Joe Biden asinzia wakati Makamu wa Rais Dkt. Mpango akizungumza

Wewe tukupe uongozi leo utakuwa na kasoro zako, blind spots zako labda utaangalia waliokuunga mkono ukawapa vipaumbele.
Mimi sitafuti uongozi wa nchi hii. Lakini nitakwambia waziwazi hapa, hayo ya upendeleo wa mtu, kundi maalum nje ya u-Tanzania wake hilo lisingewezekana kabisa. Sifa kuu ndani ya maisha yangu ni -u-Tanzania, na uwezo wa mTanzania yeyote kushika nafasi anayo pewa kuiongoza., basi.

Na pengine, ndiyo sababu siwezi kuwa kiongozi wa nchi hii, kwa sababu hizo hizo. I am too idealistic. But I don't regret it
 
Sasa Mr kalamu.kwanini huoni uzalendo wa Magufuli. Ni kujifanya kipofu tu, wakati mwingine inachangiwa na itikadi, udini ukabila wa watu. Ukiwa neutral ukiangalia aliyoyafanya kwa wananchi ni ukweli alikuwa mzalendo. Uzalendo nini. Ni kuangalia maslahi ya taifa,watu wote,kupata huduma zote kama haki, umeme, maji, barabara, masoko, kupunguza rushwa, SGR, NIDA, kuheshimika kwenye mamlaka.

Uzalendo ni nini kwa mwananchi wa kawaida? Kufanya nini ni uzalendo? Ni kusogeza huduma zote kwa kila mwananchi, tafsiri yako ya uzalendo ikoje?
 
Sasa Mr kalamu.kwanini huoni uzalendo wa Magufuli. Ni kujifanya kipofu tu, wakati mwingine inachangiwa na itikadi, udini ukabila wa watu. Ukiwa neutral ukiangalia aliyoyafanya kwa wananchi ni ukweli alikuwa mzalendo. Uzalendo nini.
Humo humo, ndimo palikuwemo na ubaya wa Magufuli, kwenye makundi hayo, na hadi leo ni baadhi ya hayo hayo yanayo zidi kutuumiza wakati huu chini ya Samia ambaye naye amekuja kuyatila mkazo zaidi.
Mimi nipo 'neutral' sana, ndiyo sababu niliona mapema sana baadhi ya mambo ya Magufuli yalikuwa siyo ya kizalendo.
 
May be you can not accept others people from different backgrounds, lower on your opinions background, interior background kuwa viongozi.

Mnahitaji makabila yenu, dini zenu, watu wenu. Hakuna tofauti na CCM. Genge flani, lenye itikadi flani linataka kuchukua nchi.
 
Uzalendo ni nini kwa mwananchi wa kawaida? Kufanya nini ni uzalendo? Ni kusogeza huduma zote kwa kila mwananchi, tafsiri yako ya uzalendo ikoje?
Hapana.
Leo hii tukipata mfadhili kupitia kwa Samia ili tujengewe kila kitu unacho kitaja hapo; mara hiyo Samia tayari amekuwa "Mzalendo'?
Uzalendo kwa nchi ni zaidi ya hivyo vitu. "Uzalendo haununuliwi"
 
Alikuwa na mapungufu yake. Ila positive kusaidia nchi, kujenga mifumo, miundombinu ya shule, barabara, hospitali, vivuko, SGR, hata negotiate mikataba yote toka uhuru vizuri sana, mnapata 40% ya share watu kwenye bodi. Usimamizi.
 
LOOOoooh!

Mbona sasa nashindwa kabisa kukuelewa mkuu 'Lookmasin'! Kwani nimeeleza kitu gani hapo juu, post mbli/tatu tu toka hapa tulipo sasa?
hata sielewi unacho lenga kueleza katika hii mistari miwili uliyo andika hapa. Sasa nianze upya kujieleza juu ya haya?
 
Hapana.
Leo hii tukipata mfadhili kupitia kwa Samia ili tujengewe kila kitu unacho kitaja hapo; mara hiyo Samia tayari amekuwa "Mzalendo'?
Uzalendo kwa nchi ni zaidi ya hivyo vitu. "Uzalendo haununuliwi"
Wewe unaweza kufanya hata kujenga shule tu, hospitali, barabara, kufukuza wala rushwa, kufuta mikataba dhalimu kama Barracks Gold na kuja na mikataba mpya.
 
Wewe unaweza kufanya hata kujenga shule tu, hospitali, barabara, kufukuza wala rushwa, kufuta mikataba dhalimu kama Barracks Gold na kuja na mikataba mpya.
EEEeeenHEEeeeee!
Basi bhwanah. Nadhani tumalizie hapa, maana sasa tunazungukia mle mle ambamo tayari tumekwisha elezana.

Mimi siwezi "kujenga shule" kwa sababu sina pesa ya kujenga na kuendesha shughuli hiyo; na wala sidhani kuwa Magufuli alikuwa akitoa pesa yake mfukoni kufanya hayo yaliyo amriwa kufanyika wakati wa uongozi wake.

Ni hivi, mkuu 'Lookmasin', mimi simwondolei sifa yoyote katika hayo mazuri aliyo onekana kuyafanyia maamuzi. Mimi pia niliyapenda. Tofauti yangu na wewe, nadhani ipo katika kufumbia macho mabaya aliyo yatenda.
 
Leta Alternative 2015 wakati CCM inakufa. Magufuli ndio alikomboa CCM. Ilibidi Lowassa apite, ila sera za JPM ndio ziliwapa CCM ushindi.

Na pia sera, mipango ndio imeipa nguvu CCM hadi leo kuondoa machafuko. Walionekana at least wanajali.
 
Leta Alternative 2015 wakati CCM inakufa. Magufuli ndio alikomboa CCM. Ilibidi Lowassa apite, ila sera za JPM ndio ziliwapa CCM ushindi.

Na pia sera, mipango ndio imeipa nguvu CCM hadi leo kuondoa machafuko. Walionekana at least wanajali.
Ukiniambia nilete 'Alternative', bila shaka ukiwa na maana mbadala wa CCM? Kwa rahisi tu nitakwambia, anything is better than having the current CCM. Hata kile chama cha mzee Rungwe kushikilia nafasi tukitafuta mbadala ni bora kabisa. Sababu ikiwa kwamba CCM haiwajibiki tena kwa waTanzania, bali CCM inawafanya waTanzania ndio wawajibike kwa serikali yao na wao, ili waendelee kuchafua bila kuhojiwa. Kwa maana hiyo ni kuwa CCM sasa kazi yake kubwa ni kubaki madarakani kutenda maovu dhidi ya waTanzania.
Chama kinacho wanyima waTanzania UHURU na HAKI ya kuchagua viongozi wanao wataka hakifai kuwa madarakani

Sasa naomba unielewe vizuri hapa kuhusu hiyo 'alternative' unayo nihimiza nikupe.
Waambie CCM wenzio huko ndani ya chama, ambao bado wanazo akili za kutambua chama kilipo sasa; fanyeni mageuzi huko huko ndani ya chama haraka, tuone juhudi zenu za kufanya hivyo, tukiridhika tutawaunga mkono. Vinginevyo, kama mtabaki kuwa viongozi wa kujitafutia maslahi yenu na kuuza watanzania kama bidhaa; mtatupeleka mahali pabaya sana kama nchi.
 
Ni hivi haku
Kwanza mimi ni mtu huru, sina chama. Naweza kuwa na maoni huru. Naangalia nia ya dhati ya mtu, ukweli. JPM sera zake alizuchuku nyingi chadema, ufisadi, rushwa, uchafu aliachukua kuukomesha Tanzania kwa watanzania wengi wa chini. Akaenda mbali zaidi kumomesha mikataba isiyo na kichwa wala miguu, kuinyonya Tanzania.

Vitu vichache akikosea kama wewe ambavyo ungekosea au Lissu, Mbowe, Zitto.
 
Unaweza kuwa "mtu huru" uliye uza roho yako kwa Magufuli, hii ipo wazi sasa.

Hivyo "vitu vichache unavyo sema alikosea", ndivyo vitu vinavyo mwondolea heshima na uzalendo unao mtakia akumbukwe juu yake.
Mimi siwezi kuwasemea hao wengine ulio wataja hapo; lakini nime kwisha kueleza vitu ambavyo nisinge vifanya, kama Magufuli alivyo vifanya. Hili ninalo uhakika nalo, kwa hiyo usining'ang'anize kuwa ninge fanya kama Magufuli alivyo fanya..

Tumalizie hapa, au unaonaje wewe?
 
Nafikiri huwezi kukubali ukweli. Kwenye hili taifa wangapi utasema wamejitahidi kulisimamia hili taifa? Au wewe ni kupinga tu.
 
Nafikiri huwezi kukubali ukweli. Kwenye hili taifa wangapi utasema wamejitahidi kulisimamia hili taifa? Au wewe ni kupinga tu.
Kwa vile "nina pinga" baadhi ya mambo ya Magufuli ambayo hayakuwa mazuri? Nitakubali sifa hiyo bila ya kinyongo.
nimejieleza vya kutosha kwako msimamo nilio nao, ambao hauyumbishwi na mtu yeyote.
"kwenye hili taifa" nimeeleza tayari ninao juwa bila ya shaka juu yao kuwa wamefanya kila walilo weza katika uongozi wao kwa manufaa ya taifa hili. kama matokeo hayakuwa kama yalivyo tegemewa, hilo ni jambo jingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…