
“Tulifika mahali ambapo live camera ikaliharibu bunge, watu wakawa wanatukana, wanakuwa na tabia mbaya. Unakuta mmekubaliana kabisa kwenye kamati kila kitu, jambo lile lile likiingia bungeni inakuwa kama mchezo wa kuigiza” - Mhe Ndungai
“Hata kwa Mabunge ya nchi zilizoendelea kama Uingezereza si kweli kwamba ni live kihivyo, wanaicheleweshea kama dakika mbili au tatu kati ya kinachotokea live na kinachokuwa live wanajaribu ku-edit kidogo vitu ambavyo ni aibu kwa taifa” - Mhe Ndungai
“Ni ukweli usiopingika kwamba yako mambo Watanzania hawayajui na huwa hatupendi sana kusema ni kweli baadhi ya wabunge na hasa hao wenye fujo baadhi yao wanatumia madawa ya kulevya, wanatumia bangi, baadhi yao wanakunywa konyagi au gongo gani, wanakuja pale sio yeye” -Mhe Ndungai
“Tulifika mahali ambapo tumewafungia wabunge wengine mwaka mzima asirudi bungeni, mbunge mwingine mnampeleka kwenye kamati ya maadili anaenda anawaambia mimi nimefanya na nikipata nafasi narudia tena na msinisamehe na viadhabu vyenyewe kwenye vitabu ni vidogo” - Mhe Ndungai
“Nitumie nafasi hii kuwaomba vyombo vya habari, tumekuwa tukikuza watu wa hovyo, waropokaji ndio wanakuzwa kuonekana ni heroes. Bahati nzuri naamini wapiga kura watawachuja watu wengi katika hawa maana hamna walichokifanya jimboni” - Mhe Ndungai
“Hakuna ambalo sikufanya kumsaidia Tundu Lissu siku ya tukio nilikuwa Dar nilipotua Dodoma nikaenda Hospitali tuka-mobilize madaktari waliokuwepo Mhe Mbowe na wenzake wakasema si kweli kwamba hawaamini Muhimbili bali ili wapate amani ya moyo wanaomba wampeleke Nairobi”-Mhe Ndugai
“Sijawahi kuongea na Tundu Lissu kwa simu kwa sababu namjua namfahamu vizuri ni mtu ana imani zake fulani na mapambano, ana ruti yake anayoiendea ambayo yeye ndio anaweza kuielewa vizuri zaidi na anaona sisi wengine ni mashetani, mtu aina hiyo unampa amani, unamuacha”- Mhe Ndugai
“Bunge la 9 wakati wa kina Mzee Slaa palikuwa na wapinzani ambao walikuwa wakifanya kazi yao, walikuwa wanashusha hoja ambazo tukikaa pembeni kama CCM tunaambiana kuwa tunaharibiana” - Mhe Ndugai
MheshimiwaJob ndugai wiki iliyopita alifanya mahojiano na kituo kimoja cha Tv na alieleza mengi.Mawili mmakubwa ni kwa sababu za kuzuia bunge mubashara lakini la pili ni kukiri kwa kinywa chake kuwa kuna wabunge wanaotumia bangi na madawa ya kulevya.
Huyu ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa bunge la kumi na moja.
Kwa wahudhuriaje wa bunge tungeomba mtusaidie kukanusha au kukubaliana na hoja alizotoa.
Hivi aliposema ana faili mirembo, kilichompeleka mirembe ni nini< ua alikuwa mvutabangi ambayo ilimfanya kichaa?MheshimiwaJob ndugai wiki iliyopita alifanya mahojiano na kituo kimoja cha Tv na alieleza mengi.Mawili mmakubwa ni kwa sababu za kuzuia bunge mubashara lakini la pili ni kukiri kwa kinywa chake kuwa kuna wabunge wanaotumia bangi na madawa ya kulevya.
Huyu ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa bunge la kumi na moja.
Kwa wahudhuriaje wa bunge tungeomba mtusaidie kukanusha au kukubaliana na hoja alizotoa.
Mvuta bangi na kichaa nani ana nafuu?Sugu aliwahi kukiri anavuta bangi, sioni kosa la spika
Dawa za usingizi zilifyatua ubongoNdugai mjinga tu ....yeye ndo mvuta bangi asiyejuwa hata katiba ya nchi.
Mvuta bangi na kichaa nani ana nafuu?View attachment 1484921
Kumbe wewe zwazwa huyo andunje si amekiri mwenyewe hapo?Kichaa kama kichaa wanacho wabunge wa Chadema